TANZIA Jenerali Tumainiel Kiwelu afariki Dunia, kuzikwa Mbezi Loius Dar

TANZIA Jenerali Tumainiel Kiwelu afariki Dunia, kuzikwa Mbezi Loius Dar

Jenerali Tumainiel Kiwelu amefariki tarehe 18 Mei 2021 na atazikwa shambani kwake Mbezi Luis Dar es salaam tarehe 22 May 2021

Bwana ametoa Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.

Pia soma
- Historia ya Jenerali Tumainiel Kiwelu

Makamanda wetu wakuu wengi tulioachiwa na Nyerere wameshatangulia mbele ya haki. Mungu aliza pema peponi rohgo ya Kamanda.

On a side note, nimeshangaa kuona JWTX bado inatumia Telex, Telegram na Fax kwa mawasiliano!!

1689688987688.png
 
View attachment 2692128
KWANINI umemkumbuka jamaa leo!?

Unaandaa akili yetu KWA lipi jipya!!?

Au ndio zile za Tumia Akili Kwamba tusubiri KWA siku chache zijazo!!?uzi wake wa majuzi eti General msaliti wa america!!?
 
KWANINI umemkumbuka jamaa leo!?

Unaandaa akili yetu KWA lipi jipya!!?

Au ndio zile za Tumia Akili Kwamba tusubiri KWA siku chache zijazo!!?uzi wake wa majuzi eti General msaliti wa america!!?
Nimesoma taarifa hii kwa mara ya kwanza leo. Kuna mambo mengi sana yanayotokea duniani kiasi kuwa taarifa nyingine kama hii hupita bila kuziangalia.
 
Hivi kumbe? yaani wengine tupo mbali sikusikia taarifa za David Musuguri ambaye naye kama tumainiel Kiwelu ameshika eneo kubwa sana maeneo ya Kimara tena pana kituo kabla ya Kibanda cha mkaa.
Pia Mayunga alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro sikumsikia muda mwingi. Ila Gen Sarakikya ingawa vita hakupigana ila naona bado tupo naye Mungu awalinde
Umenikumbusha Brigedia Mayunga, alikuwa jirani yangu mtaani pale Garden Avenue. Nyumba yake ilikuwa pale mahali ambapo panatazamana na ubalozi wa Uingereza.

Alipohama nyumba ile akaingia Mama Makinda Spika mstaafu wa bunge, pale walipojenga ubalozi wa Uingereza palikuwa na nyumba ya railway alikuwa anaishi Mzee Kitenge. Long time ago.
 
..unadhani tatizo lilikuwa kamanda wa vita, au askari aliokuwa nao hawakuwa tayari kwa mashambulizi waliyokutana nayo uwanja wa vita? huoni kwamba ana mchango wa kuleta ushindi toka Kagera mpaka Sembabule?
Ilikuwaje alipokuwa boss wa TACAIDS? Historia ina tabia ya kujirudia
 
asingeweza kuwa cdf kwa mambo aliyotufanyia wakati wa nduli

..kitendo cha Raisi Mkapa kumpandisha cheo Tumainieli Kiwelu kuwa Jenerali baada ya kuwa Mnadhimu wa Jwtz wakati wa Mwalimu Nyerere, na Alhaj Mwinyi, kinathibitisha kuwa rekodi ya Kiwelu jeshini ni ya kutukuka.
 
Jenerali pekee ambaye hakuwahi kuwa CDF

..Kiwelu pia ndiye Mnadhimu Mkuu wa Jwtz aliyetumikia kwa muda mrefu kuliko wote.

..aliteuliwa na Mwalimu Nyerere kuwa Mnadhimu Mkuu mwaka 1975 akiwa na umri mdogo wa miaka 33.

..ardhi yetu ilipotekwa na majeshi ya Uganda Kiwelu ndiye kamanda aliyepewa jukumu la kuandaa askari na kuongoza operation ya kukomboa ardhi yetu.

..baada ya kukamilika kwa operation chakaza ya kufukuza askari wa Uganda, Kiwelu alirejea makao makuu na kuendelea na majukumu ya Mnadhimu Mkuu mpaka mwaka 1980 vita ilipomalizika.

..baada ya vita Kiwelu aliteuliwa Mkuu wa mikoa kadhaa. Lakini mwaka 1988 Raisi Ali Hassan Mwinyi alifanya mabadiliko jeshini kwa kuwateua Ernest Mwita Kiaro kuwa Cdf, na Tumainieli Kiwelu kuwa CoS.

..Kiwelu alikuwa CoS mwaka 1975 mpaka 1980, na mwaka 1988 mpaka 1994, jumla ni miaka 11.
 
Hivi yule aliyeagiza mv bukoba itobolewa wakati inaelekea kuzama na ikazama kabisa alikuwa nani vile?

..ajali ya Mv Bukoba ilikuwa mwaka 1996.

..Kiwelu alikuwa RC wa Kagera mwaka 1999 mpaka 2006.

..taarifa hizo ziko ktk tovuti ya historia ya mkoa wa Kagera.
 
..Kiwelu pia ndiye Mnadhimu Mkuu wa Jwtz aliyetumikia kwa muda mrefu kuliko wote.

..aliteuliwa na Mwalimu Nyerere kuwa Mnadhimu Mkuu mwaka 1975 akiwa na umri mdogo wa miaka 33.

..ardhi yetu ilipotekwa na majeshi ya Uganda Kiwelu ndiye kamanda aliyepewa jukumu la kuandaa askari na kuongoza operation ya kukomboa ardhi yetu.

..baada ya kukamilika kwa operation chakaza ya kufukuza askari wa Uganda, Kiwelu alirejea makao makuu na kuendelea na majukumu ya Mnadhimu Mkuu mpaka mwaka 1980 vita ilipomalizika.

..baada ya vita Kiwelu aliteuliwa Mkuu wa mikoa kadhaa. Lakini mwaka 1988 Raisi Ali Hassan Mwinyi alifanya mabadiliko jeshini kwa kuwateua Ernest Mwita Kiaro kuwa Cdf, na Tumainieli Kiwelu kuwa CoS.

..Kiwelu alikuwa CoS mwaka 1975 mpaka 1980, na mwaka 1988 mpaka 1994, jumla ni miaka 11.
sio kweli, kwa maelezo maj gen ghemoge kiwelu ndio alikuwa mkuu wa command ya kyaka, alilala mbele, akamwacha Ghemoge command base.
 
sio kweli, kwa maelezo maj gen ghemoge kiwelu ndio alikuwa mkuu wa command ya kyaka, alilala mbele, akamwacha Ghemoge command base.

..Kiwelu alikuwa Mnadhimu Mkuu, na Mkuu wa operation Chakaza ambayo lengo lake lilikuwa kuyaondoa majeshi ya Uganda ktk ardhi ya Tanzania.

..baada ya kukamilika kwa operation Chakaza Kiwelu alirudi makao makuu kuendelea na majukumu yake ya Mnadhimu Mkuu wa Jwtz.

..Kiwelu angehusika na uzembe wowote vitani asingeendelea na kazi ya Unadhimu wa jeshi wakati vita ikiendelea.

..Pia asingeteuliwa na kuaminiwa kwa mara ya pili kuwa Mnadhimu, na baadae kupandishwa cheo kuwa Jenerali.

..Maraisi watatu, walitambua mchango wa Kiwelu.
 
sio kweli, kwa maelezo maj gen ghemoge kiwelu ndio alikuwa mkuu wa command ya kyaka, alilala mbele, akamwacha Ghemoge command base.
Sio kweli lakini pia hapo kwenye kamandi nadhani unamaanisha brigedi.
 
..Kiwelu alikuwa Mnadhimu Mkuu, na Mkuu wa operation Chakaza ambayo lengo lake lilikuwa kuyaondoa majeshi ya Uganda ktk ardhi ya Tanzania.

..baada ya kukamilika kwa operation Chakaza Kiwelu alirudi makao makuu kuendelea na majukumu yake ya Mnadhimu Mkuu wa Jwtz.

..Kiwelu angehusika na uzembe wowote vitani asingeendelea na kazi ya Unadhimu wa jeshi wakati vita ikiendelea.

..Pia asingeteuliwa na kuaminiwa kwa mara ya pili kuwa Mnadhimu, na baadae kupandishwa cheo kuwa Jenerali.

..Maraisi watatu, walitambua mchango wa Kiwelu.
Kiwelu, alibaki base ya Kaboya akifanyakazinya kugawa msosi na military logistics, Musuguri Mayunga Warden Kyaro ndio walioongoza infantry, huku Waitara akiongoza Airbase na Dr Mahinga akiongoza kikosi cha makomando na ndio waliofanyakazi ya mumfurumua nduli kutoka kyaka

Musuguri baada ya kuingia ikulu ya uganda na kumkosa nduli alimwacha kijana wake mtiifu Joseph na vijana 12 kulinda ikulu ya uganda, joseph ndiye aliyetawala uganda hadi alipokuja rais mteule na kijana Joseph aliendelea kulinda ikulu ya uganda kwa weledi na utii wa juu sana hadi vita vilivyoisha, huyu joseph alikuwa kijana wa jkt na mwalimu wa primary,
 
..kwa hapa Tz, kutokana na muundo, na ukubwa wa jeshi letu, cheo au rank ya juu kabisa ni Jenerali [ 4 star general ].

..Vivyo hivyo cheo cha pili kwa ukubwa ktk jeshi letu ni Luteni Jenerali [ 3 star general].

..Raisi akimpandisha askari cheo kuwa Jenerali maana yake amelenga kumteua kuwa Cdf.

..Vilevile Raisi akimpandisha askari cheo kuwa Luteni Jenerali maana yake amelenga kumteua kuwa CoS.

..Hivyo basi Cdf lazima awe the most senior General / 4 star general in active duty.

..Vivyo hivyo CoS lazima awe the most senior Lieutenant General serving in the army.

..Haijawahi kutokea ktk historia ya JWTZ kuwa na Cdf mwenye rank inayolingana na askari mwingine in active duty.

..Sarakikya alikuwa Cdf na Major General pekee jeshini. Twalipo alipoteuliwa Major General, Sarakikya aliondolewa jeshini na kuteuliwa Waziri.
Mkuu jeshini inawezekana kuwepo 4 star Generals zaidi ya mmoja ila CDF akabaki mmoja. Na pia tunaweza kuwa na Lt. Generals zaidi ya mmoja.
Rwanda tu hapo mara kadhaa wanakuwa na active duty 4 star Generals wawili.

Kwa wenzetu majeshi makubwa kuwa na full Generals wanne au watano kawaida, kila branch inaye mmoja.

Hivyo kusema Rais kumteua afisa kuwa General ni lazima amfanye kuwa CDF si lazima sana iwe hivyo.
 
..jeshini mambo yanakwenda kwa amri.

..na mwenye rank kubwa kuliko wote ndio anatoa amri, maagizo, maelekezo, kwa askari wa chini yake.

..ikitokea wanajeshi wawili wana vyeo vinavyolingana, kinachofuata ni kuangalia yupi alipewa cheo kabla ya mwenzake.
 
Back
Top Bottom