luambo makiadi
JF-Expert Member
- Nov 28, 2017
- 10,602
- 8,798
Nijaujua wote kwa tafsiri ,luambo alimsujudu Sana mobutuKama unajua kikongo ama kilingala na unapenda miziki ya Kongo, basi ukipata wimbo wa FRANCO LUAMBO MAKIADI unaitwa
''Candidat na Biso Mobutu'' part 1 , 2 na 3
Maana yake ''Our Candidate is Mobutu''
Utacheka na kujifunza sana.
Ngoja nikupe vionjo kidogo vya mashairi
Wazaire wote tokeni barabarani,tumshangilie mgombea wetu Mobutu
Bazana na bazolo(mjini na vijijin) mgombea wetu ni Mobutu
Kamati kuu ilifanya kazi nzuri kumpitisha Mobutu kama mgombea wetu,wachawi na wanafiki wote wameumbuka
Janvier à mars (mwezi January hadi machi) tutafanya maandalizi ya kampeni, de Mars à mai (mwezi wa tatu hadi wa tano) kufikia mwezi novemba tutakuwa tumeshamaliza propaganda zote na mgombea wetu atashinda
Ba gouverneur nyoso (wafanyakazi wote wa serikali mgombea wetu ni Mobutu
L'armée nationale (majeshi ya Taifa mgombea wetu Ni Mobutu)
Hivi ninavyoimba,wachawi na wanafiki wanasema kumbe luambo ni wa Mobutu? Na mimi nawauliza mlidhani mimi ni wa Nani?
Mobutu ameleta Amani Zaire,tembea nchi nzima mioyo ya watu imejaa Amani,zamani ilikuwa hivyo?
Watu wote mlio katika vyombo vya usafiri mgombea wetu ni Mobutu,hata kama unasafiri kwa Meli,mashua mgombea wetu ni Mobutu,wagonjwa mlio mahospitalin mgombea wetu ni Mobutu