Huenda kidogo sasa Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akapumua ( na nashangaa katika Kitabu chake hajazungumzia Mkwara aliopigwa na Marehemu ) wakati alipokuwa Rais wa Tanzania 1985 hadi 1995 kwani Marehemu alikuwa ni Shupavu, Makini, Asiyeogopa kama Haki na Sheria vyote viko upande wake na mwenye Kujiamini kama ilivyo Sifa Mama ya Mwanamedani ( Mwanajeshi ) yoyote yule duniani.
Ni kwamba Kipindi hicho cha Awamu ya Pili ( ya Rais Mwinyi ) Mishahara kwa Wanajeshi ilikuwa inachelewa sana Kulipwa hadi kupelekea Wanajeshi kuanza ' Kujisevia ' Bidhaa Madukani kwa Ubabe na wengine hata Kujiingiza katika Uratibu wa Uhalifu ili tu waweze Kujikimu.
Hali ilipozidi kuwa mbaya ( na hapa naiongelea 1985 hadi 1995 ) Marehemu huyu Afande Kiwelu alienda moja kwa moja kuonana na Rais Mwinyi ambapo alimweleza kuwa anampa Masaa machache tu awe ameshawalipa Mishahara yao Wanajeshi vinginevyo ' wanamtimbia ' mazima mazima pale Ikulu hali iliyomfanya Rais Mwinyi ' aufyate ' na Kuwatafutia Mishahara yao alikokujua na kuwapa mara moja ambapo Heshima ya Marehemu ndani ya Jeshi ( JWTZ ) iliongezeka maradufu na kuwa Mmoja wa Makamanda waliopendwa zaidi na Wanajeshi Kipindi chake cha Utendaji.
Na ni Juhudi hizi hizi za Marehemu Afande Kiwelu ndiyo zilisababisha tokea Siku hiyo Awamu zote za Marais mpaka sasa ( leo ) watacheza na Mishahara ya Kada zingine zote kwa Kuwacheleweshea ila siyo kwa Wanajeshi ( JWTZ ) na nahisi Rais Mstaafu Mzee Mwinyi alihakikisha kila Rais anayechukuwa nchi basi anapewa Angalizo hilo ndiyo maana tokea Awamu yake hadi sasa sijasikia Upuuzi huo ukijitokeza tena.
Mwambieni Rais Mstaafu Mzee Mwinyi akifanyie ' editing ' Kitabu chake alichokizindua hivi karibuni na aliweke hili Tukio kwani lina Umuhimu sana kwa Watu kujua na wale ambao Kipindi hicho mlikuwa bado katika Zipu za Baba zenu na wale walioko pia Zipuni kwa sasa ili wakizaliwa wakutane nayo.
Kwani ni Jambo ( Tukio ) ambalo lilitokea ( lilimtokea ) Mzee wa Watu achilia mbali na lile la ' Kuwambwa ' Kwake Makofi akiwahutubia Waislamu alipowagusia Kutumia Condoms pale Wakitiana ( Wakitinduana ) ili Kujiepusha na Maambukizi ya UKIMWI ambao miaka hiyo ulikuwa umepamba sana Moto na ' Unawafyeka ' mno Watanzania.