Jenerali David Musuguri atimiza umri wa miaka 101 leo

Jenerali David Musuguri atimiza umri wa miaka 101 leo

MKUU wa Majeshi mstaafu nchini Tanzania, Jenerali David Musuguri maarufu ‘Chakaza’ au Mtukula, ametimiza umri wa karne moja (miaka 101) tangu alipozaliwa Januari 4, 1920.

CDF (Mstaafu) kuanzia 1980 - 1988.

Mmoja wa mashujaa wa vita vya Kagera 1978-1979.

Ameweka makazi yake Musoma Mkoani Mara.

View attachment 1668029

View attachment 1668031
Mungu mkuu, familia yake inawanawake watupu vinginevyo ingekuwa shida kwa jinsi walivyo huko.
 
Askari wana kamsemo fulani eti heshima ya askari ni kufa kwa risasi badala ya kifo cha kifala. Sijui ni kutiana moyo hususan kwa "wapiganaji" wanaotangulia mbele? Anyway, HBD kwa Kamanda.
Ni kweli.
 
Happy Birthday General Musuguli.
Kinacho wasaidia wanajeshi kuishi muda mrefu ni mazoezi waliyoyafanya na wengine huendelea na discipline ya mazoezi hata baada ya kustaafu.

Umri huu mara nyingi tuliishia kusoma kwenye bible.
 
Hawa lazima waishi maisha marefu sana kwani huduma zote za muhimu anapata, kama bado yupo kazini tu!! Ndio maana hadi leo ukiwaona bado wana nguvu tu, jana nimemuona GEN. Salakikya mkuu wa majeshi wa kwanza (1964-1974) bado mzima kabisaaa!!!!

Nadhani Mwamunyange ndio ataishi sana na ule mwili wake!!! tofauti na kada nyingine ukistafu tu ndio njia ya kifo!!kwanza kuwaza mafao tu, yanakata robo ya miaka yako uliyobakiza!!
Nina baba yangu mdogo kijijini saa hivi analima ni mstaafu (ssgt)juzi katimiza miaka 96 na ni mzima analima na bado juu ya mti anakwea na nyuvu bado anazo sema tuu meno ndio yameisha yote mdomoni hapa ninavyoongea ndio juzi watoto wamemkataza asikwee juu ya miti
 
Anaijua tarehe yake ya kuzaliwa ? Hongera zake hata hivyo kwa kutimiza karne, unavuna ulichopanda Biblia inatufundisha, ...
Tarehe anaweza asiijue,ila mwaka anaweza akaujua maana ndo Vita kuu ya kwanza ilikuwa inamalizika wakati huo.
 
MKUU wa Majeshi mstaafu nchini Tanzania, Jenerali David Musuguri maarufu ‘Chakaza’ au Mtukula, ametimiza umri wa karne moja (miaka 101) tangu alipozaliwa Januari 4, 1920.

CDF (Mstaafu) kuanzia 1980 - 1988.

Mmoja wa mashujaa wa vita vya Kagera 1978-1979.

Ameweka makazi yake Musoma Mkoani Mara.

View attachment 1668029

View attachment 1668031
Neno lake pekee la Kishujaa ambalo aliwahi Kuniambia zaidi ya mara mbili nilipomtembelea mwaka 2009 Nyumbani Kwake Butiama Mkoani Mara ( jirani na kwa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ) na akarudia kuniambia tena mwaka jana 2020 Lugalo Hospital VIP Wing alipokuwa amelazwa ni kwamba Siku zote Mwanaume unatakiwa kuwa Mpambanaji, hakuna Kukata Tamaa na Kutokuogopa chochote.

Mwishoni akamalizia Kuniambia kuwa ingekuwa ni Kashfa Kwake au Kudhalilishwa kama Nduli Idi Amin Dada angemshinda Kimedani ( Kivita ) wakati Kimsingi na Kiuhalisia ni Yeye Afande Jenerali Mzee Musuguri ( Bugozi ) ndiyo aliyemfundisha Masuala ya Kijeshi Idi Amin Dada alipokuwa Trainer ( Mkufunzi ) katika Jeshi la KAR ( King's African Rifles ) lililokuwa chini ya Wakoloni wetu Waingereza.

Hongera sana Kwake Jemedari wa uhakika Afande Jenerali Mzee David Bugozi Musuguri kwa kutimiza Kwake Umri huu mkubwa wa Miaka 101 na binafsi namuombea kwa Mwenyezi Mungu kheri ya Maisha marefu na yenye Fanaka huku Afya yake ikizidi Kuimarika na kuwa njema zaidi. Ameacha Alama kubwa sana ya Ukakamavu, Ushujaa na Uzalendo kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ )
 
Nina baba yangu mdogo kijijini saa hivi analima ni mstaafu (ssgt)juzi katimiza miaka 96 na ni mzima analima na bado juu ya mti anakwea na nyuvu bado anazo sema tuu meno ndio yameisha yote mdomoni hapa ninavyoongea ndio juzi watoto wamemkataza asikwee juu ya miti
Kwa kustaafu ssgt lazima awe mkakamavu , misoto kazi ngumu madoso

angekuwa alikuwa afisa haaaa ,
wale maisha mazuri gari kali lazima iwepo ,madoso anayaona tu kwa wasio maafisa
 
HONGERA JEMEDARI
kwa kweli ndio maana idd amin alikimbia angekamatwa na huyu mzee sijui ingekuwaje
 
Japo kifo anapanga mungu ila tujitahidi kufuata miongozo ya kiafya hasa kwenye ulaji na mazoezi kidogo siyo everyday ni kujikandia kama minyama choma hiyo na mibia ya kutosha.....jana ofisini flan nilikutana na Toto dogo tu lakin akanishangaza tumbo kubwa sanaaaaa means kitambi cha haja,manyama yametuna pembeni mwa tumbo,mashavu makubwa,anatoa mijasho tu anahema balaaa alafu mahali penyew pana ngazi ndogo tu,nikasikitika sana kwa kweli
 
Happy Birthday Major General Musuguli.
Kinacho wasaidia wanajeshi kuishi muda mrefu ni mazoezi waliyoyafanya na wengine huendelea na discipline ya mazoezi hata baada ya kustaafu.

Umri huu mara nyingi tuliishia kusoma kwenye bible.
Sio wote!!wengi wanao staff wakiwa na vyeo vidogo, huwa wanapigika sana!!ma wengi wao kuwa walevi tu, ila hao maafisa hasa kama hao ma Generali ndio wanaokula nchi atatunzwa hadi kifo!!
 
Happy Birthday Major General Musuguli.
Kinacho wasaidia wanajeshi kuishi muda mrefu ni mazoezi waliyoyafanya na wengine huendelea na discipline ya mazoezi hata baada ya kustaafu.

Umri huu mara nyingi tuliishia kusoma kwenye bible.

Mbona unamshusha cheo? Huyo ni Jenerali kamili na wala sio Meja Jenerali. Hebu cheki rekodi zako vizuri dada
 
Kuna mzee kafariki kijijin kwetu alikuwa mwanajeshi alikuwa na 102 miaka
 
Back
Top Bottom