FairPlayer
JF-Expert Member
- Feb 27, 2006
- 4,145
- 723
Dr Salim Ahmed Salim, Jaji Warioba na JSMalecela nao hawamo!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna wimbo mmoja uliimbwa na kwaya ya Bulyankulu Barabara ya 13 uitwao "Samson". Sehemu ya wimbo huo nikikumbuka inasema:
"Tafadhali niambie asili ya nguvu zako, tafadhali niambie waweza kufungwa na nini?" alilalamika mwanamke wa Kifilistina. Sasa, simlinganishi RA na Samson Mnadhiri wa Mungu ila kwenye hili suala la nguvu ambazo inaonekana hazidhibitiki!
Nikiwa nafikiria hilo nikakumbuka mambo ya kuchora majedwali ambamo unaweka makundi ya vitu mbalimbali na ndipo wazo limenijia. Yawezekana ili kuweza kuelewa nguvu za RA ni lazima tuchore jedwali moja hivi na kujaribu kuweka ndani yake watu ambao wanahusiana au wamehusiana moja kwa moja na RA na sasa watu hao wako madarakani au kwenye nafasi fulani za maamuzi.
a. Wale aliowafadhili na kuwasaidia kushika au kudumisha nafasi za kisiasa.
Kundi hili litakuwa na wale wote ambao aliwasaidia wakati wa kampeni au kuwafadhili na kuwasaidia kushika nafasi za kisiasa. Wabunge, Wagombea wa Urais n.k Yaani hapa ni jumla ya wanasiasa ambao wamepata ufadhili kwa RA.
MATOKEO:
1. Jakaya M. Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2.Benno Malisa - (a) - Makamu Mwenyekiti- TAIFA, UVCCM
3.Sofia Simba - (a) - Mwenyekiti Taifa- UWT(CCM)
4. Prof. Juma Kapuya - Waziri wa Kazi & Maendeleo ya Vijana (Mbunge Urambo Magharibi)
5. Adam Malima - (a) - Naibu Waziri, NISHATI NA MADINI (Mbunge, Mkuranga)
b. Wale ambao wamewahi kuwa watumishi wake kwenye Vodacom.
Akiwa ni mmoja wa wenye hisa kubwa pale Vodacom (ingawa nasikia alikuwa na mpango wa kuuza hisa hizo) kuna watu ambao wamewahi kufanya kazi Vodacom au kupewa mkataba wa kazi Vodacom. Watu hao wengine wameenda na kuwa na nafasi za kisiasa (yawezewa kuwa kwenye "a" hapo juu). Kama mtu anatokea kwenye "a" na anatokea kwenye "b" basi wawekwe vile vile.
MATOKEO:
1.Pius Msekwa - Vodacom B. - Makamu wa Mwenyekiti CCM (Bara)
2. William Ngeleja - Vodacom - Waziri wa Nishati na Madini
3. Dr. Idris Rashid (Vodacom) - Mkurugenzi Mtendaji Tanesco
c. Wale ambao wametumika kwenye vyombo vyake vya habari
Hawa ni wale ambao kwa namna moja au nyingine wamewahi kuwa na ubia pamoja au utumishi wa vyombo hivyo vya habari na sasa hivi wako kwenye nafasi fulani fulani za kisiasa au za kiserikali. Hapa ninawaondoa watumishi ambao wanafanya kazi tu kwenye vyombo vyake vya habari. Msisitizo ni wale waliovuka toka kwenye vyombo vya habari kwenda kwenye serikali au siasa.
d. Wale wenye ushirikiano wa kibiashara.
Kundi jingine ni la wale ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa na mahusiano ya kibiashara na RA au makampuni yake mengine na hawa nao wametoka huko na sasa wana nafasi serikalini (idara, wizara au wakala mbalimbali). Na nafasi zao kwenye idara hizo.
Jinsi ya kufanya:
Bila kuweka maelezo mengi, linatajwa
Jina (Salva Rweyemamu);
kundi lake (c)
na nafasi yake ya sasa (Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais).
Nitaendelea kuupdate tunayoyapata labda tunaweza kuona pattern ya aina fulani hivi ikijitokeza. Ukiweza kuweka na some kind of the story behind ya chaguo lako that will help too to make sense.
Baada ya hapo tutachora majedwali ya watu wengine wawili halafu tutaona hiyo picha inayotokea inatuonesha nini. Yawezekana kuna kitu ambacho tumekimiss kwa muda mrefu juu ya RA na nadharia niliyonayo yaweza kuthibitika kisayansi juu ya "asili ya nguvu yake".
Kama huna lolote unalojua; sit down and enjoy!
Hon. H.E Dr. Jakaya Mrisho Kikwete (a) - President of URT and Chief of the Army.
Kapuya amekwishakuwa waziri wa kazi na yeye ndie mwenye kupendekeza kwa Rais nani awe Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF na kama waziri huteua wajumbe wa bodi!! Kwa taarifa tu akiwa waziri mwenye dhamana, alimpetekeza Siraju Juma Kaboyonga akawa mwenyekiti wa NSSF wakati Manji anakomba fedha za wafanyakazi. Na kaboyonga sasa ni mbunge wa Tabora mjini anayewatetea mafisadi bungeni[ Mtetezi wa kampuni iliyokodisha reli RITES na mmoja wa wapinzani wakuu wa hoja za DR. Slaa]. GT kwahiyo Kapuya anaproxies!!amekaa kwenye board ya NSSF lini na kama nani? hebu fafanua hii
naona bado uko kwenye vitendawili na hadithi
na narudia mwacheni Mwamvita Makamba peke yake kama alivyo
Watanzania tusiwe wajinga kiasi hicho kufikiri matatizo ya Tanzania ni ya mtu mmoja badala ya system nzima ambayo ni mbovu na imeshindwa kutimiza majukumu yao. Hii ni tabia ya watu ambao wanashindwa kukubali part yao katika failures hizi mbalimbali na badala yake wanakimbilia kutafuta scapegoat.
Hata leo akifa RA ufisadi hautaisha Tanzania. Ni siasa za mufilisi kuamini kwamba nchi inayumba shauri ya mtu mmoja. Huyo RA hajaenda kuiba bank kwa mtutu au hajawafunga kamba viongozi wetu, amefanya anayofanya kwa kutumia watu ambao sisi wenyewe wengi wetu tukiwepo hapa JF tumewaweka serikalini pamoja na makosa yao mengi ya huko nyuma.
Miaka 20 iliyopita hakukuwa na ufisadi na bado nchi ilikuwa maskini pamoja na jitihada kubwa za watu kama Nyerere. Sasa badala ya kuelemisha jamii juu ya tufanye nini ili kuwasaidia wananchi wengi hasa wa vijijini ambao wanaishi kwa dhiki kubwa, kushuka kwa elimu, huduma mbovu za afya, mifuko iliyotoboka, sisi tunatumia zaidi ya 90% ya muda wetu kumjadili mtu mmoja tena with zero result.
Watu hao hao ambao kwa wakati mbalimbali walikuwa wakishirikiana na RA huku wakijua madudu yake, leo wanajifanya ni vinara wa kutuambia matatizo ya TZ ni RA.
Ili Tanzanzania iende mbele ni muhimu sisi sote nikiwemo mimi mtanzania, tujiangalie tena kwa kioo na kuona vipi tunaweza kubadilika na kutenda haki kwa watu wetu, kabla ya kummulika mtu mwingine kwa kioo hicho, tujimulike sisi kwanza. Tuna uwezo wa kubadili matendo yetu kabla ya kubadili matendo ya mtu mwingine.
Ni sawa ni vizuri kuweka pressure kupambana na madhambi mbalimbali katika jamii lakini sio kwa kiwango cha sasa cha upotoshaji kuonyesha kwamba kama sio RA nchi ingekuwa na mabomba yanayotoa maziwa. Nenda kwenye kampuni zozote za Tanzania au institutions za serikali au hata kwenye majumba ya wasomi, utagundua madudu lundo tu kwa muda mfupi. Je na huko nako RA ndiye anatutuma?
RA tumemtengeneza wenyewe shauri ya tamaa zetu za haraka haraka na kufikiri maisha bora yanakuja kwa ujambazi. Kuamua kusaliti mamilioni ya wananchi waliotupa nafasi ili tujilundikie mapema na kuishi kama tuko ahera. Leo sisi Watanzania wote tukiamua kutimiza wajibu wetu, hao akina RA hawatakuwepo.
Ni nani mbunge wa CCM ambaye anaweza kuapa kwa mungu kwamba hakufaidika na mapesa yaliyooza ya Rostam na genge lake? Mtu akisema hivyo atakuwa anadanganya tu kama wanavyodanganya kwenye mambo mengi.
Ndio maana watu wengine tumepunguza kuchangia JF kwasababu mwelekeo sasa umeanza kuwa mtu badala ya system au fikra. Tumeanza kugeuza fikra zetu na kuanza kuwa mimi na yule au sisi na wale. Tunajaribu kwa nguvu zote bila mafanikio kuingiza pumba kwenye vichwa vya Watanzania ili waweze kuamini kwamba tatizo letu ni mtu mmoja.
Binafsi naamini mawazo kama haya hayamsaidii mtu yeyote na badala yake yanazidi tu kuligawa taifa. Lazima tutengeneze principles ambazo tuko tayari kuzisimamia na kuzilinda bila kujali aliyekiukwa na RA au Mengi. Vinginevyo na sisi wengine tunageuka kuwa vikaragosi vya hawa wababe ambao wameitumia system kufika pale walipofika na sasa wameamua kugeukana.
Kwikwi ... hapa umekamatika
Labda Mkijiji ongeza jedwali special la walioko kwenye payroll ya RA
Game Theory cheo mtetezi wa RA na muharibu thread JF kwa ajili ya kumtetea!
narudia tena....
Lini Kapuya alikaa kwenye bodi ya NSSF? Kama nani?
its that simple
Hayumo CCM au Serikalini!
...........Ni sawa ni vizuri kuweka pressure kupambana na madhambi mbalimbali katika jamii lakini sio kwa kiwango cha sasa cha upotoshaji kuonyesha kwamba kama sio RA nchi ingekuwa na mabomba yanayotoa maziwa. Nenda kwenye kampuni zozote za Tanzania au institutions za serikali au hata kwenye majumba ya wasomi, utagundua madudu lundo tu kwa muda mfupi. Je na huko nako RA ndiye anatutuma?
.......