Jeff Bezos na wenzake wafanikiwa kurudi duniani baada ya kusafiri anga za juu

Machame Juu

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2013
Posts
1,514
Reaction score
3,363
Tajiri namba moja duniani Jeff Bezos, kaka yake, kibibi kizee miaka 82 na kijana mdachi miaka 18 wamefanikiwa kurudi duniani baada ya kusafiri anga za juu/mbali kwenye chombo chao The new Shephard.

Safari iyo ya dakika 15 tu iliyogharimu mabilion. Kwa dakika moja walivyokuwa angani iligharimu dollars za kimarekani 550 million piga mara 15. Wafanyakazi wake wa Amazon wanalipwa dollar 12 kwa saa. Mabilion ya wanadamu wenzake duniani wanaishi chini ya dollar kwa siku na hata mlo mmoja shida.

Ndo maana watu wengi waliwaombea wasirudi duniani wapotelee huko huko milele. Afadhali mke wake waliyetalakiana amejotolea kugawa mabilioni kwenye charity kusaidia chakula na scholarship kwa wasiojiweza.

Ila yamerudi salama duniani. Dua la maskini halimpati tajiri.
 
Tajiri namba moja duniani Jeff Bezos, kaka yake, kibibi kizee miaka 82 na kijana mdachi miaka 18 wamefanikiwa kurudi duniani baada ya kusafiri anga za juu/mbali kwenye chombo chao The new Shephard.

Safari iyo ya dakika 15 tu iliyogharimu mabilion. Kwa dakika moja walivyokuwa angani iligharimu dollars za kimarekani 550 piga mara 15. Wafanyakazi wake wa Amazon wanalipwa dollar 12 kwa saa. Mabilion ya wanadamu wenzake duniani wanaishi chini ya dollar kwa siku na hata mlo mmoja shida.

Ndo maana watu wengi waliwaombea wasirudi duniani wapotelee huko huko milele. Afadhali mke wake waliyetalakiana amejotolea kugawa mabilioni kwenye charity kusaidia chakula na scholarship kwa wasiojiweza.

Ila yamerudi salama duniani. Dua la maskini halimpati tajiri.
Nimetazama nikasikitika hata hawakuizunguka dunia ni kama vile wamerusha juu halafu wakarudi. Nikamuonea hurumajamaa aliyenunua siti kwa dollar sijui milioni 20, yani amefanana yulle mtu anayenunua malaya kwa pesa nyingi halafu within no time wazungu hao na pesa imeenda hivi hivi.
Mimi nilidhani wataingia space waizunguke dunia, kumbe ilikuwa tu wanavuka mstari ambao umekubaliwa kwamba ukiuvuka umeingia kwenye space basi na kurudi.
Mkuu hiyo ya mabilion ya watu kuishi chini ya dollar moja siyo jukumu lake maana pesa kaitafuta mwenyewe hajapewa hivyo ni uamuzi wake kusaidia au kutosaidia. Serikali yako yenyewe inaona bora kununua ma v8 wakati hakuna madarasa na hapo pesa hawajaitafuta wenyewe bali ni kodi unayoitoa wewe
 
Mkuu siyo dollars millions 20 bali dollars millions 28 na tena ilikuwa mnada jamaa alishinda huo mnada na kupata iyo siti kulikuwa na watu kibao wanagombania.
 
Hizo dola 550 kwa dakika si kuna watu wamelipwa?
Kuna watu wana mawazo ya ajabu sana, as if hizo fedha jamaa amezigeuza kuni akachomea mishkaki, kumbe kuna ajira zimepatikana ktk hiyo project, kuna kodi imelipwa, kuna watu wemetengeneza hela na wanaendelea kutengeneza hela kwa sababu ya hilo tukio na sasa jamaa wanazungumzia juu ya space tourism kwa wale watakaoweza wakati wengine wanaenda kuangalia simba na swala wenye fedha waende huko juu wakaone yanayoendelea.
 
Nikajua wanaenda kukaa uko miezi
 
Mkuu siyo dollars millions 20 bali dollars millions 28 na tena ilikuwa mnada jamaa alishinda huo mnada na kupata iyo siti kulikuwa na watu kibao wanagombania
Yah niliona mnada ulianza na dollar milion 4, ila kaharibu pesa tu mimi nilidhani wataingia kwenye orbit wazunguke dunia yani sijaona kitu cha kulipia pea hiyo yote kwa kurushwa juu na kurudi chini
 
Atazileta huko kwa wenye njaa waanze kugawana na kununulia magari ya washa washa.
 
Kama kapata utajiri kwa njia halali nampongeza ila kwa ulimwengu wa roho kwa kutesa wengine nalaami.
 
Yah niliona mnada ulianza na dollar milion 4, ila kaharibu pesa tu mimi nilidhani wataingia kwenye orbit wazunguke dunia yani sijaona kitu cha kulipia pea hiyo yote kwa kurushwa juu na kurudi chini
Walichotaka ni kuhisi ile weightlessness kwa dakika tatu. Pia walitaka kuwa katika historia kuwa wasafiri wa kwanza kwa Blue Origin ndani ya New Shepherd.
Jeff yeye alitaka kuaminisha watu kwamba kampuni yake inafanya kitu halisi akamleta na kaka yake, huyo mama mwenye miaka 82 wamempa nafasi kwa vile enzi za ujana wake NASA ilimkatalia kuwa astronaut sababu ni mwanamke, huyo dogo Daemen ni mwanafunzi wa Physics baba yake ni real estate billionaire kalipa hela ili dogo atimize ndoto zake za kusafiri nje, uenda ndio vitu atasoma.
 
Safari iyo ya dakika 15 tu iliyogharimu mabilion. Kwa dakika moja walivyokuwa angani iligharimu dollars za kimarekani 550 piga mara 15. Wafanyakazi wake wa Amazon wanalipwa dollar 12 kwa saa. Mabilion ya wanadamu wenzake duniani wanaishi chini ya dollar kwa siku na hata mlo mmoja shida.
Sasa mbona hela kidogo hivyo? Yaani US$ 550 x 15 tu?
 
Back
Top Bottom