Je Zitto Amepoteza Uhalali wa kuwa Kiongozi?

Je Zitto Amepoteza Uhalali wa kuwa Kiongozi?

Shida Salum, maarufu kama First Lady ameshukia Dr Slaa na kumtuhumu kwamba amemuita mwanae kuwa ni fisadi. Shida Salum ambaye ni mama mzazi wa Zitto Kabwe aliyesama hayo katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA(BAWACHA).

Akifungua mkutano huo, Dr Slaa alisema kwamba wanawake wa CHADEMA wawe mstari wa mbele katika kupiga vita ufisadi na kuhakikisha kwamba mafisadi hawasambaratishi CHADEMA.

Dr Slaa akatoa mfano wa jinsi ambavyo mafisadi walitaka kuichafua CHADEMA wakati wa kifo cha Wangwe na kufikia hatua ya kupika habari kwamba Mbowe alifukuzwa na mapanga Tarime.

Dr Slaa alisema kuwa huo ni mkakati wao kwa kuwa hata wakati wa hoja ya BOT walifikia hatua hata ya kuutumia usalama wa taifa kutimiza azma hiyo kwa kunukuu barua yao ya kuzuia hoja hiyo.

Dr Slaa alisema kuwa CHADEMA ndio mbadala wa CCM hivyo inatazamwa kwa matumaini na watanzania wote na kuwataka wanawake wawe mstari wa mbele kulea chama.

Mara baada ya Hotuba hiyo, Mama Shida ambaye alikuwa ni mgeni waalikwa kwenye ufunguzi wa mkutano huo kama Mwenyekiti wa Chama cha Wenye Ulemavu(CHAWATA) alinyoosha kidole kusema neno.

Moja kwa moja akamlaumu Dr Slaa kwa kumuita mwanae kuwa ni fisadi. Akamtaka afahamu kuwa makao makuu ya chama hicho yamejaa uchafu.

Hata hivyo, Dr Slaa ambaye katika hotuba yake hiyo hakusema popote kuwa Zitto ni fisadi alimshukuru Mama Zitto kwa swali lake, na kumweleza kuwa kama ofisi ya katibu Mkuu inauchafu basi ni jukumu la yeye na Naibu Wake ambae ni mwanae Zitto Kabwe kuundoa ama kuwajibika.


..........ndiyohiyo

Please either change the title or delete your thread, hili siyo gazeti na hutangazi biashara ili watu wasome ulichoandika.
 
He he mpambano naona ngoma inogile, ngoja nivute whisky taratibu niweze kuyasoma kwa uzuri haya maelezo ya wenye 'weledi' na 'uchungu na nji hii'..
 
Eric;

Well said on Zitto. We are now waiting for the otherside of the coin.

Mbowe naye hajafanya lolote kama Zitto "alivyofanya" hayo uliyotaja?

Jamani leteni basi BALANCED STORIES. Hicho tu ndio sisi wakongwe tunataka humu jamvini.

Au weka toka mwanzo kuwa "mimi nipo pamoja na Mbowe" thing kisha endelea/anza kumshambulia Zitto.

FP
 
Zitto Kabwe, hana msimamo ni mwanasiasa hatari sana huwezi mwunga kwa matamshi yake, huwa hatafakari wala hapimi nini anasema au kufanya. Kwa hulka yake hiyo ndio maana anajikanyaga kila kukicha, viongozi kama yeye ndio mzigo wa taifa letu, huwezi kujua ni nani wa kumwamini wala nini wanakimaanisha, huyumbishwa na kaupepo kadogo sana.

Mfano Zitto amewahi kusema hatagombea tena ubunge ila sasa naona ameanza kampeni sijui kesha waambia wapiga kura wake amebadili mawazo au la.

Zitto alisema anakwenda kusoma tumemwona anataka uenyeketi.
Zitto alikurupuka kuchukua form katishwa kidogo kaachia, kweli anaweza kuvumilia vishawishi vya CCM kama fungu la Dowans, hongo ya kamati ya nk.

Zitto kila akitoka kwenye mikutano ya ndani na viongozi wenzake anakuja nje na kukutana na waandishi na kujifanya yeye hajakubaliana na maamuzi yao, mfano saga aliposema kwamba alitakiwa kuhongwa cheo.

Pili Zitto anashangaza pale anapotoa kauli mama yake aachwe wakati anajua wazi mama yake ni mwana siasa na hakuna atakaye jali eti ni mama yake Zitto akiongea pumba atapewa, mfano pumba aliyoitoa juzi akimwambia Slaa eti kamwita mwanae Fisadi.

Ukijaribu kuangalia uwezo wa Zitto kupanga, kuamua na busara hafai kuwa hata diwani sema bongo iliyoishiwa wananchi hawaruhusiwi kujadili mambo magumu na kujua viongozi wao.

hakuna kosa kama kuwa na kiongozi asiye na msimamo au kujua nini dhamira yake. Ndio maana tumezalisha mtu kama Kikwete ambaye hakuna anayejua yupo na mafisadi au wasafi yeye wote anapuliza na nchi inaliwa kama mchwa.

Zitto ndugu yangu jaribu kufikiri kabla ya kutoa kauli, kauli zako nyingi zinakatisha tamaa sana, zinafanya kila mmoja akuweke fungu analoona linafaa, unajiua kisiasa kwa watu makini, hekima na busara ni vitu muhimu sana katika maisha kuliko degree saba, ukivikosa hivi utateseka sana.

Mwisho kitendo cha kuchomoa form ya kugombea kwa sababu ya wazee msimamo nimeona ziro si kwamba nilipenda uwe mwenyeketi la hasha usingeweza kuongoza chama, ila sipendi watu wasio na msimamo hata kidogo, ni rahisi kununuliwa na kwenda na tamaa zao. Ulitakiwa upime mapema na ulijue hilo kwamba huwezi kwenda mpaka juu, au unaweza na hakuna wa kukutisha. Je kweli utaweza kupambana na dunia hii ya leo ya dot.com?????!!!!!!!!
 
"......................Mimi Chadema ni basi langu ambalo nasafiria au sawa na mtumbwi wangu baharini, sasa nitawezaje kuivuruga, halafu nitapata faida gani au nitakwenda wapi,".
 
"......................Mimi Chadema ni basi langu ambalo nasafiria au sawa na mtumbwi wangu baharini, sasa nitawezaje kuivuruga, halafu nitapata faida gani au nitakwenda wapi,".

Sasa na nyie mmezidi.... threads kumi Zitto, unganisheni basi........ KERO SASA!!!! MMEKUWA KAMA CHAMA CHA MIPASHO WAKATI KUNA WATU WENYE BUSARA NA UTASHI MKUBWA SANA HUMO NDANI

ACHENI KUJIAIBISHA SASA

Mods, hebu saidia basi kuungaunga
 
We can not under estimate nguvu ya mafisadi. Naamini maneno ya Mzee Mtei kuwa mafisadi wamepenyeza rupia Chadema. Kuna uwezekano kuwa haya tunayoyaona ni matokeo ya operesheni hiyo. Kama Chadema wakionesha maturity kwenye ku-deal na hili litakuwa jambo la maana na itaweka mazingira mazuri ya chama kujijenga. Lakini kama kesho wakifanya fyongo watawapa CCM a big greenlight.

.

Ukiamini maneno ya mtei yasiyo na vithibitisho basi hakuna MPAMBANAJI ALIYE SALAMA!
 
Mpendwa Zitto,

Salam sana. Ama baada ya salamu naomba nichukue nafasi hii kukupa pole na majukumu uliyonayo pamoja na misukosuko yake.

Ukiacha suala la Dowans, kujitoa kwenye kugombea nafasi ya uenyeketi CHADEMA - Taifa, kumeonyesha kukosa kwako principles. Huku kunapelekea wewe kuyumba na kupoteza sifa za uongozi bora.

Kuhamia CCM kutakuwa jambo la mbolea kwani huko hakuna watu wenye principles na pia unaweza ukawa juu ama ukapotezwa kabisa katika ramani ya siasa za Tanzania.

Vipi kuhusu kuachana na siasa na kujikita katika academia? Nadhani kungekufaa zaidi. Sijui ni jinamizi gani aliyekushauri ukaachana na wazo hili.

Walijua lazima utachemsha soon or later baada ya kukuona ni mtu usiye na principles na kama unazo basi huishi kwazo.

Pole sana, ndio ya kidunia. Maisha ni mapambano lakini angalia sana kwani kikulacho ki nguoni mwako.

Wakatabahu

Mapinduzi.
 
Last edited:
Mpendwa Zitto,

Kuhamia CCM kutakuwa jambo la mbolea kwani huko hakuna watu wenye principles na pia unaweza ukawa juu ama ukapotezwa kabisa katika ramani ya siasa za Tanzania.

Hapa nakubaliana na wewe kuwa SISIEMU hakuna watu wenye principles, lakini sishauri Zitto aende huko. Mwache abaki kwenye upinzani kwani kuteleza sio kuanguka.

Vipi kuhusu kuachana na siasa na kujikita katika academia? Nadhani kungekufaa zaidi. Sijui ni jinamizi gani aliyeushauri ukaachana na wazo hili.

Hili mbona litakuwa gumu sana kwa Zitto...!!!
 
Ukiacha suala la Dowans, kujitoa kwenye kugombea nafasi ya uenyeketi CHADEMA - Taifa, kumeonyesha kukosa kwako principles. Huku kunapelekea wewe kuyumba na kupoteza sifa za uongozi bora.

kati ya controversial ambazo hana budi kurethink the direction in political race ni hizo; 1.dowans2.vying for chairmanship.
1.Dowans; ulitaka tununue tu mitambo wakati wanaharakati wote wakikataa, na kufikia kuongea lugha zisizo na nidhamu kwa mh. Mwakyembe-people discredit for that!

2.Chairmanship;nakuunga mkono kujitoa kwa sababu ulikuwa umejichimbia kaburi la kisiasa, too eary kwa sisi kukuamini kama unaweza kuongoza chama cha vijana na wazee. nimestudy the way unawatreaty wazee, nikaona, bado, huwezi. the way ulivyodili na mwakyembe, sitta na slaa hivi majuzi, bado

wayfoward; stop politicing youth wing, sababu your very senior to them in national issues, ikiwezekana achana na vyeo ndani ya chama, show that u r loyal even out of system. stop connection with untrusted networks.
otherwise mwakani utakuwa mwisho wa siasa zako, wakati siasa zitapokuwa tamu zaidi-when smart, neat and intellectual politics will prevail.
 
kiukweli zito namwita jina halisi la kibantu sio zitto la baada ya kupata vijisenti bado hajapevuka kisiasa wengi tulikuwa tunamuaminia lakini amepruv felia, karubunika kirahisi yaani inatia huruma kuona kijana wa umri wake akihamanika kwa kuwa karibu na kiongozi au mtu maarufu akaacha msimamo aliokuwa nao wa kutetea maslahi ya nchi. nilishangaa kusoma makala moja anajieleza anamiliki magari matano hivyo anunuliki ni mtu aliyeelimika au alihudhuria madarasa
 
Omary, unapotumia wingi unaniwekwa mimi katika kundi gani? Kama una aamini mimi nimeandika kwa msukumo wa makundi au kutumia na kama huo ndio msingi wako wa kuamini kuwa kuna makundi basi ya makundi hayapo na ni hewa.

Binafsi siamini kama kuna makundi.Hata hivyo wewe unalazimisha kuwepo makundi na kujipachika katika kundi la kubuni la zito. Mtazamo wako huu umekupofusha na usione mantiki ya hoja zangu. Nimekuonyesha mwezi wewe umetazama kidole.

Msingi wa hoja zangu ni maandiko yalikosa mwelekeo ya Zito.Nimempima zito na Zito mwenyewe. Matendo yake, misimamo yake, muonekano wake katika jamii na matarajio ya jamii kwake ndio msingi wa maandiko yangu. Amepwaya dhidi ya mizani aliyoibuni mwenyewe.


Nimesema mwanzo kuwa sitetei ukiritimba na naamini ushindani ni chachu muhimu kwa ustawi wa chama. Hoja zangu zimejikitka katika uwezo wa kitaasi kwa sasa kubeba ushindani huu? Pia ni nimehoji msukumo halisi wa Zito kugombea(wewe unakaribia kusema aligombea kwa kuwa hakuwa na uhakika wa kuteuliwa kuwa katibu mkuu!) na mwisho nimemlaumu Zito wa kutofanya maandalizi ya kutosha kama mgombea, kushindwa kwake kusoma mazingira ya chama anachokiongoza alikuwa tayari majiandalia mazingira ya kushindwa kwa maksudi! Na hapo ndipo ninapoibua shaka ya lengo lake...........



Suala la Zito kuzungumzia kusimamishwa/kufukuzwa kwa viongozi na wanachama ni hoja inayomkaba Zito pia. Nakumbuka Zito ni moja ya watu waliotetea umuzi ule Tanga na alitoa mifano ya CCM kuwahi kufanya maamuzi kama hayo huku nyuma kwa kina ml0o, seif, jumbe n.k.

Jitihada za kumuibua Zito kama shujaa kwa uzembe wake aliofanya hazitasaidia. Nimekusoma unajaribu kujengwa taswira kuwa Zito amefanya vyema kusema aliyoyasema kwa minajili ya kusafisha chama? Eti anatetea Ukweli ? Huu ndio uwezo wako kweli Omar?

Suala hapa ni je Zito anafaulu kuwa muumini na mtetezi wa ukweli kwa maelezo aliotoa? Kama yeye ni muumini wa ukweli kwanini awe anasema "ukweli" akiwa amekasirika tu? Ni pale tu inapothibitishwa kuwa ana nyama ndio ukweli unatoka? Ukweli ungetoka kwa msimamo wake halisi(as a matter of principal) ningemuunga mkono. Zito hajafanya hivyo, kaandika kwa muskumo wa hasira, mazingira aliyotumia hayampi uwanja sawaia wa kufanya ukweli wake ukaaminika, hizi ni hujuma kwa ukweli(kama upo) anaojaribu kuutetea, uwezo wake wa kuvumilia uovu na kuutoa pale tu anapokasirishwa ni kielezo cha udhaifu wake.

Isitoshe hajaeleza ukweli wowote zaidi ya umbea. Kama angekuwa na nia ya kutoa ukweli angefafanua suala la "kumtenda wangwe" na masuala ya ubadhirifu kinagaubaga,yeye kugusia na kuwaaacha watu wafikiri watakavyo sio sifa ya mwkeli, lengo lake ni kupandikiza hisia mbaya dhidi ya chama na sio kukisafisha. Kama amaamua kusafisha asafishe kwa ustadi tuliouona kwenye uwasilishaji wa hoja ya Buzwagi na sio kutoa madokezo ya kimbea yenye mguso wa kishangingi. Uamuzi wake wa kueleza maneneno nusu na kutafuna maneno hapa hatuwezi kusema ana nia ya kusafisha chama. Hapa ametweta.


Suala la Zito kumfahamu Mbowe na Mnyika mda mrefu sio hoja,na sijui inaingia vipi hapa, wandelee kufahamiana maana mahuisiano ni hitaji la kiutu.Sikuandika kwa minajili ya kuhoji mahusiano yao nimehoji weledi na uwezo wa Zito kioungozi.

Hilo swala la Zito kuchoma kisu linatokea wapi? Kwanini unakuwa mwepesi kupandikiza hoja zisizo na maana yoyote ile? sikuona mazingira ya hatari kwenye uchaguzi wa BAVICHA. Sehemu kubwa ya hoja zako ni za kufikirika na kuweweseka nakosa pa kuanzia kuzijibu. Invayolekea mvutano ulipo sasa umechangiwa na umbea na majungu. Umbea wako kama huu wa Zito kutaka kuchomwa kisu unanipa picha ya mchango wako katika kumpotosha Zito na kumjaza majungu. Inalekea kiu yako ya kuwa na msisimko wa kisiasa wakati wote inakulazimisha kubuni mambo ambayo hayapo wakati wote na kisha kuyaamini kama ni ya kweli. Ni aibu kwa mtu wa taaluma yako kujidhalilisha katika kiwango hiki. Pengine ushauri wako ndio mwiba kwa mustakabali kisiasa wa zito. Hakika kikulacho……….

Mkuu Eric nimevutiwa na uwezo wako wa kusasambua hoja!
 
Zitto kafulia hakuna hata haja ya kumjadili hapa jamvini.
 
Mpendwa Zitto,

Salam sana. Ama baada ya salamu naomba nichukue nafasi hii kukupa pole na majukumu uliyonayo pamoja na misukosuko yake.

Ukiacha suala la Dowans, kujitoa kwenye kugombea nafasi ya uenyeketi CHADEMA - Taifa, kumeonyesha kukosa kwako principles. Huku kunapelekea wewe kuyumba na kupoteza sifa za uongozi bora.

Kuhamia CCM kutakuwa jambo la mbolea kwani huko hakuna watu wenye principles na pia unaweza ukawa juu ama ukapotezwa kabisa katika ramani ya siasa za Tanzania.

Vipi kuhusu kuachana na siasa na kujikita katika academia? Nadhani kungekufaa zaidi. Sijui ni jinamizi gani aliyekushauri ukaachana na wazo hili.

Walijua lazima utachemsha soon or later baada ya kukuona ni mtu usiye na principles na kama unazo basi huishi kwazo.

Pole sana, ndio ya kidunia. Maisha ni mapambano lakini angalia sana kwani kikulacho ki nguoni mwako.

Wakatabahu

Mapinduzi.

Hivi swala la Dowans Zito alitoa sababu gani? kwa nini alitaka inunuliwe? maana hii ishu ipo tu kama magazeti ya udaku, ukiwza kujibu mswali hayo utajijua unafuata mkumbo au la! au unafuata mawazo ya Mwakyembe?

Kufa kisiasa hayo mawazo yako, wengi wanampenda Zito,

Halafu je wote mkiwa wapinzani hamuwezi kutofautiana kimawazo? ili nalo linahitaji uzee kidogo? kila kitu mkumbo akitokea mwenye mawazo ya tofauti , msaliti and we alwayscry TUWAZE



Ukiacha suala la Dowans, kujitoa kwenye kugombea nafasi ya uenyeketi CHADEMA - Taifa, kumeonyesha kukosa kwako principles. Huku kunapelekea wewe kuyumba na kupoteza sifa za uongozi bora.

kati ya controversial ambazo hana budi kurethink the direction in political race ni hizo; 1.dowans2.vying for chairmanship.
1.Dowans; ulitaka tununue tu mitambo wakati wanaharakati wote wakikataa, na kufikia kuongea lugha zisizo na nidhamu kwa mh. Mwakyembe-people discredit for that!

2.Chairmanship;nakuunga mkono kujitoa kwa sababu ulikuwa umejichimbia kaburi la kisiasa, too eary kwa sisi kukuamini kama unaweza kuongoza chama cha vijana na wazee. nimestudy the way unawatreaty wazee, nikaona, bado, huwezi. the way ulivyodili na mwakyembe, sitta na slaa hivi majuzi, bado

wayfoward; stop politicing youth wing, sababu your very senior to them in national issues, ikiwezekana achana na vyeo ndani ya chama, show that u r loyal even out of system. stop connection with untrusted networks.
otherwise mwakani utakuwa mwisho wa siasa zako, wakati siasa zitapokuwa tamu zaidi-when smart, neat and intellectual politics will prevail.

Akiondoka nafasi yake utachukua wewe? au mwingine atakayekuja uttaka asiwaze wala kusema mawazo yake kwa sababu atakuwa kinyume na wanaharakati?

Au kwako wewe ni nani mpiganaji asiyetofautiana na wenzake hata kidogo(robot??)

Hilo kaburi la kisiasa ni lipi ebu eleza how? ni jinsi gani angejichimbia?

jamani siyo kijiwe hiki! message wanaoandika wengi hawaandiki HAYA YOTE MWISHO WAKE NI NINI?
Hivi unafikiri Zito ana la kupoteza?

Graduates wengine mko wapi basi, au ndio kuishia kukopa magari, kupanga sinza na kusimamia harusi!!!!

Naomba mnisaidie ni mpambanaji gani mtakaye believe in him/her? maana hili linarudisha nyuma wengi sana

SIJAONA MKISEMA LOLOTE JUU YA CHADEMA KUIBAKA DEMOKRASIA, are you thinking in one direction only?, even blind changes directions.

CHADEMA kw ujumla wanafaa kuongoza nchi? lengo letu ni CCM waondoke , je hayatotokea ya Kenya? wapinzani wanachukua kesho wanamwaga damu kisa hawataki kutoka madarakani??

We need to think twice though, hizi post hazijengi lolote maana hazimuharibii zito zinaharibu na kurudisha nyuma wapiganaji wooote, kila mtu anaandik taarabu.

Kesho utamsems Slaa,
then ....

the.....
 
Eric baba, hayo mawazo yako wala usifikiri kila mtu anawaza kama wewe!

Kwangu mimi Zito mpiganaji na kiongozi mzuri, andika weeeeeeeee jaza hata thread zote kwangu mimi ni hivyo hiyo haitabadilika; sijamjua leo wala jana!

Pili, weka dhamana au insuarance kuwa wengine woote wapiganaji hawawezi kuhudhiwa na kubadilika; ama sivyo kutakuwa hakuna mpiganaji !

swala la kuwa huyu jamaa atakufa kisiasa pia ni theory is not practical, na wote wanaosema hivyo ni kujaribu kutabiri kama akina Yahaya!

Tukiwa wakali kuwalinda wale wapiganaji wetu tutawaokoa wengi, tukiwa waandika nakala kama wewe tutaua wengi mwishowe utabaki wewe peke yako maana wooote watachukuliwa na upepo.

Uwazi wa Zito ni mzuri ndugu , ni picha tunapata kuwa ni jinsi gani vyama vinavyojiita mbadala vinaishi, Zito angekuwa wa kujikomba angekaa kimya!

KWA NAKALA YAKO UNAPROVE PIA KUWA ZITO YUKO JUU SANA ZAIDI YA CHADEMA, CCM huwa hawafanyi ujinga huu, angekuwa mdogo; why all this unconvicing articles!

Mwambie Mtei na Chadema wote kuwa habari zenu tumezipata na mnavyoishi humo, hamna tofauti na CUF, NCCR, TLP.

Shida ilikuwa nini si angeachwa ashindwe kwenye kibox cha kura, wewe hili hufikirii??

swali la kumalizia, tunawalindaje hawa wapiganaji?? maana juzi tu ulikuwa unampenda Zito , leo humtaki, kesho utamkacha Slaa, maana tuhuma zipo tu, na tusivyopenda vithibitisho!

why are we not believing in them, when then we will belive them as true dream leaders??

Mtu gani mkweli atakayeingia kwenye siasa na kuishi namna hii??

...................................

mchaga nini wewe!!!!!!!!!!

mengine yote yawezekana kuwa una hoja,...................ila hiyo ya mwisho hapo....mkuu umepotea.......
 
shida salum, maarufu kama first lady ameshukia dr slaa na kumtuhumu kwamba amemuita mwanae kuwa ni fisadi. Shida salum ambaye ni mama mzazi wa zitto kabwe aliyesama hayo katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa baraza la wanawake wa chadema(bawacha).

Akifungua mkutano huo, dr slaa alisema kwamba wanawake wa chadema wawe mstari wa mbele katika kupiga vita ufisadi na kuhakikisha kwamba mafisadi hawasambaratishi chadema.

Dr slaa akatoa mfano wa jinsi ambavyo mafisadi walitaka kuichafua chadema wakati wa kifo cha wangwe na kufikia hatua ya kupika habari kwamba mbowe alifukuzwa na mapanga tarime.

Dr slaa alisema kuwa huo ni mkakati wao kwa kuwa hata wakati wa hoja ya bot walifikia hatua hata ya kuutumia usalama wa taifa kutimiza azma hiyo kwa kunukuu barua yao ya kuzuia hoja hiyo.

Dr slaa alisema kuwa chadema ndio mbadala wa ccm hivyo inatazamwa kwa matumaini na watanzania wote na kuwataka wanawake wawe mstari wa mbele kulea chama.

Mara baada ya hotuba hiyo, mama shida ambaye alikuwa ni mgeni waalikwa kwenye ufunguzi wa mkutano huo kama mwenyekiti wa chama cha wenye ulemavu(chawata) alinyoosha kidole kusema neno.

Moja kwa moja akamlaumu dr slaa kwa kumuita mwanae kuwa ni fisadi. Akamtaka afahamu kuwa makao makuu ya chama hicho yamejaa uchafu.

Hata hivyo, dr slaa ambaye katika hotuba yake hiyo hakusema popote kuwa zitto ni fisadi alimshukuru mama zitto kwa swali lake, na kumweleza kuwa kama ofisi ya katibu mkuu inauchafu basi ni jukumu la yeye na naibu wake ambae ni mwanae zitto kabwe kuundoa ama kuwajibika.


..........ndiyohiyo

mbona kiporo ?
 
Back
Top Bottom