Mkuu kuhusu Zitto kuingia kamati ya madini kuna kasoro moja kubwa sana. Zitto anawakilisha sera za Chadema ambazo zinahitaji nchi yetu kuwa na hisa katika amshirika ya madini. Sasa ikiwa serikali yetu haina hisa ndani ya mashirika hayo, hakuna sera wala kifungu cha mtazamo wa chama chake (Chadema) umekubalika na serikali kuu kutumiwa ili kuboresha sekta ya madini. Zitto hakutakiwa kufanya kazi huko kwa sababu ni Kinyume cha katiba ya chama chake.
Kaka nakushauri upitie ripoti yao na uone kama hilo halikushauriwa ama la. Na jee una taarifa yoyote ya mabadiliko yanayoendelea katika STAMICO? Na si kweli kuwa serikali haina hisa atika makampuni yote ya madini. Huo ndio ilikuwa mwelekeo hapo mwanzo kabala ya kamati ya Bomani lakini sasa wameanza kurudi katika masuala ya umiliki wa hisa na hata NDC inajirekebisha ili kuendeleza mfumo uo kama ilivyo katika mradi wa Mchuchuma.....
Siku zote wabunge wanashirikiana na serikali kuu ikiwa tu serikali kuu itakubali kubadilisha baadhi na sera zake na kufuata mkondo wa kati kaisi kwamba hata Wapinzani wanakuwa na mchango wa sera zao.. Lakini sii mtu kuingia kamati ambayo malengo yake ni kinyume kabisa chga mtazamo wa chama chako..
Una maana maelngo ya kisiasa ama malengo yaliyokuwemo katika TORS za utendaji wa kamati hizo? Jaribu kupitia TORs za kamati ya bomani halafu ndio ufikie conclusion kama ilikuwa makosa kuingia huko? Hivi sio CHADEMA hao hao waliokuwa wakidai kuwa Tundu Lissu ndio aingie katika kamati hiyo. mmesahau maneno ya Slaa na Chacha Wangwe? Ama huo ulkuwa msimamo wao binafsi na sio wa chama chao?
Anyway haya yalikwisha pita.. Zitto alichemsha, akachemsha na anaendelea kuchemsha kutokana na tatizo kubwa na siasa nchini. Yaani vyama vyote vya siasa havina mrengo, Zitto ni Conservative na anahusudu mrengo huo wakati Bongo kila mtu ana dini yake lakini unaambiwa nchi haina dini..hivyo hivyo principal hiyo ipo ktk Mrengo..
Si kweli mkandara. Inawezekana vyama hivi vinashindwa kutengeneza na kuzisimamia sera zinazoendana na mirengo yao lakini wanayo. CUF wao ni waliberali ingawa ni mabingwa wa siasa za chuki na kukosa uvumilivu. Chadema walikuwa mabwanyeye na sasa wamepunguza makali na kuwa mabepari ingawa ukiangalia sera na misimamo na kauli mbiu zao zimejaa fikira za kijamaa. CCM wao ni wajamaa ingawa sera zao ni za kibepari.
Zitto hajawahi kuwa conservative. nimemjua Zitto kama mjamaa ingawa kuwepo kwake CHADEMA kumemfanya aanze ku-accomodate sera za kibepari. Na ni wao ndio waliokuwa wakipush CHADEMA kuelekea kushoto lakini mwisho wa siku 'busara za wazee" zikawalazimu wakubali kushindwa kwa kusogea kutoka kwenye ubwanyenye hadi ubepari. No wonder unawaona kina Kitila, Baregu na hata Mnyika wapo humo ilhali hawana asili ya ubepari wala ubwanyenye. Inawzekana wanaamini ku-camouflage kwa sasa hadi hapo baadae "wakati takaporuhusu"
Na tunapokuja katika mantiki ya Conservatism, mtizamo wangu ni kuwa ubepari wala ubwanyenye hauwezi kuwa conservatism kwa mantiki ya historia na fundamentals za Utanzania....Kwetu hapa ma-conservatives ni wale wanaokataa kukubali kushindwa na kufakamia ubepari. Consevatism kwa Tanzania imejikita katika misingi ya ujamaa na kujitegema kwani hiyo ndiyo iliyounda nchi na jamii ya Tanzania...
omarilyas