Jeff Bezos na wenzake wafanikiwa kurudi duniani baada ya kusafiri anga za juu

Kwa hayo maelezo yako na figure ulizotoa mbona ni hela ya kukodi UBER, anyway kila MTU ana matumizi yake kulingana na hela yake, Kwa kuwa wewe hauna baiskeli haimzuii Diamond kununua Rolls Royce.
 
Kwa hayo maelezo yako na figure ulizotoa mbona ni hela ya kukodi UBER, anyway kila MTU ana matumizi yake kulingana na hela yake, Kwa kuwa wewe hauna baiskeli haimzuii Diamond kununua Rolls Royce.
550 million dollars kwa dakika ni hela ya kukodi Uber? Barabara ya mwendo kasi iligharimu 400 million dollars na watu walipiga gharama halisi ilikuwa 250 million dollars. Daraja la salender iligharimu 500 million dollars. Sasa hawa kuwa angani kwa dakika tu 550 million dollars wamekaa dakika 15 tu 550 m dollars x15 kama siyo kukufuru ni nini?
 
Kubali ulikosea kuandika mwanzo siyo uedit ndo urudi, wewe uliandika Dola 550 Kwa dakika mara dakika 15 ni Sawa USD ngapi? Japo kwangu hii Stori siyo ngeni nilijaribu kukurejesha kwenye umakini na ndo maana nika kuquote
 
Point! Jamaa anashadadia utazani alisaidia kumtafutia pesa Jeff. Kutoa ni kuzuri lakini pia ni hiyari yake.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Tafuteni zenu ndo mgawe
 
Yah niliona mnada ulianza na dollar milion 4, ila kaharibu pesa tu mimi nilidhani wataingia kwenye orbit wazunguke dunia yani sijaona kitu cha kulipia pea hiyo yote kwa kurushwa juu na kurudi chini
Pesa anazo
 
Ndo tukazane kutafuta hela unyonge sio sifa nzuri
 
Maafrika ni mambwa kabisa,wewe unafikiri matumizi ni kuhonga tu na kunywa vibia uchwara

Kwa taarifa yako Jeff anakwenda kuvuna mabilioni kwenye huo mradi wake wa space

Ni suala tu la muda ila ana uhakika wa kulamba mabilion ya $$$$$ ndani ya kipindi kifupi sana

Habu fikiria kama akina Vasco da gama na wenzake wasingetumia mabilion kutangatanga baharini leo hii ulaya pangekuwa na hali gani
 
Mabilion ya wanadamu wenzake duniani wanaishi chini ya dollar kwa siku na hata mlo mmoja shida.
Kote ulikuwa sahihi lakini hapa umeharibu and I seriously hate this kind of mindset.

Mawazo ya masikini siku zote anadhani mtu akiwa tajiri basi ni wajibu wake kusaidia masikini, kitu ambacho ni ujinga hata kukifikiria.

Masikini ni masikini kwa sababu ya uvivu wake wa kufikiri na makosa yake yeye mwenyewe na hakuna wa kumlaumu.
Na tajiri ni tajiri sababu ya akili na jasho lake mwenyewe na hivyo sio wajibu wake kusaidia yoyote yule.

Considering kila mtu amezaliwa peke yake na ana malengo yake duniani so no damn's given.

Na ndio maana utakuta masikini wengi wanaishia kulaumu serikali.

Kama nia yako ya kuwa duniani ni kusaidia masikini basi kuwa tajiri then be it kama ni rahisi.
 
Unajua ana charity ngapi duniani? Masikini wengi sijui mkoje? Wivu tu.
 
Tafuta zako usimpangie matumizi
 
Kufuru ni kwako mkuu.

Yaani unataka kulinganisha uchumi wa marekani na utajiri wa jeff na Tanzania?

You can't be serious.
 
Wenzetu wamefika huku wakati sisi tupo busy kumnyonga mnyonge kwa kumuongezea tozo zisizo na kichwa wala miguu!!
 
Unajua ana charity ngapi duniani? Masikini wengi sijui mkoje? Wivu tu.
Ana mawazo ya kimaskini kama mwendazake aliye taka matajiri waishi kama mashetani. Kwa kifupi kwa kuwa yeye alikua maskini aliwachukia matajiri na kutaka kila mtu maskini/mnyonge kama yeye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…