Jean-Paul Mobutu: Mtoto wa Kwanza wa Mobutu Sese Seko aliyetazamiwa kuwa Rais wa tatu wa DR Congo

Nimekusoma toka page 1 mpaka mwisho nimepata kitu kichwani kuhusu Zaire, vp we hujawahi fika huko au unaishi huko?
Mkuu mimi siishi zaire
Na sijawahi kifika.ila nina mpango wa kwenda siku moja na kuinunua nyumba ya mobutu niikarabati nikipata pesa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh! Mkuu huyu Mzee ambaye alimkabidhi Lumumba kwa kina Tshombe akauwawa huko Katanga kwa usimamizi wa mabeberu huyu huyu aliyechangia kudhoofisha harakati za ukombozi huku kusini mwa Africa akisaidiana na makaburu huyu huyu anayetajwa kuwa fisadi mkubwa kuwahi kutokea Africa leo unasema aliipenda Congo kweli!
 
Mkuu, wakati lumumba anauliwa Mobutu alikua kinshasa. Alimueka house arrest lumumba pale kinshasa ila lumumba akatoroka mwenyewe matokeo yake akakamatwa huko

Unajua lumumba pia alikua anatumiwa na mabeberu ? Ilikua hivi. Lumumba alitumiwa na wasoshalisti ussr walitaka kupandikiza ideas zao pale congo kitu ambacho aliyekua rais wakati huo mzee kassavubu alikikataa akamfukuza kazi lumumba lumumba akakataa kuacha ofice akawa na kakikundi kake ka waasi .rais akamuagiza mobutu ambaye alikua chief of staff amkamate lumumba. Mobutu akaamua awapige chini wote awe rais yeye kwa kusaidiwa na US

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasikia Bongo Movie inabamba sana Zaire kama si tunavyo ikubali Ndomboroo

Sio bongo movie tu hadi bongo fleva inapendwa wasanii wa maigizo kama late kanumba, ray na majuto wanamashabiki huko, Ali kiba na diamond na aslay kule wanavuma hapo wasanii kama martha mwaipaja na shusho na bahati bukuku wanamajina sana congo
 
Kuna fursa sana ya sanaa ya tanzania nchini DRC sema hua hawaendi sijui kwa nini?
 
Baadhi ya watanzania waliotumia fursa wamewekeza kwenye usafirishaji mfano watu wa taqwa ruti za lubumbashi dar au wale classic wanapiga kisangani kwenda butembo,
 
Yule aliyezungumzia fursa congo sio za kuuliza, ukiweza kafungue mgahawa lakini ukubali kuuza pia nyama ya makako (ngedere) na wanapenda bugali ya muhogo
 
Yes fursa nyingine ni ukauze bazee sijui mnaita batik.
 
Dagaa kutoka Tanga na zanzibar ndio ilikua inalika sana lubumbashi nadhani mnaita dagaa nyama zinachemshwa kwenye chumvi kama sijasahau, hii ni kwa wale mnaochungulia fursa japo watanzania wengi hasa vijana ni waoga
 
Wacongoman hupenda pia kiingereza hii fursa wapo baadhi ya wakenya na waganda wanamadarasa ya kiingereza kwenye miji kadhaa kama Kinshasa, goma, kisangani, lubumbashi na kadhalika
 
Mkuu huwezi kumtenga Mobutu na mauaji ya Lumumba alimuweka kizuizini na kumkabidhi kwa wahuni wa Katanga na kuhusu Ussr ni kwamba Lumumba aliamua kuomba msaada huko baada ya UN kwa ushawishi wa US kukataa kushirikiana nae kumaliza uasi wa Katanga kifupi huyu Mobutu ni msaliti mkubwa wa Congo ndio maana Karma ilimtafuna akafia ukimbizini
 
Sasa huoni huyo padri kamwandalia njia kuwa Rais kwa kwenda jeshini. Pengine angeachwa aendelee na masomo bila kwenda jeshini asingeipindua serikali ya Kasavubu na Wala tusingemfahamu. Sijui kwanini aliwachukia waliomwandalia njia.
 
Sio bongo movie tu hadi bongo fleva inapendwa wasanii wa maigizo kama late kanumba, ray na majuto wanamashabiki huko, Ali kiba na diamond na aslay kule wanavuma hapo wasanii kama martha mwaipaja na shusho na bahati bukuku wanamajina sana congo
Wangekuwa wanaenda kupiga shoo
 
Wacongoman hupenda pia kiingereza hii fursa wapo baadhi ya wakenya na waganda wanamadarasa ya kiingereza kwenye miji kadhaa kama Kinshasa, goma, kisangani, lubumbashi na kadhalika
Napenda kiswahili cha kicongo kwa nn Congo wanaongea sana kiswahili kuliko Wazambia?
 
 
mabutu ni mtu wa equateur ni north pamoja na jean pierre bemba but wakasai wanatoka pronvince ya kasai- oriental(mashariki) na kasa -lomani na kasai central ziko south wana boda na angola ndiko kwa kina shalamwana and "mutwashi" is their dance kama unajua bolingo
 
Yeah najua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…