Zogwale
JF-Expert Member
- Jul 10, 2008
- 15,295
- 10,928
I have this Feeling,
Wakati mwingine wakati unahisi mtu akimtetea ROstam au kina Lowassa au Mkuu wa nchi basi huyo yupo kwenye Payroll ya mafisadi.
Kwa ushaihidi ule ule mie nahisi watu hawa watakuwa kwenye payroll ya mengi,haiwezekani watu kumtetea tu mzee huyu wakati huo huo wanpigia chepuo utawala wa kisheria(Mzee kaingilia mahakama)!
Ni utawala gani wa kisheria unaruhusu watu kuzungumia kesi zilizoko mahakamani na kutoa hukumu?
Mie mpaka sasa huwa nasikia Rostam ni Fisadi,ila sijawahi kuona ushahidi wa ufisadi wake!
Aliye nao naomba kwa nia nzuri tu aulete,aje na uthibitisho kama,Rostam alikuja na vithibitisho kwa yale aliyoyafanya mengi.
Ila mpaka sasa mie naona ni tetesi kuwa Rostam ni fisadi ila hakuna vithibi,mpaka nitakapothibitishiwa hayo!
uje na ushihidi wa makaratasi yeye ndiyo mmiliki wa KAGODA,yeye ndiyo miliki wa DOWANS na malipo yaliyowahi kufanywa naye!
watu hawa nimewasoma sana na leo nafikia kusema wako katika payroll,Nahisi ila kuna ukweli,maelezo yao kumtetea mengi ni unbiased
Naomba tuchole Jedwali lingine,mie i have a feeling na siku zote huwa sibahatishi nikihisi,huyu ni mmoja watakaokuwa wanafadhiliwa na Mengi!
1.Mzee Mwanakijiji
2.Kubenea
3.Invisible
Namheshimu sana Mwanakijiji ila naomba aje akanushe tu kwa maneno yake kuwa yeye siyo miongoni mwao!
sitaweza kumhukumu mtu bila ya kuwa na ushahidi ila kama tunavyohisi kina rostam ni mafisadi bais mie nahisi kina Mwanakijiji wanalipwa na Mengi,Period
Kumbe unahisi, nilifikiri ni kweli. Hao uliowataja, na mimi maane na watanzani wazalendo hasa maskini tutakubali kuwa katika payroll ya Mengi ambayo kwa jinsi tulivyo wengi kila mtu angeambulia kasumni tu (50 cents), na tuko tayari kupokea kasumni hako kwa kuwa kanapatikana kwa haki kuliko fadhila ya pesa za mafisadi ambazo hawana uchungu nazo ndiyo maana huzigawa strategically kama njugu!!!! Kama vile Yesu alimwaga damu msalabani kwa ajili ya kuukomboa ulimwengu bila malipo basi nasi tulio nyuma ya Mengi ni mfano halisi, hatuhitaji mshahara wala malipo.
Kwanza kwa invisible ni kumdhalilisha, kazi anayoifanya hapa na private ni kubwa sana na hakuna mtu anaweza kumfidia (i.e compensation) hivyo hawezi kudhalilika na pesa ya Mengi. Hata Kubenea na Mwanakijiji si watu wa bakuli la ombaomba wamejitosheleza kwa kuwa wao wanafahamu kiasi katika maisha!!! Wote hao wana uchungu na nchi hii na rasilimali zake kama ilivyo mimi maana long run impact ya ufisadi ni mbaya sana kwa nchi ya Tz. Nashangaa kwa nini tunatetea mafisadi bila ku think twice!!!!
Well done and congrats Mkuu Invisible, Kubenea, Mzee Mwanakijiji na wale wote ambao ni wazalendo halisi wa Tz.