Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeongea vizuri sana. Hakika hawezi kujibu hoja hii.Hii ni kwa mtu mpumbavu tu.
Kwani nchi hii kuna timu ngapi hazina wachezaji wa nje?
Kama hao wachezaji wazuri wapo mbona hawachezi prisons au jkt?Je ni lazima wacheze Simba na Yanga?
Fikiria kama Akina Pacome wakina Ahoua wakipewa uraia pacha mama makwao wamejaa mnatengeneza first eleven kabisa ya ivory coast tiwe kama FranceKila jambo unalofanya wakati fulani huwa na faida au hasara. Kuongezeka kwa idadi ya wachezaji wa kigeni kumesaidia kuongeza ushindani baina ya vilabu, na pia ubora wa baadhi ya vilabu kwenye mashindano ya Kimataifa umeongezeka maradufu!
Ila ukija kwenye timu ya Taifa (ambayo haijawahi kuwa na maajabu yoyote yale hata pale idadi ya wachezaji wa nje ilipokuwa ndogo!), hali imeendelea kubakia palepale.
Nini cha kufanya!!! Mimi nashauri TFF na serikali watengeneze mpango mkakati wa kupeleka nje vijana wenye vipaji vikubwa vya soka ili kuwajengea uwezo wa kupata nafasi ya kusajiliwa na vilabu vikubwa duniani.
Lakini pia serikali ifikie wakati sasa iruhusu uraia pacha, ili wachezaji wenye asili ya nchi yetu waliopo kwenye baadhi ya nchi zilizoendelea kisoka, wapatate nafasi ya kuja kuichezea timu yetu ya Taifa huku wakibakia na uraia wa nchi zao.
Al in all, huyo Jemedari Said aache kumtafuta mchawi, huku ukweli ukijulikana ya kwamba sisi Wabongo mpira siyo kipaji! Sisi tunaweza kufanya ngono, kupiga majungu, umbea, uchawa, rushwa, wizi, ufisadi, uchawi, nk.
Nakubaliana na wewe ndugu Cashman. Pointi yako ni ya msingi sana kuizingatia. Vilabu vya soka nchii vipo vya kutosha kuanzia ligi kuu hadi ligi za mchangani. Ikiwa wenye vipaji wapo, wataonekana tu huko. Si lazima wacheze au waanzie Simba na Yanga.Hii ni kwa mtu mpumbavu tu.
Kwani nchi hii kuna timu ngapi hazina wachezaji wa nje?
Kama hao wachezaji wazuri wapo mbona hawachezi prisons au jkt?Je ni lazima wacheze Simba na Yanga?
Halafu kila kituo kipya kikifunguliwa yeye na Kitenge huwa hawakosi.Binti Kazumari hata yeye ni takataka hafai kuwa mchambuz pale Crown... Apunguzwe
Naungana na wewe, wapunguzwe wageni ili vipaji vya ndani viinuke."Naendelea kusisitiza sitaki makipa wa nje na wachezaji wa nje wapunguzwe kutoka 12 hadi wabakie 5. Kilichoitokea Kilimanjaro Stars kule Zanzibar ndio uhalisia wa soka letu".
JEMEDARI SAID, Mchambuzi CROWN FM
My intake:
Mbona ukiwaza nje ya box kama Kuna ukweli mkubwa
1. Itasaidia kuwapa nafasi wachezaji wa ndani ( scouts watazunguka kuanzia mtaa,Kijiji, kata,tarafa kusaka vipaji halisi
2. Kujengwa timu ya taifa ( kutakuwa na option kibao ya wachezaji kuitwa timu ya taifa kwenye Kila nafasi uwanjani )
3. Itapunguza upigaji kwenye usajili wa wachezaji kwa hivi vilabu vyetu pendwa, mpaka mchezaji asajiliwe ni lazima awe mchezaji kweli na sio wa kuokota au wa mkopo
4. Academy zitaongezeka maana soko la soka kwa wachezaji wazawa litaongezeka
Nk. Nk.
Hayo ni maoni yangu, Nini maoni Yako??
Karibuni