Analeta hoja zake za kukaririshwa kuhusu charity, tangu ameitwa mnyonge anaishi Kwa ndoto za kusaidiwa na kama haya ndo mawazo yake atakuwa maskini mpaka kizazi chake cha nne. Jambo asilolijua ni kwamba Bezos Yuko kwenye marketing strategies ya hiyo project yake ya space. Huyu ndo wale ukimpita njia anatembea Kwa mguu usipompatia rift ataongea siku nzima hizi akili za kimaskini mbaya Sana.Mleta mada anapigwa na vitu vizito hahahaha
Huyu jamaa namfanananisha na wazigua kipindi nimeanza shughuli za kilimo Huko Handeni baada ya kuniuzia mashamba walisema sitoyalima, nilipolima wakasema analima mahindi yote haya ya nini, Kwa kuwa wao akilima sehemu ya kupata chakula amemaliza.
Huyu jamaa Hana tofauti na wale majirani ambao ukijenga nyumba kubwa utasikia linyumba lote Hilo la nini? Ukisomesha wanao shule nzuri utasikia ana mihela ya kuharibu.
Sasa ndo huyu jamaa ana roho ya kimaskini na ya kichawi ndo maana anatamani Bezos apate ajali. Acha aendelee kupasua mayai njia panda