Jenerali Mabeyo, unayasikia yasemwayo na makomandoo wetu mahakamani kwenye kesi ya Mbowe?

Hao kwa sasa sio askari wa Jwtz, wapambane na hali zao tu.
Maskini akipata kazi au pesa kidogo anafikiria ndio mwisho wa maisha

Kuna kupata ulemavu Katika magari tupandayo na tunayoendesha

Usijione umefika kwa kuwaambia ambao hawapo kazini kwa kustaafu wapambane na hali zao

Nani wa kuwapambania wazee wetu kama sio sisi tulio kazini

Leo kijana kesho nawe unazeeka

Chunga mdomo na kauli zako, omba yasikukute

Kuna wazee walipitisha Bungeni wenzao wapate pensheni ya elfu hamsini Leo wanalialia mtaani
 
JWTZ hawana sera ya kuwalinda watu ambao wanakuwa trained kwa kiwango cha Ukomandoo, hawa jamaa walitelekezwa na wamepitia wakati mgumu mno.
kuwatupa mtu mtaani watu wenye mafunzo kama hayo ni hatari. Hata kama walionekana kuchanganyikiwa na hawastahili kukaa jeshini, kuwatupa tu mtaani si sawa, Magonjwa yao karibu wote wanasema yanahusiana na akili, inawezekana ni athari za kivita - tunawatupaje?
Askati wa vyeo vya juu wanapostaafu tunaona wanapewa ukuu wa wilaya, mkoa nk. hata hawa wa chini si vibaya wakawa wanapata kaposho fulani ili kujikimu kimaisha. Kumbukeni Jerry Rawlings hakuwa na cheo kikubwa!
 
Nafikiri tungejikita zaidi kwenye kutendewa haki na vyombo vyetu.

Hao makomandoo kuteswa ni jambo moja. Lakini mbaya zaidi ni kuteswa na chombo tunachokiamini na kupewa dhamana ya usalama wa raia.

Ikiwa wanautendea hivi mti mbichi, itakuwaje kwa mti mkavu?

Hapa tungeweka pembeni tofauti zetu zote na kupiga kelele kuangaziwa kwa namna hiki chombo kinavyotekeleza majukumu yake, leo kwa makomandoo, nani anajua kesho watamwangukia nani? Anaweza kuwa ndugu yako au wewe mwenyewe.
 
CCM imeharibu kila kitu katika nchi hii. Haya yote ni matokeo ya utawala mbaya husiozingatia sheria. Pata picha Hawa watu madhila waliyopitia ingekuwa miongoni mwao kuna mtoto wa mkubwa naye angepitia haya? Hawa watu wamedhalilishwa sana. Mungu wa Isaka na Yakobo na awapiganie ila kuna watu watalipa maovu haya na vizazi vyao.
 
Sh!t hol3 country
 
Halafu inaonekana jeshi huwa linawatupa Hawa vijana wetu wakipata tatizo la akili, wakati inajulikana wanayapata huko huko jeshini. Maana mashahidi Kama watatu wanasema wakipata tatizo la akili wakiwa jeshini.
 
Duuh hii scenario kiboko
 
Kuandamana jeshini ni uhaini . Kuna njia za kudai haki huko jeshini uache maneno mengi

Umesoma vizuri maelezo ya mdau uliyemnukuu?

Unafikiri nnaongea vitu nisivyovifaham?
Kama maandamano ni kosa, wangeadhibiwa kwa mujibu wa vifungu vyao vinavyohusu maandamano na uhaini, sio kuwabambikia kesi. Maneno mengi ni maneno kiasi gani?
 
We acha tu. Mtu kama huyo unaweza dhani anamaisha mazuri Ni vile tu hapa tunatumia fake Id.
 
Halafu inaonekana jeshi huwa linawatupa Hawa vijana wetu wakipata tatizo la akili, wakati inajulikana wanayapata huko huko jeshini. Maana mashahidi Kama watatu wanasema wakipata tatizo la akili wakiwa jeshini.
Occupational health effects au Adverse health effect related to work zinatatuliwa na Boss/ mwajiri na kupewa compensation.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…