TANZIA Jenerali Tumainiel Kiwelu afariki Dunia, kuzikwa Mbezi Loius Dar

TANZIA Jenerali Tumainiel Kiwelu afariki Dunia, kuzikwa Mbezi Loius Dar

Kwanini anazikwa Dar na wakati kwao ni Moshi?
Huyu mzee kwanini wanamzika Dar? kwa nini asipelekwe kwao Moshi? Maana serikali inaweza kugharimia.
Anyway, maybe ni wish yake azikwe Dar. But I find it strange.
Nafsi yake ipumzike alipoandaliwa na mola wake.
Kijijini kwake Mamba Kokirie ni eneo dogo sana naona aliamua azikwe karibu na Miradi na mashamba yake kwani alishika maeneo makubwa na kuwekeza eneo kubwa kuliko hicho kijiji alichozaliwa, nasikia huko Bukoba na Morogoro ni maeneo makubwa, sasa akilinganisha na kupelekwa huko Kijijini mazishi hapangetosha
naona jibu zuri analo YEHODAYA
Wachaga wengi Siku hizi wanaziikwa kwenye maeneo yao Dar wanaitika wito Wa Waziri Wa Ardhi Lukuvi anasema ardhi Moshi kumejaa makaburi tu hata kufanya maendeleo kunakuwa kugumu kila sehemu makaburi tu na hawataki yahamishwe
Manispaa ya Moshi haiendelei wala kupanuka sababu hiyo kila ukigusa Ardhi unakutana na makaburi na wenyewe hawataki yahame
Kimji cha Moshi kimejibana utafikiri ujiji kwa Zitto Kabwe
 
Umezungumzia CDF ukawasahau wengine km Mkuu wa Majeshi wa 6 Robert Mboma huyu kapiganisha vita na kaingia mstari wa mbele akiwa Pilot na kachakaza ndege za Idd amini akitokea Ngerengere
Kwa vile tunamzika Mzee wetu Gen Tumainiel Kiwelu nitatafuta muda nikumegee kipigo cha Kagera au akipatikana Echolima
Jambo jingine, Generali Mboma wakati huo alikuwa Pilot na ndiye aliyeongoza kipigo kilichoziacha ndege yingi za amini kwenye uwanja wa Entebe taabani. Kama mnakumbuka ndege yetu iliyotunguliwa na majeshi yetu wenyewe kwa bahati mbaya,Rubani wa kijeshi aliyetunguliwa kwa makosa na JWTZ alikuwa ni Capt. Alexander Kaleya Mshana. Basi hawa akina mbona waliondoka Ngerere bila kutoa taarifa kwa makamanda wa vikosi vya nchi kavu (Hili lilifanyika makusudi) na wakaruka hadi Uganda. This wa the most precise target JWTZ did. hadi Amin akalalamika kwamba JWTZ ina mamluki wa kukodiwa. Kwa sababu ndege za amini zilikuwa zinajianda kuja kushambulia TZ, lakini ghafla, wakajikuta Ndege zetu zinaruka chini sana usawa wa ziwa hivyo kusababisha taharuki kubwa sana, na kwa kuwa ziliruka chini sana na kwa mwendo wa SUPERSONIC yaani mwendo unaozidi sauti zilisababisha hofu kubwa na majengo mengi ya vioo vilivunjika-vunjika na wetu wengi walitibiwa kwa Presha,wakati huo Benki kuu ya Uganda nayo ikapigwa.
Battelfield tactics zilipangwa na Col. Lupogo.

Makamnada walioongoza vita walikuwa ni Brig. Marwa, Brig. Mayunga, Brig. Kiwelu, na Brigadier Walden. Hawa ndio waliongia msituni na wapiganaji. Makamanda hawa alipata vyeo vyao hivyo kutokana na umahiri wao wa katika uongozi wa kijeshi, na wote walihudhuria mafunzo ya uongozi wa kijeshi ndani na nje ya nchi
................. itaendelea nimeinukuu mahali ................................
Uko sahihi Lupogo alikuwa namba mbaya kwenye MK yaani Medani ya kivita ni anzijua hadi basi Ukianzisha vita Mzee enzi hizo kijana alikuwa akiangua kicheko!! Sijawahi ona mtanzania asiyeogopa Vita kama Lupogo Anapenda vita hadi basi kustaafu tu jeshini ilikuwa shida alikuwa hataki hata bila kulipwa chochote alitaka abaki tu jeshini akisema yeye anachotaka kukitokea vita aatumiwe bure hahitaji hela hata mia .Ndio serikali wakampa Kazi ya mkurugenzi Wa TACADS kupaki kuwa asubiri vita ikitokea watamtumia !!! Akakubali kwa shingo upande .Loo Mzee anapenda vita huyo sihapata kuona
 
Mwinyi Kweli anatakiwa a Edit hicho kitabbu chake

Kabla kwenda kumkabili Raisi hakuwa peke yake walienda kwenye landrover na viongozi wengine wa juu JESHINI ila kiongozi akiwa yeye KIWELU na walienda sababu ya hasira waliyokuwa nayo

Walimwita waziri wa Fedha wakati huo Profesa Kighoma Malima awaeleze sababu ya mishahara kuchelewa na maslahi duni Jeshini ,wakati huo ukusanyaji kodi ulikuwa chini mifisadi ilikuwa kibao serikali ilkuwa hela haina!!

Profesa Malima ,Profesa wa uchumi akaanza kusema ngoja niwaeleweshe kichumi tatizo liko wapi tatizo kodi ndogo!!! Kiwelu akasimama akasema wewe karani wa wizara ya fedha kamwambie bosi wako atuachie nchi atupe masaa hata matatu tu tutakusanya kodi .UMESIKIA WEWE KIKARANI CHA WIZARA YA FEDHA

Profesa Malima akakimbia anahema akamwambia Mwinyi wanataka kupindua nchi.Hawajakaa muda KIWELU AKAINGIA IKULU NA TEAM YAKE WANA MIHASIRA KIBAO WAKAONGEA wakamaliza

Walipotoka mishahara ikapanda na maslahi kuboreshwa na kila askari mwenye kuanzia nyota wakakopeshwa magari ya kutembelea pick up kwa bei nafuu na wakaanzishiwa maduka yao ya kununua vitu ambayo ni duty free hayana kodi .Magufuli ndiye alikuja kuyafunga baada ya kuona yanatumika kama uchochoro wa kukwepa kodi vitu vinaenda kwenye hayo maduka halafu vinashushwa maduka binafsi

Baada ya sakata lile Mwinyi alimuondoa uwaziri wa Fedha Profesa Kigoma Malima na kumuweka Jakaya KIkwete mwanajeshi mwenzao kuwa waziri wa fedha!!! mambo yakatulia
ubarikiwe kwa historia nzuri uliyoitoa
 
Huenda kidogo sasa Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akapumua ( na nashangaa katika Kitabu chake hajazungumzia Mkwara aliopigwa na Marehemu ) wakati alipokuwa Rais wa Tanzania 1985 hadi 1995 kwani Marehemu alikuwa ni Shupavu, Makini, Asiyeogopa kama Haki na Sheria vyote viko upande wake na mwenye Kujiamini kama ilivyo Sifa Mama ya Mwanamedani ( Mwanajeshi ) yoyote yule duniani.

Ni kwamba Kipindi hicho cha Awamu ya Pili ( ya Rais Mwinyi ) Mishahara kwa Wanajeshi ilikuwa inachelewa sana Kulipwa hadi kupelekea Wanajeshi kuanza ' Kujisevia ' Bidhaa Madukani kwa Ubabe na wengine hata Kujiingiza katika Uratibu wa Uhalifu ili tu waweze Kujikimu.

Hali ilipozidi kuwa mbaya ( na hapa naiongelea 1985 hadi 1995 ) Marehemu huyu Afande Kiwelu alienda moja kwa moja kuonana na Rais Mwinyi ambapo alimweleza kuwa anampa Masaa machache tu awe ameshawalipa Mishahara yao Wanajeshi vinginevyo ' wanamtimbia ' mazima mazima pale Ikulu hali iliyomfanya Rais Mwinyi ' aufyate ' na Kuwatafutia Mishahara yao alikokujua na kuwapa mara moja ambapo Heshima ya Marehemu ndani ya Jeshi ( JWTZ ) iliongezeka maradufu na kuwa Mmoja wa Makamanda waliopendwa zaidi na Wanajeshi Kipindi chake cha Utendaji.

Na ni Juhudi hizi hizi za Marehemu Afande Kiwelu ndiyo zilisababisha tokea Siku hiyo Awamu zote za Marais mpaka sasa ( leo ) watacheza na Mishahara ya Kada zingine zote kwa Kuwacheleweshea ila siyo kwa Wanajeshi ( JWTZ ) na nahisi Rais Mstaafu Mzee Mwinyi alihakikisha kila Rais anayechukuwa nchi basi anapewa Angalizo hilo ndiyo maana tokea Awamu yake hadi sasa sijasikia Upuuzi huo ukijitokeza tena.

Mwambieni Rais Mstaafu Mzee Mwinyi akifanyie ' editing ' Kitabu chake alichokizindua hivi karibuni na aliweke hili Tukio kwani lina Umuhimu sana kwa Watu kujua na wale ambao Kipindi hicho mlikuwa bado katika Zipu za Baba zenu na wale walioko pia Zipuni kwa sasa ili wakizaliwa wakutane nayo.

Kwani ni Jambo ( Tukio ) ambalo lilitokea ( lilimtokea ) Mzee wa Watu achilia mbali na lile la ' Kuwambwa ' Kwake Makofi akiwahutubia Waislamu alipowagusia Kutumia Condoms pale Wakitiana ( Wakitinduana ) ili Kujiepusha na Maambukizi ya UKIMWI ambao miaka hiyo ulikuwa umepamba sana Moto na ' Unawafyeka ' mno Watanzania.
Ni kipi kutoka kwa marehemu kilikua kinafanya mpaka mwinyi asipumue
 
Wakati huo tukiongelea TPDF General walioiiva kikazi...
Unaanza na General Musuguri, then General Mwita Kiaro , anafuata General Twalipo,
bila kumsahau General "Black Mamba" John Butler Walden, na Genaral Kiwelu ndani
Hawa walipanda through the ranks sio kupatiwa uchele na Raisi mshikaji wako.........

Katika list hiyo umemsahau retired General Mwakalindile!!
 
..Ukumbuke alitolewa ngome / makao makuu akiwa chief of staff na kupelekwa mstari wa mbele kuandaa majeshi na kuongoza operation chakaza.

..baada ya Tz kupata ushindi ktk operation chakaza ndipo Kiwelu aliporudi ngome na kuendelea na majukumu yake ya u-chief of staff.

..wakati Kiwelu akiongoza operation chakaza martin mwakalindile ndiye aliyekaimu nafasi ya chief of staff. Baadae Mwakalindile alitumikia kama mkuu wa mafunzo / chief instructor wakati wa vita vya kagera.

NB.

..yuko mchangiaji mmoja hapa JF alikuwa akibisha kwamba Gen.Kiwelu ndiye aliyeongoza mapigano ya kumtoa Nduli ktk ardhi ya Tz. Nimefarijika kwamba Jwtz wametoa taarifa ambayo haitatoa nafasi kwa wapotoshaji wa historia ya vita vya Kagera.

JF imejaa kina sisi wala isikusumbue...ni General Kiwelu ndio aliyopanga na kuendesha yale mapigano ya kumtoa Idd Amin ndani ya Tanzania. Chini ya usimamizi wake, makomandoo wa Tanzania walivuka mto, wakaweka ulinzi ili daraja la muda lijengwe na vifaa kuweza kupita. Kuna General Mmoja anaitwa Kabunda, pengine sasa amestaafu, ndio aliongoza makomandoo hao katika kuwezesha daraja kujengwa.
Hili Jeshi la Wananchi ni jeshi kweli kweli. Toka waasi mwaka 1964 wale waliokuwa KAR, limejengwa kama moja ya majeshi madhubutu, yenye nidhamu na uthubutu mkubwa.
Inapendeza kuona mpaka leo JWTZ bado ni jeshi lililo vile vile
 
RIP Kamanda.
Kwa MKurugenzi wa Habari an Mahusiano wa JWTZ asante sana kwa taarifa na uandishi uliosimama:
Sahihisho: Ukiamua kutujulisha familia ya marehemu huwezi kuandika nusu kuwa ameacha Mke na Watoto. Utaulizwa Watoto wangapi; Majina ya Mke na hao Watoto n.k
 
Uko sahihi Lupogo alikuwa namba mbaya kwenye MK yaani Medani ya kivita ni anzijua hadi basi Ukianzisha vita Mzee enzi hizo kijana alikuwa akiangua kicheko!! Sijawahi ona mtanzania asiyeogopa Vita kama Lupogo Anapenda vita hadi basi kustaafu tu jeshini ilikuwa shida alikuwa hataki hata bila kulipwa chochote alitaka abaki tu jeshini akisema yeye anachotaka kukitokea vita aatumiwe bure hahitaji hela hata mia .Ndio serikali wakampa Kazi ya mkurugenzi Wa TACADS kupaki kuwa asubiri vita ikitokea watamtumia !!! Akakubali kwa shingo upande .Loo Mzee anapenda vita huyo sihapata kuona
Marehemu Lupogo is not in good books of the then good Generals.
Ukifuatilia historia ya vita vya Kagera Lupogo alishindwa kuongoza vikosi kukabiri adui maeneo ya Sembabule na kupoteza wapiganaji wengi kwenye uwanja wa mapambano.
Aliondolewa kwenye uwanja wa mapambano na nafasi yake akapewa Brigadier Muhidin Kimario akiwa mkuu wa mkoa Mwanza wakati huo.
Brigadier aliwapanga wapiganaji wake na kuwajegea morali wakasonga mbele na kuwasambaratisha majeshi ya adui.

Someni kinaitwa ;War in Uganda and legacy of IDD Amin msitake kupotosha ukweli.
 
..unadhani tatizo lilikuwa kamanda wa vita, au askari aliokuwa nao hawakuwa tayari kwa mashambulizi waliyokutana nayo uwanja wa vita? huoni kwamba ana mchango wa kuleta ushindi toka Kagera mpaka Sembabule?
 
Kijijini kwake Mamba Kokirie ni eneo dogo sana naona aliamua azikwe karibu na Miradi na mashamba yake kwani alishika maeneo makubwa na kuwekeza eneo kubwa kuliko hicho kijiji alichozaliwa, nasikia huko Bukoba na Morogoro ni maeneo makubwa, sasa akilinganisha na kupelekwa huko Kijijini mazishi hapangetosha
naona jibu zuri analo YEHODAYA
Siyo kweli mkuu napafahamu vizuri sn na siyo kwamba eti kumejaa makaburi hizo ni hear say
 
..Kuna jambo wengi tumelisahau kuhusu Gen.Tumainieli Kiwelu.

..alipotoka jeshini aliteuliwa kuwa Balozi wetu Ufaransa.

..baadae uteuzi huo ukabadilishwa na akateuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Inawezekana host country ili mkata au yeye mwenyewe aliona hivyo.
Enzi zile wakati mwingine wakita kukutenganisha na strong area zako wanakupeleka Ubalozini ili uwe mpweke na mnywaji pombe tu au wanawake
 
JF imejaa kina sisi wala isikusumbue...ni General Kiwelu ndio aliyopanga na kuendesha yale mapigano ya kumtoa Idd Amin ndani ya Tanzania. Chini ya usimamizi wake, makomandoo wa Tanzania walivuka mto, wakaweka ulinzi ili daraja la muda lijengwe na vifaa kuweza kupita. Kuna General Mmoja anaitwa Kabunda, pengine sasa amestaafu, ndio aliongoza makomandoo hao katika kuwezesha daraja kujengwa.
Hili Jeshi la Wananchi ni jeshi kweli kweli. Toka waasi mwaka 1964 wale waliokuwa KAR, limejengwa kama moja ya majeshi madhubutu, yenye nidhamu na uthubutu mkubwa.
Inapendeza kuona mpaka leo JWTZ bado ni jeshi lililo vile vile
Naona kuna jadi ya kusifia marehemu inaendelezwa kupita kiasi.

Ninakubali ndiyo kuwa huyu Marehemu Kiwelu(Gen rtd) alikuwa ndiyo kamanda muasisi wa vita vya Kagera (ops chakaza).

Lakini je nisababu gani iliyomfanya mwalimu Nyerere kumuondoa haraka sana chini ya moto wa adui mwanzo wa vita mwaka 78?

Yeye pamoja na marehemu Yusufu Himid (brig gen rtd) waliondolewa mwanzo kabisa wa vita, tena kwa sababu maalumu zinazofahamika na kila askari aliyekuwepo vitani wakati ule.

Embu uliza afisa ama askari yeyote aliyeshiriki dhahiri mwanzo wa vita hiyo pia askari waliokuwepo jeshini miaka ya 70-90 wanaomfahamu vizuri marehemu, ukipata wasifu wake wa kweli hautakuja kurudia kumpamba na kumpa sifa za kisiasa.
 
Siyo kweli mkuu napafahamu vizuri sn na siyo kwamba eti kumejaa makaburi hizo ni hear say
Siajasema Mamba Kokirie pamejaa makaburi, ila nimesema eneo la Kiwelu hapo Mamba Kokirie hapatoshi kuubeba mzigo huo, na nilisema toka awali atazikwa shambani kwake Mbezi Luis kwani hilp eneo ni lake kanunua kwa wazaramo na ni kubwa kuliko huko Kokirie km angeenda
Generali Kiwelu amemzika mke wake mkubwa, hapo na upande mwingine alimzika Mkwe (mke wa mtoto wake huyu binti alikuwa Mwanajeshi kabila mmasai hapohapo Mbezi Luis) Kwa hiyo ni mahali patakapodumu kwa familia na ukoo wake
 
Sawa mkuu nimekuelewa
 
Naona kuna jadi ya kusifia marehemu inaendelezwa kupita kiasi.

Ninakubali ndiyo kuwa huyu Marehemu Kiwelu(Gen rtd) alikuwa ndiyo kamanda muasisi wa vita vya Kagera (ops chakaza).

Lakini je nisababu gani iliyomfanya mwalimu Nyerere kumuondoa haraka sana chini ya moto wa adui mwanzo wa vita mwaka 78?

Yeye pamoja na marehemu Yusufu Himid (brig gen rtd) waliondolewa mwanzo kabisa wa vita, tena kwa sababu maalumu zinazofahamika na kila askari aliyekuwepo vitani wakati ule.

Embu uliza afisa ama askari yeyote aliyeshiriki dhahiri mwanzo wa vita hiyo pia askari waliokuwepo jeshini miaka ya 70-90 wanaomfahamu vizuri marehemu, ukipata wasifu wake wa kweli hautakuja kurudia kumpamba na kumpa sifa za kisiasa.
Yusuph Himid si ndio alikuwepo wakati Kagera inatwaliwa? Siwezi kumuongelea sana huyu bwana. General Kiwelu alikuwa mkorofi sana. Inasemekana aligoma kabisa kuelezea mipango ya kivita kwa Marehemu Sokoine. Alikuwa na communication problem ambayo sio kitu kizuri kwa operations kubwa kama zile. It could insurbodination of some kind in other places.
Pamoja na hayo, yeye ndio alianza kazi ya kumtoa nduli. Hilo hata kama watu hawakumpenda, lilikuwa la kwake. Yeye ndio alisimamia ujenzi wa daraja la muda baada ya kuvuka mto. Ingawa alirudi makao makuu ya jeshi baada tu ya zoezi lile
 
Back
Top Bottom