Zitto alitangaza kugombea na kisha akachomoa (sioni connection yoyote ya kukemea maovu ya Chadema).
What if kugombea nafasi ya uenyekiti ilikuwa hatua ya kwanza ambayo akalazimika kurudi nyuma kutokana na "busara za wazee" na kulazimika kuchukua hatua ya pili kwa style tofauti ili kushughulikia kitu hicho hicho
Kabla ya hapo, Zitto alifanya yafuatayo-
1. Alijiunga na kamati ya madeni ya Kikwete (akipingana na wenzake)
2. Aliungana na mafisadi kwenye issue ya Dowans
3. Hakujulikana msimamo wake kwenye bajeti ya serikali iliyopita.
Kupingana na wenzake kunahusiana gani na kukosa msimamo. Ama una maananisha kuwa kutokubali kuburuzwa kimtizamo ndio kukosa msimamo?
Kuhus dowans, tatizo lilikuwa the so called kuungana na mafisadi ama kupingana na MASIHA feki wenu ambao kutokana na ugoigoi wa kuuliza mswali maswali magumu mmeamua kuwakumbatia huku wakipiga bao la kisigino katika nia yao ya kulinda uhalali wa mfumo fisadi....
Hayo mengine ya uchaga na chadema nadhani unarudi kule kule kwenye ukabila na chuki zisizofaa ndani ya nchi na hivyo kukufanya wewe kuwa mtu mwenye chuki mbaya sana za kikabila na unayefaa kuogopwa kama ukoma.
Kujenga alliances zinazothamini ukabila na udini kunafaa, kuhoji na kukosoa matendo kama hayo ndio hakufai? Ukabila, Udini, ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa kijinsia, ufisadi yote haya ni matatizo yaliyopo katika jamii yetu na sasa yanaota mizizi....ni lazima yaongelewe kwa uwazi ili kuyashughulikia ipaswavyo....
Kama CUF wanavyokosolewa kwa udini, CCM kwa ufisadi na Chadema kwa ukabila....mnachopaswa ni kuyashughulikia kwa kuepuka kufanya mambo ama maamuzi yanayotoa taswira hasi hizo na sio kuwajengea uadui wale wanaohoji ama kukosoa.....
omarilyas