TANZIA Jenerali Tumainiel Kiwelu afariki Dunia, kuzikwa Mbezi Loius Dar

TANZIA Jenerali Tumainiel Kiwelu afariki Dunia, kuzikwa Mbezi Loius Dar

Sasa naelewa kwa nini alikuja kuondolewa jeshini wakaona heri wampe vyeo vya kisiasa ili ajifunze nidhamu ya kiraia pia.

Rais ni Jemedari Mkuu unapaswa kumtii hata alipokuwa anadai mishahara alipaswa kutumia busara kama sio nidhamu ya juu ya kijeshi sio kumtishia Rais.

Hii kwa watu waliowahi kupitia majeshi watakubaliana kwamba ilibidi kumtoa pale maana siku nyingine atakuwa na madai mengine atakosa nidhamu kwa kiongozi then ikageuka ugaini, tena ana bahati Mwinyi alikuwa mtu poa Yani angekuwa Nyerere angemtandika kesi ya uhaini . Rais hatishiwi hata kama unahisi unaweza kufanya hayo.

Naelewa ndio maana walimpandisha vyeo baada ya kustaafu kigoma alikokuwa Major General then mpaka full four star General amebaki na sarakikya nae alipigwa Pini sababu hizi hizi.

Huwezi kuwa kiongozi halafu unaendeshwa na askari wa chini kiasi unamkosea heshima mkuu wa nchi.

By the way alikuwa shupavu sana rip to the best General who never became a general 🤷
Kuna nyingine ya Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ( Poti wangu kabisa kutoka Mkoani Mara ) Jenerali George Mwita Waitara ila kwa leo naomba nisitiririke wala kuserereka nayo Kwanza.
 
Huyu Tumainieli kiwelu ndie aliyekua mkuu wa mkoa wa Iringa aliyemuua Mwamwindi?
Kha, mkuu umepuyanga Sana. Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Iringa aliuawa na siyo alimuua Mwamwindi. Mwamwindi alipomuua mkuu wa mkoa Dr. Kleruu alishtakiwa na kupatikana na hatia a kahukumiwa kifo na akanyongwa.Hivyo wahusika wa tukio hilo wote walishakuwa Kama mwendazake toka miaka hiyo ya 70.
 
Nimekuwa naona majina mengi ya uchagani na upareni yana eithaer anzia na el au kumalizikia na el je eli katika majina hayo humaanisha nini
Tumainiel
Eliatosha
Sifael
Happiel
Elbariki
Eliona
Elikunda
Baniel
 
Nimekuwa naona majina mengi ya uchagani na upareni yana eithaer anzia na el au kumalizikia na el je eli katika majina hayo humaanisha nini
Tumainiel
Eliatosha
Sifael
Happiel
Elbariki
Eliona
Elikunda
Baniel
Eli = mungu wa kimila
 
RIP Jenerali Kiwelu, utumishi wako ulikuwa uliotukuka. Umepigana vita iliyo njema, imani umeilinda.
 
Pumzika kwa amani kamanda, wewe na Luteni Generali Silas Mayunga (Mti Mkavu) mnakukukwa sana na watanzania hasa hasa kwenye ile vita ya Kagera ya kumtokomeza / Kumchakaza nduli Iddi Amini dada. Vikosi vyenu mlivyokuwa mkiviongoza vilifanya maajabu makubwa!!
 
Huenda kidogo sasa Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akapumua ( na nashangaa katika Kitabu chake hajazungumzia Mkwara aliopigwa na Marehemu ) wakati alipokuwa Rais wa Tanzania 1985 hadi 1995 kwani Marehemu alikuwa ni Shupavu, Makini, Asiyeogopa kama Haki na Sheria vyote viko upande wake na mwenye Kujiamini kama ilivyo Sifa Mama ya Mwanamedani ( Mwanajeshi ) yoyote yule duniani.

Ni kwamba Kipindi hicho cha Awamu ya Pili ( ya Rais Mwinyi ) Mishahara kwa Wanajeshi ilikuwa inachelewa sana Kulipwa hadi kupelekea Wanajeshi kuanza ' Kujisevia ' Bidhaa Madukani kwa Ubabe na wengine hata Kujiingiza katika Uratibu wa Uhalifu ili tu waweze Kujikimu.

Hali ilipozidi kuwa mbaya ( na hapa naiongelea 1985 hadi 1995 ) Marehemu huyu Afande Kiwelu alienda moja kwa moja kuonana na Rais Mwinyi ambapo alimweleza kuwa anampa Masaa machache tu awe ameshawalipa Mishahara yao Wanajeshi vinginevyo ' wanamtimbia ' mazima mazima pale Ikulu hali iliyomfanya Rais Mwinyi ' aufyate ' na Kuwatafutia Mishahara yao alikokujua na kuwapa mara moja ambapo Heshima ya Marehemu ndani ya Jeshi ( JWTZ ) iliongezeka maradufu na kuwa Mmoja wa Makamanda waliopendwa zaidi na Wanajeshi Kipindi chake cha Utendaji.

Na ni Juhudi hizi hizi za Marehemu Afande Kiwelu ndiyo zilisababisha tokea Siku hiyo Awamu zote za Marais mpaka sasa ( leo ) watacheza na Mishahara ya Kada zingine zote kwa Kuwacheleweshea ila siyo kwa Wanajeshi ( JWTZ ) na nahisi Rais Mstaafu Mzee Mwinyi alihakikisha kila Rais anayechukuwa nchi basi anapewa Angalizo hilo ndiyo maana tokea Awamu yake hadi sasa sijasikia Upuuzi huo ukijitokeza tena.

Mwambieni Rais Mstaafu Mzee Mwinyi akifanyie ' editing ' Kitabu chake alichokizindua hivi karibuni na aliweke hili Tukio kwani lina Umuhimu sana kwa Watu kujua na wale ambao Kipindi hicho mlikuwa bado katika Zipu za Baba zenu na wale walioko pia Zipuni kwa sasa ili wakizaliwa wakutane nayo.

Kwani ni Jambo ( Tukio ) ambalo lilitokea ( lilimtokea ) Mzee wa Watu achilia mbali na lile la ' Kuwambwa ' Kwake Makofi akiwahutubia Waislamu alipowagusia Kutumia Condoms pale Wakitiana ( Wakitinduana ) ili Kujiepusha na Maambukizi ya UKIMWI ambao miaka hiyo ulikuwa umepamba sana Moto na ' Unawafyeka ' mno Watanzania.
Mwinyi Kweli anatakiwa a Edit hicho kitabbu chake

Kabla kwenda kumkabili Raisi hakuwa peke yake walienda kwenye landrover na viongozi wengine wa juu JESHINI ila kiongozi akiwa yeye KIWELU na walienda sababu ya hasira waliyokuwa nayo

Walimwita waziri wa Fedha wakati huo Profesa Kighoma Malima awaeleze sababu ya mishahara kuchelewa na maslahi duni Jeshini ,wakati huo ukusanyaji kodi ulikuwa chini mifisadi ilikuwa kibao serikali ilkuwa hela haina!!

Profesa Malima ,Profesa wa uchumi akaanza kusema ngoja niwaeleweshe kichumi tatizo liko wapi tatizo kodi ndogo!!! Kiwelu akasimama akasema wewe karani wa wizara ya fedha kamwambie bosi wako atuachie nchi atupe masaa hata matatu tu tutakusanya kodi .UMESIKIA WEWE KIKARANI CHA WIZARA YA FEDHA

Profesa Malima akakimbia anahema akamwambia Mwinyi wanataka kupindua nchi.Hawajakaa muda KIWELU AKAINGIA IKULU NA TEAM YAKE WANA MIHASIRA KIBAO WAKAONGEA wakamaliza

Walipotoka mishahara ikapanda na maslahi kuboreshwa na kila askari mwenye kuanzia nyota wakakopeshwa magari ya kutembelea pick up kwa bei nafuu na wakaanzishiwa maduka yao ya kununua vitu ambayo ni duty free hayana kodi .Magufuli ndiye alikuja kuyafunga baada ya kuona yanatumika kama uchochoro wa kukwepa kodi vitu vinaenda kwenye hayo maduka halafu vinashushwa maduka binafsi

Baada ya sakata lile Mwinyi alimuondoa uwaziri wa Fedha Profesa Kigoma Malima na kumuweka Jakaya KIkwete mwanajeshi mwenzao kuwa waziri wa fedha!!! mambo yakatulia
 
Juma Nkangaa ndie juma ikangaa au?
Acha ubwege wewe, mwenyewe katika maandishi yako umetofautisha halafu unauliza swali? nakusalimu kwa jina la jamuhuri ya muungano wa Tanzania, itikiaaaaa.
 
Huyu mzee kwanini wanamzika Dar? kwa nini asipelekwe kwao Moshi? Maana serikali inaweza kugharimia.

Anyway, maybe ni wish yake azikwe Dar. But I find it strange.

Nafsi yake ipumzike alipoandaliwa na mola wake.
 
Tangu shujaa asepe naona hata taarifa zinatolewa na jeshi zinakua zimekamilika/ziko kisomi.

Tunaona mabadiliko kila sehemu.
shujaa gani ujinga wa kujaana utukufu wsiokuwa nao. Alwaya dictators are like that, angalia Idd Amin kama kichaa

1621593983851.png


1621593668132.png


1621593740373.png
 
Jenerali Tumainiel Kiwelu amefariki tarehe 18 Mei 2021 na atazikwa shambani kwake Mbezi Luis Dar es salaam tarehe 22 May 2021

Bwana ametoa Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.

Pia soma
- Historia ya Jenerali Tumainiel Kiwelu


Jenerali Tumainiel Kiwelu amefariki tarehe 18 Mei 2021 na atazikwa shambani kwake Mbezi Luis Dar es salaam tarehe 22 May 2021

Bwana ametoa Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.

Pia soma
- Historia ya Jenerali Tumainiel Kiwelu

Pole sana Ndugu,jamaa na marafiki pamoja na jeshi la wananchi kwa kupoteza mtu mashuhuri nchini.
 
Huyu Tumainieli Kiwelu ndie aliyekua mkuu wa mkoa wa Iringa aliyemuua Mwamwindi?
Soma hapa
 
Back
Top Bottom