Jeff Lea: Simba hamfiki mbali kwa ulinzi ule

Jeff Lea: Simba hamfiki mbali kwa ulinzi ule

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2015
Posts
1,479
Reaction score
3,788
Akiongea leo asubuhi katika kipindi cha michezo cha Efm, mchambuzi nguli wa mpira Jeff Lea asema kwa safu ile ya ulinzi wa Simba dhidi ya Dodoma Jiji jana, mabeki wao wameonesha udhaifu mkubwa sana hivyo kama watakutana na timu yenye washambuliaji wazuri basi hawatafiki mbali katika ligi ya mabingwa Afrika.

Mimi namuunga mkono kwa 100% kwa mbaaaali naona mtu akienda kuchezea goli 5 kwa kila mechi ya ugenini.

Msijenge chuki, fanyieni kazi mapungufu yenu Simba
 
Akiongea leo asubuhi katika kipindi cha michezo cha Efm mchambuzi nguli wa mpira jeff lea asema kwa safu ile ya ulinzi wa simba dhidi ya Dodoma Jiji jana, mabeki wao wameonesha udhaifu mkubwa sana hivyo kama watakutana na timu yenye washambuliaji wazuri basi hawatafiki mbali katika ligi ya mabingwa afrika...
Hii Ndio shida ya wachambuzi wa bongo, ni watu wa matukio. Ukuta wa simba umecheza mechi nne za mtoano imeruhusu goli moja tu za mashindano ya CAF championship.

Afu Leo unaongea kama umejisahulisha eti kwa ukuta ule wa simba itaenda kupigwa goli nyingi.
Simba ina mabeki 5 wa kati, hapo sioni point yoyote ya msingi
 
Simba imecheza mechi 16 za ligi kuu imeruhusu magoli 6 imeruhusu magoli machache kuliko timu yoyote, imecheza mechi nne za champions league na kuruhusu goli moja tu, ikacheza mechi mbili za simba super cup ikaruhusu goli moja. Tatizo la wachambuzi wa kibongo wanasubiri matukio, Onyango akosee au Wawa akosee wapate pa kukosoa.

Na wanajitahidi sana kuficha statistics. Mpira ni mchezo wa makosa, hadi league ya Uingereza kuna magoli ya kizembe yanatokea. Kabla ya goli la jana simba mara ya mwisho kuruhusu goli kwenye ligi ilikuwa ni mechi ya Yanga (penalt ya Sarpong) sasa sijajua wanataka simba isifungwe kabisa ili wajue kuwa ina beki nzuri.
 
Akiongea leo asubuhi katika kipindi cha michezo cha Efm mchambuzi nguli wa mpira jeff lea asema kwa safu ile ya ulinzi wa simba dhidi ya Dodoma Jiji jana, mabeki wao wameonesha udhaifu mkubwa sana hivyo kama watakutana na timu yenye washambuliaji wazuri basi hawatafiki mbali katika ligi ya mabingwa afrika...
Mlipeni Tambwe kwanza na wengine wanakuja, mtakomaje nyani wa Utopolo?

IMG-20210205-WA0002.jpg
 
Yuko sahihi, mara nyingi ninapotizama mpira kwenye vibanda hasara, huwa nawaambia watu, tuna tatizo la marking hasa kwenye robo yetu.

Utakuta Kapombe kaenda, kachelewa kurudi, mtu yuko nyuma ya mabeki wawili wa kati peke yake. Mipira ya faulo na kona ndio kabisa, tunategemea mpigaji kichwa akosee au golikipa atusitiri, hakuna mtu na mtu.

Hili kama tusiporekebisha bado kazi tunayo.

Sent from my COR-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Simba imecheza mechi 16 za ligi kuu imeruhusu magoli 6 imeruhusu magoli machache kuliko timu yoyote, imecheza mechi nne za champions league na kuruhusu goli moja tu, ikacheza mechi mbili za simba super cup ikaruhusu goli moja...
Ndugu yangu, huu mpira wenu wa takwimu una changamoto sehemu, we unaongelea karuhusu goli chache, vipi zile kosa kosa, tunakoswa koswa saana kwa uzembe, takwimu zisikuongopee, game ya jana chupuchupu iishe droo km sio manula kudaka kile kichwa cha mchezaji was dodoma jiji, game ingekuwa 2-2 ile, vipi game na platnum yule jamaa aliyebaki yeye na goli angefunga? Mchezo ungebadilika siku zile

Sisi hatutaki haya makosa ya kizembe tusubiri adui nae akosee ndio tuwe salama, hata msimu wa kuvuka makundi mpaka tunaingia makundi tulikuwa na rekodi nzuri kitakwimu km ulivyotoa ww, kipi kilitusibu wapinzanj walipoweza kubadili makosa yetu kuwa magoli?? Mwendo wa 5, 5.

Sent from my COR-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Mapenzi yanatuzidia, ni kweli wachambuzi wengi wabongo ni weupe, ila katika hili kuna ukweli, hasa ukiwa ni mtizamaji mzuri wa mpira.
Simba tuna tatizo pale nyuma.

Mpira sio mchezo wa chumbani, unachezwa hadharani na kila mtu anaona.

Nawashauri ndugu zangu game zijazo tutizame hili jambo kwa makini kuna mambo mtang'amua

Sent from my COR-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Mbali Ndiyo Wapi?
Ilipofika Simba Mpaka Sasa Hivi
Wale Hawajafika/Hawatafika Hivyo Acha Waseme Wajifurahishe
 
Mtu anayeongea bila kutoa suluhisho huwa ni maamuma tu, kama walivyo wengine.
Ndiyo kuna mapungufu kadhaa, hasa wakati wa dead balls ( kona na faulo) nadhani benchi la ufundi watalirekebisha hilo kwa kuwa sasa Wanaye parfomance analyst, sidhani kama atakuwa hajaliona hili.
NB: Upungufu upo ila sio wa kiwango ambacho yanga na wachambuzi wao wanaowapa pilau wanataka tuamini.
 
Akiongea leo asubuhi katika kipindi cha michezo cha Efm mchambuzi nguli wa mpira Jeff Lea asema kwa safu ile ya ulinzi wa Simba dhidi ya Dodoma Jiji jana, mabeki wao wameonesha udhaifu mkubwa sana hivyo kama watakutana na timu yenye washambuliaji wazuri basi hawatafiki mbali katika ligi ya mabingwa Afrika.

Mimi namuunga mkono kwa 100% kwa mbaaaali naona mtu akienda kuchezea goli 5 kwa kila mechi ya ugenini.

Msijenge chuki, fanyieni kazi mapungufu yenu Simba
Wawa is not a back but batakisi
 
Ndugu yangu, huu mpira wenu was takwimu una changamoto sehemu, we unaongelea karuhusu goli chache, vipi zile kosa kosa, tunakoswa koswa saana kwa uzembe, takwimu zisikuongopee, game ya jana chupuchupu iishe droo km sio manula kudaka kile kichwa cha mchezaji was dodoma jiji, game ingekuwa 2-2 ile, vipi game na platnum yule jamaa aliyebaki yeye na goli angefunga? Mchezo ungebadilika siku zile

Sisi hatutaki haya makosa ya kizembe tusubiri adui nae akosee ndio tuwe salama, hata msimu wa kuvuka makundi mpaka tunaingia makundi tulikuwa na rekodi nzuri kitakwimu km ulivyotoa ww, kipi kilitusibu wapinzanj walipoweza kubadili makosa yetu kuwa magoli?? Mwendo wa 5, 5.

Sent from my COR-AL10 using JamiiForums mobile app
Shida yako unataka simba icheze zisiwepo hata kosakosa langoni kwa simba, wale wote uwanjani ni binadamu kuna kuswitch ki akili huwezi ukawa perfect 100% kwenye dk 90. Na hakuna timu duniani itacheza pasiwe na kosa kosa langoni kwake
 
Mwambie huyo Jeff wanasimba tunadema hivi, kila mgonjwa na dozi yake. Ile ilikuwa dozi ya Dodoma jiji kulingana na ugonjwa wao.
 
Akiongea leo asubuhi katika kipindi cha michezo cha Efm mchambuzi nguli wa mpira Jeff Lea asema kwa safu ile ya ulinzi wa Simba dhidi ya Dodoma Jiji jana, mabeki wao wameonesha udhaifu mkubwa sana hivyo kama watakutana na timu yenye washambuliaji wazuri basi hawatafiki mbali katika ligi ya mabingwa Afrika.

Mimi namuunga mkono kwa 100% kwa mbaaaali naona mtu akienda kuchezea goli 5 kwa kila mechi ya ugenini.

Msijenge chuki, fanyieni kazi mapungufu yenu Simba
Watanzania wajinga sana! Sijui muliumbwa na udongo gani? Jeff Leah ni nani hata kama reference? He is just a nut! So far Simba ndio timu iliyo fungwa magoli machache sana kwenye VPL, Timu bora kama TP Mazembe hajafunga goli na walipata wakati mgumu sana kuipenya ile defense ya Simba. Halafu mjinga mmoja anafanya hitimisho kwa kutumia mchezo mmoja! Shame! A hilal pamoja na ubora wao walipata goli moja tu kwa Simba hii.
 
Back
Top Bottom