Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,433
- 8,585
Wachezaji wazawa wenye Uwezo hawapati namba dhidi ya Wageni?"Naendelea kusisitiza sitaki makipa wa nje na wachezaji wa nje wapunguzwe kutoka 12 hadi wabakie 5. Kilichoitokea Kilimanjaro Stars kule Zanzibar ndio uhalisia wa soka letu".
JEMEDARI SAID, Mchambuzi CROWN FM
My intake:
Mbona ukiwaza nje ya box kama Kuna ukweli mkubwa
1. Itasaidia kuwapa nafasi wachezaji wa ndani ( scouts watazunguka kuanzia mtaa,Kijiji, kata,tarafa kusaka vipaji halisi
2. Kujengwa timu ya taifa ( kutakuwa na option kibao ya wachezaji kuitwa timu ya taifa kwenye Kila nafasi uwanjani )
3. Itapunguza upigaji kwenye usajili wa wachezaji kwa hivi vilabu vyetu pendwa, mpaka mchezaji asajiliwe ni lazima awe mchezaji kweli na sio wa kuokota au wa mkopo
4. Academy zitaongezeka maana soko la soka kwa wachezaji wazawa litaongezeka
Nk. Nk.
Hayo ni maoni yangu, Nini maoni Yako??
Karibuni
Kibu Denis, Ibrahim Bacca
Abdulrazack hamza, Clemen mzize na wengineo wanapataje nafasi? Kama timu inapata wachezaji wa kutosha ndani ya nchi haina sababu ya kutafuta wachezaji nje...
Katika wachezaji zaidi ya 400 wanaocheza NBCPL sidhani kama wageni wanazidi hata 80 hawa wazawa 300 na zaidi hawatoshi kungeneza timu imara ya Taifa?