Jehanamu ni uhalisia au ni jambo la kupumbaza akili za watu?

Jehanamu ni uhalisia au ni jambo la kupumbaza akili za watu?

Mkuu,
Kama unaamini ni uongo tu unaoambiwa, basi endelea kwa wakati wako kufanya dhambi. Baada ya kufa utuletee mrejesho mambo yakoje huko. Kwa maana nyingine, ipi bora: kujiweka sawa kwa kuamini unachoambiwa, au kusubiri mpaka kufa ujionee mwenyewe, na kama moto upo kweli sijui utafanyaje?
Kama kweli Mungu anafanya hayo hoja kwamba yeye ni mtenda haki basi Mungu huyo ni katili kupita maelezo. Mungu wa namna hiyo hafai kupendwa. Tumeaminishwa hadithi za ajabu sana!
 
Na huyo Mungu ambaye tunaamini anajua yote then anafanya biashara ya kuumba wanadamu na anajua baadae atapata hasara kwa binadamu kuishia kukaangwa kwenye moto, huyo ni Mungu wa aina gani? Hadithi za kujazana ujinga tu.
 
Mchungaji wangu aliwahi kuniambia hakuna sehemu ambapo ni motoni au jehanamu, peponi au mbinguni.

Pepo au jehanamu ni hali na wala si mahali. Kwa hiyo hizo sehemu hazipo kama tunavyo dhani.
 
Mchungaji wangu aliwahi kuniambia hakuna sehemu ambapo ni motoni au jehanamu, peponi au mbinguni.

Pepo au jehanamu ni hali na wala si mahali. Kwa hiyo hizo sehemu hazipo kama tunavyo dhani.
Angalau huyo alikuwa mkweli kiasi fulani. Lakini hali pia inahitaji existence. Ndipo swali linabaki MBINGUNI NI WAPI.
 
Binadamu mwenyewe mwenye UPENDO wa kibinadamu hawezi kufanya huo ukatili wa kuchoma mtu kwa moto hata kwa dakika kumi, achilia mbali kwa milele. Biblia inasema Mungu alimuumba mtu kwa sura na mfano wake. Iweje yeye Tena awe katili namna hiyo??
 
SWALI/MJADALA: Jehanamu ni kweli "moto" usiozimika ambao Mungu atawakaanga humo watu ambao hawakufuata maagizo yake?

Mungu huyu ambaye anajitanabaisha kwamba ni UPENDO na UPENDO huo unasemwa kwamba HAUHESABU MABAYA, HAULIPI KISASI, HUSAMEHE YOTE: Ndiyo huyo Mungu wa kukaanga watu kwenye moto wa milele?

Huyo Mungu anayetaka sisi tusamehe bila kikomo (7x70) ndiyo huyo huyo au mwingine? Na amkaange Jehanamu kiumbe ili iwe nini? Purpose yake ni nini? Kama haki yake inazidi UPENDO wake basi maandiko yenyewe hayajipingi?

Karibuni tujadili na labda tujitoe kwenye mawazo yanayotufunga NIRA ya utumwa.
Ni story za kakitabu kakihuni tu , Bible Ni kakitabu Fulani kakihuni Sana na kaliandikwa na wahuni Fulani hivi kwa kutumia fasihi ya juu Sana,, ukitaka kufa masikini endekeza dini
 
endelea kitenda izo dhambi utafurahii kwa mungu
 
kuna maisha baada ya kufa.
Tutakuja kufufuliwa na kwenda kuhukumiwa kuanzia Adam mpaka binadamu wa mwisho.
Tutakaa kwenye uwanja.
Kila mtu atapitia hukumu yake.
Siku hyo hakiachwi kitu.kila tendo ulilolifanya duniani utaoneshwa.
Ndipo utahukumiwa peponi au motoni
Hilo liko wazi wala sipingani nalo. Lakini nasisitiza Tena A FINITE OFFENCE DEMANDS A FINITE PENALTY. Hizi habari za Mungu kukaanga watu kwenye moto ni Hekaya za kujazana ujinga. Kwenye ulimwengu wa roho hakuna moto. Moto ili uwe moto unahitaji Oksijeni! Hiyo kwenye ulimwengu wa roho hakuna.
 
kuna maisha baada ya kufa.
Tutakuja kufufuliwa na kwenda kuhukumiwa kuanzia Adam mpaka binadamu wa mwisho.
Tutakaa kwenye uwanja.
Kila mtu atapitia hukumu yake.
Siku hyo hakiachwi kitu.kila tendo ulilolifanya duniani utaoneshwa.
Ndipo utahukumiwa peponi au motoni
Hunibu bado hoja yangu. Umekuja tu na Hekaya ulizoletewa na watu weupe
 
Haiwezekani watu wema na waovu baada ya kufa wakakaa pamoja. Mungu ni wa haki ni lazima atende haki kwa matendo yetu!
 
Kama kweli Mungu anafanya hayo hoja kwamba yeye ni mtenda haki basi Mungu huyo ni katili kupita maelezo. Mungu wa namna hiyo hafai kupendwa. Tumeaminishwa hadithi za ajabu sana!
Kwahiyo kutupwa jehanamu unaona sio haki vipi na watakao ingia peponi
 
Ni ujanja waliotumia wamisionari ili upokee imani yao iliyotungwa. Hakuna jehenamu, Mungu hawezi kuunguza watoto wake. Angalia sasa, kwa woga wako umeacha Mila yako na kufuata zao. Kwao marehemu wanakuwa watakatifu ila mwafrika wanakuwa mizimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na huyo Mungu ambaye tunaamini anajua yote then anafanya biashara ya kuumba wanadamu na anajua baadae atapata hasara kwa binadamu kuishia kukaangwa kwenye moto, huyo ni Mungu wa aina gani? Hadithi za kujazana ujinga tu.
Nooooo.We hauna future kwa sababu inaweza kuonekana. Ukiona future yako inaonekana hasa ss wanadamu ujue iyo ni past sio future. This world is like simulation game all missions are saved, utakapo zaliwa mpaka kifo.

Mungu wa kwel lazima awe na fanya mistakes nyingi mfano kuumbwa kwa lucifer ni mistake kubwa sana.
In short ukiona future yako inaonekana ujue kuna kimbe au kitu kina nguvu zaid yako kama kinakumonitor hivi.

True Most HighGod will never sees the future if does that is not the high one.
 
SWALI/MJADALA: Jehanamu ni kweli "moto" usiozimika ambao Mungu atawakaanga humo watu ambao hawakufuata maagizo yake?

Mungu huyu ambaye anajitanabaisha kwamba ni UPENDO na UPENDO huo unasemwa kwamba HAUHESABU MABAYA, HAULIPI KISASI, HUSAMEHE YOTE: Ndiyo huyo Mungu wa kukaanga watu kwenye moto wa milele?

Huyo Mungu anayetaka sisi tusamehe bila kikomo (7x70) ndiyo huyo huyo au mwingine? Na amkaange Jehanamu kiumbe ili iwe nini? Purpose yake ni nini? Kama haki yake inazidi UPENDO wake basi maandiko yenyewe hayajipingi?

Karibuni tujadili na labda tujitoe kwenye mawazo yanayotufunga NIRA ya utumwa.
Jehanamu ni dampo ambalo Wayahudi wa kale walikuwa wanachomea takataka zao ,hii tafsiri mpya ililetwa na Warumi
 
Back
Top Bottom