Haji Manara ameishiwa hoja, amesikika akimponda Bin Kazumari kuwa hajui kuongea lugha ya kiingereza, hivyo hawezi kuwa wakala wa mchezaji Farid Mussa, anasema wakala lazima ajue kimombo, akamsifia sana Oscar Oscar kuwa anajua kimombo vizuri na ndio maana anasafiri mara kwa mara nchini Marekani.
Manara amesafiri sana na Simba akiwa nje ya nchi, lini aliwahi kuonekana ama kusikika akiongea lugha hiyo zaidi ya kupiga nao picha, siku moja afanye conference kwa lugha ya kiingereza ili watu wamsikilize akijiuma uma meno, huyo Oscar anayemsifia lini aliwahi kuongea lugha hiyo, kwenda Marekani sio hoja, huyo Kitenge anashinda huko Ulaya lakini hajawahi kusikika akiongea hata siku moja, wachambuzi wanaomwaga ngeli na wanajulikana tumewaona ni Geoffrey Lea, Ibrahim Masoud, Shaffih Dauda, Edgar Kibwana, sio wewe popoma Manara, wala Kitenge wala Oscar.