Mbeya, Tanzania
Wakili Mwabukusi - Ni sawa na nchi kuvamiwa na kukaliwa
Haki za watanganyika, historia, mali zilindwe na vivyo hivyo kwa Zanzibar
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haliwezi kugawa ardhi ya Tanganyika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mlinzi tu wa ardhi na siyo mmiliki wa ardhi ya Tanganyika
Bunge haliwezi kutoa masaa 24 waTanganyika kujadili pande la ardhi ya Tanganyika na hata lile tangazo la Bunge kuita wananchi na wadau watoe maoni ni utani mtupu ... na kukebehi waTanganyika
Endelea kusikiliza kitu hiki sensitive kikichambuliwa kwa kina makosa yake makubwa yasiyokubalika hata haufahi kutambulika kutokana na nia pia kusudio la mkataba huu yaani letter of intent ... ambao nadhani haujapita ktk interministerial technical Committee kutoa ushauri, hivyo document hii haikupita kwa washauri wabobezi waliopo serikalini ...
A letter of intent is a document outlining the understanding between two or more parties which they intend to formalize in a legally binding agreement. The concept is similar to a heads of agreement, term sheet or memorandum of understanding
Waandishi wa habari wamuenzi mwandishi Stan Katabalo ambaye aliona mambo haya miaka 30 iliyopita na kutaandika kwa kina kama habari za kiuchunguzi tofauti na waandishi wa habari wa kizazi cha sasa ambao hata kuhoji wabobezi wa sheria wanashindwa anauliza wakili msomi Boniface Mwabukusi
Wakili anaendelea hili la poor negotiation katika mkataba huu hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa digrii ya sheria chuo kikuu hawezi kukubali kuuridhia na kuusaini ...
Tujiulize ndugu zetu wa Zanzibar hawatamani mamilioni ya dollar ya DP World, kwanini mkataba hauku husisha Zanzibar au kwa vile rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hana nguvu za kuwa mwangalizi wa ardhi / pande la ardhi Zanzibar kutokana na sheria pia katiba ya Zanzibar haimpi mamlaka rais wa Jamhuri ya Muungano kujinyakulia pande la ardhi Zanzibar lakini kwa upande wa Tanganyika rais wa Jamhuri ya Muungano na bunge la Muungano wanahisi wana mamlaka hayo kumega ardhi ya Tanganyika ..
Jambo ambalo wananchi wanatakiwa kufahamu ni kuwa Dubai imepewa kuwa nchi ndani ya Tanganyika huku heshima sovereignty ya Tanganyika imenajisiwa pia sheria inaipendelea Dubai wakati sheria haiwezi kutungwa
Idi Amini alituvamia kwa bunduki, mizinga na vifaru wakati Dubai imetuvamia kwa mkataba lakini katika haya yote inabaki kuwa nchi imevamiwa ..
Ushauri ni kuwa serikali iandae white paper mpya majadiliano mapya kuhusu jambo hili kisha kupelekwa Bungeni na mkataba huu wa DP World ukataliwe, uondolewe na kutupiliwa mbali ili usukwe upya..
Wakili Boniface Mwabukusi anasema bado ana mashaka kama walioshiriki katika mkataba huu pengine walikuwa na uwezo mdogo wa kufikiri na siyo hongo wala nia mbaya hivyo serikali ifanye jambo sahihi kuukataa mkataba huu baada ya wananchi na wadau kuonesha mapungufu yake makubwa ya kutisha na Mali za taifa kukabidhiwa bure kwa Dubai ...