Je Zitto Amepoteza Uhalali wa kuwa Kiongozi?


Wewe umeonyesha chuki kubwa kabisa kwa Kwayu kwa kutaja uchaga wake bila sababu yoyote ile (na wala bila kuulizwa). Wachaga wamekukosea nini?

Na pia, nani kakuuliza (au kataka kujua) kabila lako au la mke wako?
 

wewe tueleze mabaya aliyofanya Zitto alipokuwa kwenye hiyo kamati badala ya kuja na conspiracy theories ambazo nashindwa kuona vichwa chake. Haya mambo ya kuhesabu kamati na mafanikio yake hayahusiani na mada inayoonyesha kwamba Zitto hana sifa za uongozi.

Tafadhali, tupe kosa au ufisadi (kama upo) alioufanya Zitto akiwa kwenye hiyo kamati.
 
Ikumbukwe kwamba kazi kubwa ya upinzani ni kuweka checks and balance dhidi ya serikali, ushiriki wa Zitto kwenye kamati ile ulikuwa wa haki na ndio maana Chadema hawakuthubutu kumwadhibu kwa kushiriki kwake.

Kutomwadhibu Zitto (at least hadharani) haimaanishi kuwa Chadema walikubaliana na alichofanya Zitto. Zitto aliwauza watanzania na chama chake kwa kuingia kwenye kamati feki iliyoundwa kula pesa za wananchi ili kuzuia uchunguzi halali na unaojitegemea ambao ungefanyika na kulipatia ufumbuzi suala la Buzwagi na migodi mingine.

Zitto analijua hilo na ndio maana yuko kimya kabisa kuhusu Buzwagi ingawa anajua kabisa kuwa hakuna kilichobadilika.
 

Kwa kuanzia tu, ni kile ambacho Zitto hakufanya (au kamati haikufanya) kuhusiana na mkataba wa Buzwagi. Una jibu katika hilo?
 

Unajua kama wangeshindanishwa na Zitto akashindwa ndipo hii hoja ya iming kuwa mbovu ingekuwa na mshiko....lakini kitendo cha kuogopa ushindani kinatoa taswira tofauti....

Na hili la watu wengi sana CHADEMA lakini sio active katika politics ndio tatizo kiasi cha kupelekea kujengeka kwa muono kuwa katika chama kizima MBOWE ndio kimbilio. Sasa kama mngeacha kuwa timid and opportunists kama asemavyo Mbowe ni wazi CHADEMA wangekuwa mbali zaidi ya walipo sasa ambako wanalazimiko kuridhika with the least they can get.....

omarilyas
 
Mgonjwaukimwi,
Mkuu hapa nitatofautiana na wewe. Unataka kusema katiba ya Chadema inapiga marufuku kwa wanachama wake kufanya kazi serikalini? Mbona sikuelewi.
Hapana mkuu wangu kuna tofauti kubwa kati ya wawakilishi wetu (wabunge) na waajiriwa wa serikali kama vile tofauti ya Waziri wa wizara na Mkurugenzi wa wizara.. nikiwa na maana mkurugenzi wa wizara anaweza kutokuwa namwanachama wachama chochote cha siasa na akafanya kazi..lakini hai apply kwa waziri.

Sidhani kama JK anaweza kumchagua mtu toka toka Chadema awe waziri wa wizara fulani na ikakubalika ikiwa JK hakubaliani na sera wala mpango wowote wa chama ktk uendeshaji wa wizara hiyo. Pia haiwezekani mbunge wa Chadema, CUF au chama kingine kwenda kuwa waziri wa serikali ya Kikwete wakati hakubaliani na mrengo, sera za JK.. sijui atakuwa anajaribu kufanya kitu gani kama sii kuwa mtumwa na mgungwa wa utawala uliopo. Ingekuwa rahisi hivyo watu wasingekuwa na vyama vingi (demokrasia) au kuhama vyama ya nini ikiwa tunachohitaji ni vichwa vya watu kutunga Policy..
 
 

Ndiyo maana jana nilimshauri Zitto kuwa ajiunge na Swahiba wake (kikwete) kule CCM kwa mafisadi wenzake wa Dowans.
 
Mwafrika wa kike nadhani wewe ni kati ya wale wanawake wanaomburudishaga kaka Mbowe kwenye helcopter ili wapewe ubunge.....

Hili la kuita members wengine wa JF hapa wasiohusika na unachokiongelea na kuwatolea lugha ya upuuzi na utoto kama hii sidhani kama ina nafasi yake hapa JF.

jitahidi kuna nafasi moja ya wazi ya ubunge ya Muhonga ili safu ya wachaga na babab mkwe Mtei itimie

Mkuu, wachaga wataendelea kuwepo tu hapa Tanzania iwe unapenda au hupendi.
 

Mkandara,

Namba za JK kumpa Zitto nafasi ya uwaziri zimezidi kupanda hasa baada ya hili saga Zitto alilofanikiwa kulileta Chadema.

Itafikia wakati tu Kikwete alipe fadhila (na huo wakati unakaribia sana).
 
Mkandara,

Namba za JK kumpa Zitto nafasi ya uwaziri zimezidi kupanda hasa baada ya hili saga Zitto alilofanikiwa kulileta Chadema.

Itafikia wakati tu Kikwete alipe fadhila (na huo wakati unakaribia sana).
Hapana JK hana sababu wala haja ya kulipa Fadhila.. Zitto alifungashiwa kanyaboya akalikoroga na kulinywa mwenyewe kwa gharama ya Chadema.. madini yetu bado yanaibiwa, Kina Karamagi ndio imetoka tena basi nasikia Buzwagi barricks tayari wameisha anza ujenzi yaani mwaka wa hasara ni hasara tu..
Kifupi ningependa sana kumskikliza Zitto ni mabadiliko gani ya sera au hata policy za JK imebadilishwa kutokana na kuingia kwake ktk kamati hiyo. Ila sikupata nafasi hiyo kwani toka saga la Dowans mkuu amekuwa adimu hapa Kijiweni.
 
Nah,

Huyo Omar alishadai kuwa si mwanachadema. Nadhani hapa ni outsiders wanajaribu kuikaanga Chadema - na wamechemsha.

Wakati mnalamba mafuta ya Mengi na wengine wanopita kuimba ngonjera za nina imani na Kikwete hamkuona kuwa hao ni outsiders na wala hamkuuliza uswahiba wao?

Hao mnaowaita wachangiaji wenu kiuchumi ambao mnadai kuna umuhimu wa kumuacha Mbowe ili waendelee kukichangia chama chenu mbona hamhoji iweje wawachangine ninyi asilimia kuni na tisini wakizipeleka CCM?

Hivi kati ya Mbowe, Slaa, Mtei na Zitto ni nani mwenye historia ya kuwa CCM?

Achenu kutafuta mchawi kwa jirani wakati wachawi ninyi wenyewe.....

Kubaka na kudumaza demokrasia mfanye wenyewe halafu muanze kusingizia furaha ya CCM. Mlitaka wanune wakati mnajikaanga wenyewe...

omarilyas
 
Wakati mnalamba mafuta ya Mengi na wengine wanopita kuimba ngonjera za nina imani na Kikwete hamkuona kuwa hao ni outsiders na wala hamkuuliza uswahiba wao?

Hapa nitasubiria waliolamba mafuta ya Mengi na kuimba ngonjera za Kikwete wakupe jibu.

Hao mnaowaita wachangiaji wenu kiuchumi ambao mnadai kuna umuhimu wa kumuacha Mbowe ili waendelee kukichangia chama chenu mbona hamhoji iweje wawachangine ninyi asilimia kuni na tisini wakizipeleka CCM?

Haya ni mawazo yako binafsi kwa hiyo nitayachukuliwa kama ni udaku tu.


Wote hao walishakuwa CCM ila sasa Zitto yeye anataka kurudi CCM kwa kasi na mbwembe zote.
 

Mkuu Mkandara,

Issue ya Dowans ilikuwa si mchezo kwani ilimmamliza kabisa kijana wetu. Ni muda tu labda atakuja kuelezea ukweli kilichomtokea kwenye kamati hizo za Kikwete alizokuwa anahudhuria.
 
Kifupi ningependa sana kumskikliza Zitto ni mabadiliko gani ya sera au hata policy za JK imebadilishwa kutokana na kuingia kwake ktk kamati hiyo. Ila sikupata nafasi hiyo kwani toka saga la Dowans mkuu amekuwa adimu hapa Kijiweni.

Naungana mkono nawe kuhusu yeye kuelezea mabadiliko yaliyopatikana na nini ulikuwa mchango wake huko kama alivyofanya kule jimboni ambako tayari hao wanaodai ni maswahiba wake walikuwa kazini wakimwaga sumu...

Kuhusu saga la dowans kaka unategemea nini kama ukija unakutana na hoja kiduchu majungu bwelele. Na ukijibu kama wanavyopaswa kujibiwa unajikuta umefungwa minyororo ya haki ya kusema kama ilivyo....Yaani humu wamejaa watu wanaotaka useme kama watakavyo wao na sio vinginevyo. Watanzania tunapenda viongozi wanafiki wa kututongotongoza kama hao tulio nao sasa na wakitokea wenye style tofauti basi tunachokijua ni majungu, mipasho na visasi..


omarilyas

omarilyas

omarilyas
 
.....Haya...hebu tupate Tangazo la biashara kidogo.....
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=dBV6sh4cr2c[/ame]
 

Omar,

Acha jaziba na kashfa kwa wanachama wa jamvi hili. Kuna watu makini na wengi wamekuwa wanampa Zitto nafasi ili aeleze kilichomtokea kwenye kamati hizo au kwenye issue ya Dowans.

Huwezi kulazimisha watu kukubaliana nawe. Ukiwa na mpango wa kuwa mwanasiasa, inabidi ujenge ngozi yako ili iwe ngumu kiasi cha kuhimili hoja za watu (wakiwemo wana JF).
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…