Jehanamu ni uhalisia au ni jambo la kupumbaza akili za watu?

Jehanamu ni uhalisia au ni jambo la kupumbaza akili za watu?

Mkuu,
Kama unaamini ni uongo tu unaoambiwa, basi endelea kwa wakati wako kufanya dhambi. Baada ya kufa utuletee mrejesho mambo yakoje huko. Kwa maana nyingine, ipi bora: kujiweka sawa kwa kuamini unachoambiwa, au kusubiri mpaka kufa ujionee mwenyewe, na kama moto upo kweli sijui utafanyaje?
Mkuu, Mungu amesema tumpende kwa AKILI siyo kwa Hekaya zisizokubaliana na REASONING. Ukikaa kwenye mrengo huo ndio utauziwa mpaka mafuta na keki za upako!
 
Ni concept pana kidogo ambayo hiv karibun nimeanza kuifikiri upya baada ya kusoma soma maandiko ya watu tofaut tofauti.
Anayependa kusoma anaweza akatafuta kitabu kinaitwa MANY LIVES MANY MASTERS
Ukiweka link yake itawasaidia wengi.
 
Ili swali waliokufa tu ndio wana majibu yake sahihi sisi wengine tutabaki kukisia tu
 
Ilichukuliwa mfano ule Ili iwe rahisi kuwafundisha watu wa eneo lile waweze elewa
NI kweli. Lakini a finite offence demands a finite penalty. Kinyume na hivyo huyo Mungu atakuwa si Mungu wa HAKI kama anavyojieleza.
 
Kusiwepo kuwepo na jehanamu basi biblia itakuwa ni kitabu cha uongo.
Biblia ni hakika ya mambo yote yaliyo simuliwa ni lzm yatimilike
AsAnte pia kwa mchango wako. Lakini sijui ni biblia ipi unayosoma. Biblia ina matoleo (versions) mengi na imeshachakachuliwa vya kutosha. Vitabu vingi vimeondolewa kwenye mkusanyiko wa biblia. Biblia inayosomwa na wengi ni matokeo ya padri mkatoliki wa Ujerumani ,Martin Luther, muasisi wa kanisa la Lutheran, aliyeachana na na kanisa lake na kuamua kutengeneza toleo lake la biblia (Die Bibel) na kunyofoa na kutupilia mbali Aya kadhaa kutoka kwenye toleo la Kilatini (Vulgate) ambazo yeye hakuzipenda au zilimkera. Vitabu vingi vilivyo kwenye inayoitwa The Jerusalem Bible au The Catholic Bible havipo kwenye King James Bible ila wakatoliki wamebaki navyo kwenye Biblia, wanaviita vitabu vya Apokrifa ( Deuterocanonical books). Nimeeandika hayo ili mchangiaji wa Uzi wangu ufute kichwani mwako kwamba kila kilichoandikwa kwenye Biblia yako lazima tumuamini. Mengine humo watu waneongeza Aya zao kwa mawazo Yao wenyewe. Aya kadhaa unazozisoma hapo hazipo kwenye nakala za mwanzo ( nowhere to be found in the original documents). Mfuate Mungu kwa AKILI yako yote.
 
Asante ila ingekuwa vema ungesema elimu hiyo inapatikana wapi au kwa namna gani.
Vyuo vya elimu za dini, online,pia hii elimu ni pana mfano Elimu kuhusu nyota,majini, uchawi,anga,roho,nguvu zisizoonekana nk unaweza ukapakua tu hata online unapata links nyingi tu
 
SWALI/MJADALA: Jehanamu ni kweli "moto" usiozimika ambao Mungu atawakaanga humo watu ambao hawakufuata maagizo yake?

Mungu huyu ambaye anajitanabaisha kwamba ni UPENDO na UPENDO huo unasemwa kwamba HAUHESABU MABAYA, HAULIPI KISASI, HUSAMEHE YOTE: Ndiyo huyo Mungu wa kukaanga watu kwenye moto wa milele?

Huyo Mungu anayetaka sisi tusamehe bila kikomo (7x70) ndiyo huyo huyo au mwingine? Na amkaange Jehanamu kiumbe ili iwe nini? Purpose yake ni nini? Kama haki yake inazidi UPENDO wake basi maandiko yenyewe hayajipingi?

Karibuni tujadili na labda tujitoe kwenye mawazo yanayotufunga NIRA ya utumwa.
Unathubutuje kumkosea Mungu kwa Yale ayatakayo yy Kama unamuona sio wa upendo tafuta Mungu wako wa upendo umuabudu
 
Watu waovu kama Makaburu, Putin, Iddi Amin na Adolf Hitler hawataonja Jehanamu?
Yani mwisho wao ndio hapa hapa duniani?!
Hakuna kitu kama hicho Mungu kaniumbia macho na matamanio na huyo huyo Mungu akamuumba mwanamke mwenye mahips then akasema ukimtamani anakuchoma MOTO sasa ndo nini?
 
Katika kitabu cha Yuda 1:7
Mwandishi amezitaja Sodoma na Gomorra kuwa miji hiyo inateketezwa na moto wa milele akitumia PRESENT CONTINUES TENSE.
sasa jiulize ni kweli inateketezwa kama alivyoandika?
Ukinijibu hili takuja kufafanua kuhusu uwepo wa jehanamu na moto wa milele.
View attachment 2162626
Angalau wewe umetumia akili yako vizuri. Kuna watu watu wanaandika kuhusu ulimwengu wa roho lakini hata ukiwauliza ulimwengu wa roho nini sijui kama watanibu. Kwenye ulimwengu wa roho hakuna haya tuliyonayo kwenye ulimwengu wetu. Hakuna wakati (time). It is another plane of existence. Milele inayotajwa kwenye Biblia ni lugha ya picha ( metaphorical language) na haina uhusiano na sekunde,dakika masaa n.k!!
 
Tatizo watu wengi humu wana dadavua mambo ya rohoni kwa ufahamu wao wa kawaida! Ndugu zangu ukitaka kujua kweli Ingia katika mambo ya rohoni usitumie akili yako ya kawaida na tena mtu anafanya kutoa na vifungu vya biblia ili kuifurahisha nafsi yake!

Mambo ya Mungu ni Mambo ya Rohoni ili uweze kuyaelewa lazima uwe katika roho!

NB; Biblia haidanganyi maana kul e jehanamu zitakazoangamizwa ni Roho! kila binadamu ana roho( Ufahamu wa kiMungu wa mtu).Roho ndo imebeba kila kitu katika maisha yetu na kufanya kitokee katika ulimwengu wa uhalisia.

Mfano; Mshirikina/mganga akitaka kukuroga huwa anaipima kwanza roho yako na ndio anakwenda ku attack roho yako aki attack roho yako mfano kakutumia ugonjwa fulani ndio maana ugonjwa huo huwa unakuja katika hali ya mwili na nyama!
Hujawahi sikia mtu gafla kaumwa na kichwa tu alafu kwa heri!!

Tuwe makini ya rohoni tuyajue katika roho!
 
Ili swali waliokufa tu ndio wana majibu yake sahihi sisi wengine tutabaki kukisia tu
KaMa ni hivyo basi vitabu vyetu vya dini vina faida gani? Biblia inasema neno la Mungu ni taa ya kutumulikia ila kuondoa SINTOFAHAMU! Kusema tutajua tukifa ni kichekesho kisichokubaliana na hayo maandiko matakatifu
 
Vyuo vya elimu za dini, online,pia hii elimu ni pana mfano Elimu kuhusu nyota,majini, uchawi,anga,roho,nguvu zisizoonekana nk unaweza ukapakua tu hata online unapata links nyingi tu
Nakuelewa ila nilitaka ufafanue kwa manufaa ya wengine. Asante japo huko ulikokutaja pia usipoingia kwa Akali Kuna elimu tele za UONGO!
 
Mbona Yesu alipinga hilo kwenye mfano wa tajiri na masikini Lazaro?? Huoni uongo wa wazi unaopingana na Biblia kwenye hizo shuhuda feki??
Lakini mbona zinafanana toka kwa Shuhuda mbalimbali
 
Back
Top Bottom