Jedwali la RA: Nani hayumo?

Jedwali la RA: Nani hayumo?

Dr Salim Ahmed Salim, Jaji Warioba na JSMalecela nao hawamo!
 
Nani anasimamia mradi wa Mwananchi Gold na ule wa Matinje Gold ulioko Igunga?
 
Yusuf Makamba=Katibu mkuu CCM [a] from RC=> kumsaidia Manji kupata ubunge kigamboni[uraia ukamtemesha], Manji=RA=> fadhila ukatibu mkuu

Mulla =Mwenyekiti CCM(M) Mbeya..[a]

Sumry=Mbunge S'wanga ...[a]

Mudhihir ?
 
Kuna wimbo mmoja uliimbwa na kwaya ya Bulyankulu Barabara ya 13 uitwao "Samson". Sehemu ya wimbo huo nikikumbuka inasema:

"Tafadhali niambie asili ya nguvu zako, tafadhali niambie waweza kufungwa na nini?" alilalamika mwanamke wa Kifilistina. Sasa, simlinganishi RA na Samson Mnadhiri wa Mungu ila kwenye hili suala la nguvu ambazo inaonekana hazidhibitiki!

Nikiwa nafikiria hilo nikakumbuka mambo ya kuchora majedwali ambamo unaweka makundi ya vitu mbalimbali na ndipo wazo limenijia. Yawezekana ili kuweza kuelewa nguvu za RA ni lazima tuchore jedwali moja hivi na kujaribu kuweka ndani yake watu ambao wanahusiana au wamehusiana moja kwa moja na RA na sasa watu hao wako madarakani au kwenye nafasi fulani za maamuzi.

a. Wale aliowafadhili na kuwasaidia kushika au kudumisha nafasi za kisiasa.
Kundi hili litakuwa na wale wote ambao aliwasaidia wakati wa kampeni au kuwafadhili na kuwasaidia kushika nafasi za kisiasa. Wabunge, Wagombea wa Urais n.k Yaani hapa ni jumla ya wanasiasa ambao wamepata ufadhili kwa RA.

MATOKEO:
1. Jakaya M. Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2.Benno Malisa - (a) - Makamu Mwenyekiti- TAIFA, UVCCM
3.Sofia Simba - (a) - Mwenyekiti Taifa- UWT(CCM)
4. Prof. Juma Kapuya - Waziri wa Kazi & Maendeleo ya Vijana (Mbunge Urambo Magharibi)
5. Adam Malima - (a) - Naibu Waziri, NISHATI NA MADINI (Mbunge, Mkuranga)

b. Wale ambao wamewahi kuwa watumishi wake kwenye Vodacom.
Akiwa ni mmoja wa wenye hisa kubwa pale Vodacom (ingawa nasikia alikuwa na mpango wa kuuza hisa hizo) kuna watu ambao wamewahi kufanya kazi Vodacom au kupewa mkataba wa kazi Vodacom. Watu hao wengine wameenda na kuwa na nafasi za kisiasa (yawezewa kuwa kwenye "a" hapo juu). Kama mtu anatokea kwenye "a" na anatokea kwenye "b" basi wawekwe vile vile.

MATOKEO:
1.Pius Msekwa - Vodacom B. - Makamu wa Mwenyekiti CCM (Bara)
2. William Ngeleja - Vodacom - Waziri wa Nishati na Madini
3. Dr. Idris Rashid (Vodacom) - Mkurugenzi Mtendaji Tanesco

c. Wale ambao wametumika kwenye vyombo vyake vya habari
Hawa ni wale ambao kwa namna moja au nyingine wamewahi kuwa na ubia pamoja au utumishi wa vyombo hivyo vya habari na sasa hivi wako kwenye nafasi fulani fulani za kisiasa au za kiserikali. Hapa ninawaondoa watumishi ambao wanafanya kazi tu kwenye vyombo vyake vya habari. Msisitizo ni wale waliovuka toka kwenye vyombo vya habari kwenda kwenye serikali au siasa.

d. Wale wenye ushirikiano wa kibiashara.
Kundi jingine ni la wale ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa na mahusiano ya kibiashara na RA au makampuni yake mengine na hawa nao wametoka huko na sasa wana nafasi serikalini (idara, wizara au wakala mbalimbali). Na nafasi zao kwenye idara hizo.


Jinsi ya kufanya:
Bila kuweka maelezo mengi, linatajwa
Jina (Salva Rweyemamu);
kundi lake (c)
na nafasi yake ya sasa (Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais).

Nitaendelea kuupdate tunayoyapata labda tunaweza kuona pattern ya aina fulani hivi ikijitokeza. Ukiweza kuweka na some kind of the story behind ya chaguo lako that will help too to make sense.

Baada ya hapo tutachora majedwali ya watu wengine wawili halafu tutaona hiyo picha inayotokea inatuonesha nini. Yawezekana kuna kitu ambacho tumekimiss kwa muda mrefu juu ya RA na nadharia niliyonayo yaweza kuthibitika kisayansi juu ya "asili ya nguvu yake".

Kama huna lolote unalojua; sit down and enjoy!

Mkuu Mkjj hiyo sehemu inaitwa "ULYANKULU", mi nimewahi kuishi karibia na kambi hiyo ya wakimbizi kutoka Burundi. Japo naju hili halijaharibu maana nzima ya thread ila BULYANKULU ni tofauti kabisa na ULYANKULU, the former ni mgodini nafikiri itakuwa ni maeneo ya Nzega while the later ni Wilaya ya URAMBO kama sikosei ni kambi ya wakimbizi. ni hayo tu
 
Hon. H.E Dr. Jakaya Mrisho Kikwete (a) - President of URT and Chief of the Army.

Chief of the Army- Davis Mwamunyange? au, kama ni JK yeye ni Commander In Chief. Ni katika kuweka maelezo sawa sina ninalolijua zaidi ya haya niliyosahihisha.
 
Tanzania inaongozwa kama shamba la bibi,mafisadi wanawafadhili viongozi unategemea nini zaidi ya kuiba na kuambiwa warudishe walichoiba basi.
 
RA - NA CCM
Mwanakijiji thread yako ina mvuto sana tu.
Kwa mtizamo wangu tukimwangalia Rostam kama Rostam hatuwezi kupata picha kamili bila ya kumuusisha na CCM.

RA Aliingia CCM kama mtu wa kawaida tu. Lakini CCM Ndiyo iliyomtengeneza huyu RA tunayemwona sasa hivi. Rostam alipewa wadhifa wa mweka Hazina ndani ya CCM, Kazi yake ilikuwa kupitapita kwa jamaa yote ya waasia walioko Tanzania ambao wanazo ili wachangie Chama cha Mafisadi, Katika uchangiaji wake waasia hao wamekuwa wakinufaishwa sana na wadanganyika wanaoingia madarakani kwani wanatambua michango yao, wamekuwa wakinufaishwa katika Tenda, misamaha ya kodi na upendeleo wa kila aina ,na wakati mwingine hutumiwa kupitisha fedha chafu za Mafisadi Hao. Watu kama Chande, Jeetu Patel ,Somaia na wengine ni wanufaikaje wakubwa sana na syndicate ya Mafisadi. Kwa upande mmoja utaona kama rostam ndiye aliyekuwa akiwasaidia watu mbalimbali, ukweli ni Tofauti , yeye alikuwa agent tu wa CCM .Na CCM iliposhindwa kutimiza bajeti ya kampeni hapo ndipo hutumia nguvu zake ndani ya serikali na RA ndo msimamizi wa fedha yote. Na ndiyo maana kila kona ambayo serikali ya CCM imetia mkono kuchukua fedha RA yupo. Na hili hata wao wanajua kuwa yeye ni Mastemind wa syndicate tu lakini inawahusisha watu wengi, hapo tujiulize kitu kimoja yeye hajawahi kuwa na Auhtority yeyete ndani serikali lakini anayo nguvu mpaka serikalini ya kuchota fedha , ni nani amempa hiyo jeuri? ni wao hao hao wanaoshikilia dola.
ROSTAM NI CCM NA CCM NI KAGODA NA KAGODA NI KIKETWE.

KIMAHESABU,
KIKWETE(AS PRESIDENT)=f(RA,CCM,KAGODA:EPA)

NIMEWASILISHA
 
amekaa kwenye board ya NSSF lini na kama nani? hebu fafanua hii
Kapuya amekwishakuwa waziri wa kazi na yeye ndie mwenye kupendekeza kwa Rais nani awe Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF na kama waziri huteua wajumbe wa bodi!! Kwa taarifa tu akiwa waziri mwenye dhamana, alimpetekeza Siraju Juma Kaboyonga akawa mwenyekiti wa NSSF wakati Manji anakomba fedha za wafanyakazi. Na kaboyonga sasa ni mbunge wa Tabora mjini anayewatetea mafisadi bungeni[ Mtetezi wa kampuni iliyokodisha reli RITES na mmoja wa wapinzani wakuu wa hoja za DR. Slaa]. GT kwahiyo Kapuya anaproxies!!
 
naona bado uko kwenye vitendawili na hadithi

na narudia mwacheni Mwamvita Makamba peke yake kama alivyo

Wana JF tuwe makini, tusije jikuta tunatoana macho humu, wewe ulimtaja Mwamvita angalia usije gombana na mumewe bure!.

GT nafikiri watamwacha turudi kwenye mada ya Jedwari la RA.
 
Au tuseme nchi hii ina Rais (aliye Ikulu) na pia ina Mgawa Madaraka a.k.a King-maker a.k.a RA a.k.a untouchable?
 
Ndo mambo yalivyo TZ yetu hii bwana.Si waziri amekataza kutaja mafisadi kwasababu hatuna mamlaka? Mkuu angalia, hili jedwari kama lina baraka za waziri wa utawala bora.
huyu mama ameamua kutaifisha haki ya kikatiba ya kila mtanzania kwenye suala moja tu....kuwataja mafisadi. Kusema mambo mengine ruksa sio kutaja mafisadi!!
 
Watanzania tusiwe wajinga kiasi hicho kufikiri matatizo ya Tanzania ni ya mtu mmoja badala ya system nzima ambayo ni mbovu na imeshindwa kutimiza majukumu yao. Hii ni tabia ya watu ambao wanashindwa kukubali part yao katika failures hizi mbalimbali na badala yake wanakimbilia kutafuta scapegoat.

Hata leo akifa RA ufisadi hautaisha Tanzania. Ni siasa za mufilisi kuamini kwamba nchi inayumba shauri ya mtu mmoja. Huyo RA hajaenda kuiba bank kwa mtutu au hajawafunga kamba viongozi wetu, amefanya anayofanya kwa kutumia watu ambao sisi wenyewe wengi wetu tukiwepo hapa JF tumewaweka serikalini pamoja na makosa yao mengi ya huko nyuma.

Miaka 20 iliyopita hakukuwa na ufisadi na bado nchi ilikuwa maskini pamoja na jitihada kubwa za watu kama Nyerere. Sasa badala ya kuelemisha jamii juu ya tufanye nini ili kuwasaidia wananchi wengi hasa wa vijijini ambao wanaishi kwa dhiki kubwa, kushuka kwa elimu, huduma mbovu za afya, mifuko iliyotoboka, sisi tunatumia zaidi ya 90% ya muda wetu kumjadili mtu mmoja tena with zero result.

Watu hao hao ambao kwa wakati mbalimbali walikuwa wakishirikiana na RA huku wakijua madudu yake, leo wanajifanya ni vinara wa kutuambia matatizo ya TZ ni RA.

Ili Tanzanzania iende mbele ni muhimu sisi sote nikiwemo mimi mtanzania, tujiangalie tena kwa kioo na kuona vipi tunaweza kubadilika na kutenda haki kwa watu wetu, kabla ya kummulika mtu mwingine kwa kioo hicho, tujimulike sisi kwanza. Tuna uwezo wa kubadili matendo yetu kabla ya kubadili matendo ya mtu mwingine.

Ni sawa ni vizuri kuweka pressure kupambana na madhambi mbalimbali katika jamii lakini sio kwa kiwango cha sasa cha upotoshaji kuonyesha kwamba kama sio RA nchi ingekuwa na mabomba yanayotoa maziwa. Nenda kwenye kampuni zozote za Tanzania au institutions za serikali au hata kwenye majumba ya wasomi, utagundua madudu lundo tu kwa muda mfupi. Je na huko nako RA ndiye anatutuma?

RA tumemtengeneza wenyewe shauri ya tamaa zetu za haraka haraka na kufikiri maisha bora yanakuja kwa ujambazi. Kuamua kusaliti mamilioni ya wananchi waliotupa nafasi ili tujilundikie mapema na kuishi kama tuko ahera. Leo sisi Watanzania wote tukiamua kutimiza wajibu wetu, hao akina RA hawatakuwepo.

Ni nani mbunge wa CCM ambaye anaweza kuapa kwa mungu kwamba hakufaidika na mapesa yaliyooza ya Rostam na genge lake? Mtu akisema hivyo atakuwa anadanganya tu kama wanavyodanganya kwenye mambo mengi.

Ndio maana watu wengine tumepunguza kuchangia JF kwasababu mwelekeo sasa umeanza kuwa mtu badala ya system au fikra. Tumeanza kugeuza fikra zetu na kuanza kuwa mimi na yule au sisi na wale. Tunajaribu kwa nguvu zote bila mafanikio kuingiza pumba kwenye vichwa vya Watanzania ili waweze kuamini kwamba tatizo letu ni mtu mmoja.

Binafsi naamini mawazo kama haya hayamsaidii mtu yeyote na badala yake yanazidi tu kuligawa taifa. Lazima tutengeneze principles ambazo tuko tayari kuzisimamia na kuzilinda bila kujali aliyekiukwa na RA au Mengi. Vinginevyo na sisi wengine tunageuka kuwa vikaragosi vya hawa wababe ambao wameitumia system kufika pale walipofika na sasa wameamua kugeukana.

MTZ hapa umeeleza point ya maana sana kuwa, tuangalie system na si mtu mmoja na ndiyo maana mwanakijiji anataka tuangalie ni jinsi gani system hiyo ina connection na RA. Kwa kuwa tumeshajua kuwa yeye ndiye masterminder wa wizi unaofanywa na CCM (system) basi tuangalie ni nani ambaye hayumo?. Likipatikana jibu sasa tutaanza kuichambua system.

Kumbuka wakati wa Mwalimu ilikuwa mfanyakazi serikalini ukiwa na mali zisizolingana na kipato chako, ulikuwa unaulizwa umezipataje? una biashara au una nini cha kukufanya uwe juu ya wenzako mnaopata mshahara sawa wa shs360 kwa mwezi?. Siku hizi ukiwa na mali watu wanakuita mjanja. Sasa kama system inawalea watu kama RA kuendelea kutamba japo watu wanapiga kelele basi something is wrong katika system nzima ya TZ.

Ukianza na watu kama RA na genge lake kuna nafasi kubwa sana ya kuwabana wale wa bandarini, TRA n.k, kwani hapo sasa system itaonekana kuwa haina ombwe ila kuendelea kuwaacha hawa walio na alama za spices mikononi kutawafanya wale wanaokula kwa umma na vijiko kuwa na confidence zaidi ya kuendelea kula.

Ikumbukwe kuwa CCM ndiyo hasa mlengwa wa hii system, kitu wanachokifanya wao kama "accounting officers" wa hazina ya nchi ni kuchota na kuwapa hawa akina RA type kwa kigezo cha ufanyabiashara wao ili warudishe kama misaada kwa Chama na ionekane kuwa wamesaidiwa badala ya kuwa wamewaibia wananchi. Na huu ndiyo ukweli wenyewe kuhusu system inavyoiibia nchi na watanzania.
 
Kwikwi ... hapa umekamatika

Labda Mkijiji ongeza jedwali special la walioko kwenye payroll ya RA

Game Theory cheo mtetezi wa RA na muharibu thread JF kwa ajili ya kumtetea!

Much respect Rwabugiri!
Game Theory anajaribu kushift mada itoke kwa RA.

You can't fool all people all the time
 
While it is true that our corruption problems are systemic and do not span from a single individual, it is also true there is an individual that is almost omnipresent when it comes to corruption.This individual is none other than Rostam Aziz.The master of grand corruption.

I am one of those advocating combating this in a systemic way, but at the same time realize that if you want to kill a snake, hit it hard on the head.

Rostam is the head of corruption in Tanzania.Hit nhim hard and every petty ape corruption baron will see you mean business.

Unfortunately I am convinced that will never happen.Not under the current administration.And if it does come back here and make me eat my own words.
 
Influence ya Kapuya na NSSF ni hivi yeye kama waziri wa kazi alimchagua ndugu yake Siraju Kaboyonga ambaye alikuwa EADB kuwa mwenyekiti wa bodi na pia baada ya kumfunga Rage, kapuya huyu akamfanyia mpango kaboyonga kuchukua jimbo la Tabora mjini ambalo Rage angekuwa mbunge wake
 
Dr Dau ni Fisadi mkubwa na nitamuanika hivi karibuni,Nini alikifanya Bandari na kwanini yeye na Mkullo hawaelewani?

Walikwaruzana wapi?na kwanini nasema DAU siyo Mtu safi..Wote wezi tu na Mungu atakuja kulipa.Mie nauliza hivi hakuna waganga wa kufanya mafisadi wawe vichaa?
 
...........Ni sawa ni vizuri kuweka pressure kupambana na madhambi mbalimbali katika jamii lakini sio kwa kiwango cha sasa cha upotoshaji kuonyesha kwamba kama sio RA nchi ingekuwa na mabomba yanayotoa maziwa. Nenda kwenye kampuni zozote za Tanzania au institutions za serikali au hata kwenye majumba ya wasomi, utagundua madudu lundo tu kwa muda mfupi. Je na huko nako RA ndiye anatutuma?
.......

Hivi kuna mtu aliye-imply huo upotoshaji unaousema?.......au hapa watu wanajaribu kuonyesha/kupambana na mafisadi........
............Hivi unaijua influence ya huyu RA au unaisikia tu.......

.......wengi wetu hapa tunaelewa jinsi system nzima ilivyo mbovu...na jinsi RA et al wanavyotumia udhaifu huo (kinara wake ikiwa UONGOZI) kutufisadi
 
Back
Top Bottom