Jehanamu ni uhalisia au ni jambo la kupumbaza akili za watu?

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
SWALI/MJADALA: Jehanamu ni kweli "moto" usiozimika ambao Mungu atawakaanga humo watu ambao hawakufuata maagizo yake?

Mungu huyu ambaye anajitanabaisha kwamba ni UPENDO na UPENDO huo unasemwa kwamba HAUHESABU MABAYA, HAULIPI KISASI, HUSAMEHE YOTE: Ndiyo huyo Mungu wa kukaanga watu kwenye moto wa milele?

Huyo Mungu anayetaka sisi tusamehe bila kikomo (7x70) ndiyo huyo huyo au mwingine? Na amkaange Jehanamu kiumbe ili iwe nini? Purpose yake ni nini? Kama haki yake inazidi UPENDO wake basi maandiko yenyewe hayajipingi?

Karibuni tujadili na labda tujitoe kwenye mawazo yanayotufunga NIRA ya utumwa.
 
Jehhana ni jalala kubwa lililopo huko Jerusalem, hapo hula masikini na palitupwa taka mbalimbali watu mbalimbali waliuliwa na kuchomwa hapo.

Hii ndio asili ya neno Jehanam kulingana na mazingira magumu na mateso ya eneo hilo watu wa dini wakalichukua kama mfano wa hicho wakiitacho mateso kwa wenye dhambi. Hii ni kwa mujibu wa kamusi za Kibibilia.
 
Zamani kabla akili haijakomaa vizuri tukihadithiwa kuhusu moto wa jahanamu na ukali wa moto huo tuliambiwa ni mara 1000 zaidi ya moto wa dunia, yaani huu moto wa duniani tuliambiwa ni sawa na majivu tu ya huo moto wa jahanamu.
Hili lilinipa mashaka sana kuamini kama kweli kuna uwezekano wa kuwepo kwa moto mkali kwa kiwango hicho, nilipofika secondary na kusoma kuhusu nyuzi joto ya volcano ndio nikaanza kupata picha kumbe upo uwezekeno wa kuwepo moto mkali mara 1000 zaidi ya huu moto tunaoutumia hapa duniani.

Kitu kingine kilichokua kinanitia mashaka ni kuwepo kwa rekodi ya matendo yetu yote tunayoyafanya hapa duniani, nikawa nawaza hizo mishe zangu ninazozifanya kwa siku tu sijui madaftari mangapi yatajaa yakiwa yanarekodiwa, haya matendo yangu ya mwezi, mwaka mpaka kufikia miaka yote ya uhai wangu, akili ikaniambia haiwezekani kumbukumbu za matendo yangu yote yakaweza kurekodiwa maana yanaweza kujaza madaftari yote ya hapa ulimwenguni.
Ila baada kugunduliwa hard disk ya 1TB akili yangu ikaanza kurudi kwenye mstari kuwa yawezekana matendo yote ya binaabamu yakarekodiwa katika kifaa kimoja, tena kifaa hicho kikawa kidogo kama memory card au kikawa kidogo zaidi hata ya hio memory card yenyewe.
 
Mkuu,
Kama unaamini ni uongo tu unaoambiwa, basi endelea kwa wakati wako kufanya dhambi. Baada ya kufa utuletee mrejesho mambo yakoje huko. Kwa maana nyingine, ipi bora: kujiweka sawa kwa kuamini unachoambiwa, au kusubiri mpaka kufa ujionee mwenyewe, na kama moto upo kweli sijui utafanyaje?
 
Ni concept pana kidogo ambayo hiv karibun nimeanza kuifikiri upya baada ya kusoma soma maandiko ya watu tofaut tofauti.
Anayependa kusoma anaweza akatafuta kitabu kinaitwa MANY LIVES MANY MASTERS
 
Jehhana ni jalala kubwa lililopo huko Jerusalem, hapo hula masikini na palitupwa taka mbalimbali watu mbalimbali waliuliwa na kuchomwa hapo.

Hii ndio asili ya neno Jehanam kulingana na mazingira magumu na mateso ya eneo hilo watu wa dini wakalichukua kama mfano wa hicho wakiitacho mateso kwa wenye dhambi. Hii ni kwa mujibu wa kamusi za Kibibilia.
Ilichukuliwa mfano ule Ili iwe rahisi kuwafundisha watu wa eneo lile waweze elewa
 
SWALI/MJADALA: Jehanamu ni kweli "moto" usiozimika ambao Mungu atawakaanga humo watu ambao hawakufuata maagizo yake?

Mungu huyu ambaye anajitanabaisha kwamba ni UPENDO na UPENDO huo unasemwa kwamba HAUHESABU MABAYA, HAULIPI KISASI, HUSAMEHE YOTE: Ndiyo huyo Mungu wa kukaanga watu kwenye moto wa milele?

Huyo Mungu anayetaka sisi tusamehe bila kikomo (7x70) ndiyo huyo huyo au mwingine? Na amkaange Jehanamu kiumbe ili iwe nini? Purpose yake ni nini? Kama haki yake inazidi UPENDO wake basi maandiko yenyewe hayajipingi?

Karibuni tujadili na labda tujitoe kwenye mawazo yanayotufunga NIRA ya utumwa.
Kusiwepo kuwepo na jehanamu basi biblia itakuwa ni kitabu cha uongo.
Biblia ni hakika ya mambo yote yaliyo simuliwa ni lzm yatimilike
 
Katika kitabu cha Yuda 1:7
Mwandishi amezitaja Sodoma na Gomorra kuwa miji hiyo inateketezwa na moto wa milele akitumia PRESENT CONTINUES TENSE.
sasa jiulize ni kweli inateketezwa kama alivyoandika?
Ukinijibu hili takuja kufafanua kuhusu uwepo wa jehanamu na moto wa milele.
Screenshot_20220324-115238.jpg
 
Kwa ushuhuda wa waliopata neema ya kwenda na kurudi kuzimu ipo ni kitu halisi
 
Kulingana na biblia mshahara wa dhambi ni mauti wala haijawahi kuwa moto...Adamu alipofanya dhambi aliambiwa atakufa na kurudi mavumbini wala siyo motoni..
Pia kuna kipindi waisraeli walikuwa wakiwatoa watoto wao dhabibu ya kuteketezwa kwa miungu..Mungu wa Biblia alionya jambo hilo

Yer. 7:31 Wamejenga mahali pa juu pa Tofethi, palipo katika Bonde la Mwana wa Hinomu, ili kuwateketeza motoni wana wao na mabinti wao, jambo ambalo sikuamuru na ambalo hata halijawahi kamwe kuingia moyoni mwangu.
...
 
SWALI/MJADALA: Jehanamu ni kweli "moto" usiozimika ambao Mungu atawakaanga humo watu ambao hawakufuata maagizo yake?

Mungu huyu ambaye anajitanabaisha kwamba ni UPENDO na UPENDO huo unasemwa kwamba HAUHESABU MABAYA, HAULIPI KISASI, HUSAMEHE YOTE: Ndiyo huyo Mungu wa kukaanga watu kwenye moto wa milele?

Huyo Mungu anayetaka sisi tusamehe bila kikomo (7x70) ndiyo huyo huyo au mwingine? Na amkaange Jehanamu kiumbe ili iwe nini? Purpose yake ni nini? Kama haki yake inazidi UPENDO wake basi maandiko yenyewe hayajipingi?

Karibuni tujadili na labda tujitoe kwenye mawazo yanayotufunga NIRA ya utumwa.
Kissendi Nyanda NTALIMA MPANDAGOYA upo?
 
Jehhana ni jalala kubwa lililopo huko Jerusalem, hapo hula masikini na palitupwa taka mbalimbali watu mbalimbali waliuliwa na kuchomwa hapo.

Hii ndio asili ya neno Jehanam kulingana na mazingira magumu na mateso ya eneo hilo watu wa dini wakalichukua kama mfano wa hicho wakiitacho mateso kwa wenye dhambi. Hii ni kwa mujibu wa kamusi za Kibibilia.
Ni sawa. Jalala hilo la kuchoma taka liliitwa Gehena lakini taka hizo na miili ya wahalifu waliosulibiwa ilichomwa na kuteketea. Idea ya eternal torment haina mashiko.
 
Madhani ni jambo la kudikirika. Tukifa ndio tutafahamu ukweli
Mungu huyo aliyesema tumpende kwa AKILI zetu zote ndo huyo Tena tumuamini kwa hadithi za kusadikika??!! Maana yake tuweke AKILI pembeni??!
 
Mambo ya ulimwengu wa roho kuyajua ni hadi uwe na elimu ya mambo ya ulimwengu usioonekana.
Asante ila ingekuwa vema ungesema elimu hiyo inapatikana wapi au kwa namna gani.
 
Zamani kabla akili haijakomaa vizuri tukihadithiwa kuhusu moto wa jahanamu na ukali wa moto huo tuliambiwa ni mara 1000 zaidi ya moto wa dunia, yaani huu moto wa duniani tuliambiwa ni sawa na majivu tu ya huo moto wa jahanamu.
Hili lilinipa mashaka sana kuamini kama kweli kuna uwezekano wa kuwepo kwa moto mkali kwa kiwango hicho, nilipofika secondary na kusoma kuhusu nyuzi joto ya volcano ndio nikaanza kupata picha kumbe upo uwezekeno wa kuwepo moto mkali mara 1000 zaidi ya huu moto tunaoutumia hapa duniani.

Kitu kingine kilichokua kinanitia mashaka ni kuwepo kwa rekodi ya matendo yetu yote tunayoyafanya hapa duniani, nikawa nawaza hizo mishe zangu ninazozifanya kwa siku tu sijui madaftari mangapi yatajaa yakiwa yanarekodiwa, haya matendo yangu ya mwezi, mwaka mpaka kufikia miaka yote ya uhai wangu, akili ikaniambia haiwezekani kumbukumbu za matendo yangu yote yakaweza kurekodiwa maana yanaweza kujaza madaftari yote ya hapa ulimwenguni.
Ila baada kugunduliwa hard disk ya 1TB akili yangu ikaanza kurudi kwenye mstari kuwa yawezekana matendo yote ya binaabamu yakarekodiwa katika kifaa kimoja, tena kifaa hicho kikawa kidogo kama memory card au kikawa kidogo zaidi hata ya hio memory card yenyewe.
Asante kwa kuchangia. Kwa hiyo hii hadithi ya Mungu wa kutengeneza mishikaki ya binadamu huko Jehanamu waiona kuwa ni hadithi ya kuaminiwa?
 
Back
Top Bottom