Inashangaza sana kwamba kuna baadhi yetu hatuamini ayasemayo Jenerali. Lakini penye ukweli uongo hujitenga. Ayasemayo Jenerali ni kuntu tupu.
Nachoshangaa Tanzania ya leo, badala ya kukaa kuwaza nini tunahitaji kwa nchi hii iendelee, tumekalia kulalamika ati alikuwa mazuzu. Hivi kama ulikubali kuwa zuzu unamlalamikia nani?
Rais alopita alikuwa na yake kaondoka, hata tukae tumseme mara mia haitobadili kitu. Na cha ajabu kesha tangulia mbele ya haki. Kwanini kama nchi tusijikite katika kuangalia ya sasa na yajayo. Kuliko kila siku vikao na hotuba zisizo na tija kwa nchi yetu.
Kuna nchi nyingi Ulaya ziliongozwa na madikiteta na walikuwa na mabaya hata zaidi ya rais alopita. Lakini uwa sisikii wakipoteza muda kukaa na kulaumu na kumsema au kuwasema vibaya hao madikteta. Ulaya wanaangalia kuendeleza nchi zao na si kukalia umbea.
Mrusi anakombora la supersonic, Mmarekani, Mwingereza na Australia wameungana kubuni ugunduzi utakao saidia namna ya kujikinga na makobora ya supersonic.
Akili ya mtanzania inawaza kumsuta na kumsema vibaya marehemu ambaye hawezi wajibu. Tunajioona kuwa sisi ndo sisi. Huyu Ulimwengu amekuwa kiongozi wa nchi hii, hivi nini alianyia nchi hii ambacho tunaweza tukakikumbuka? Au yeye ni kukosoa kila siku, na cha maana hatukioni toka kwake. Nasi tunakaa kumshangilia. Na kuonesha ameishiwa kila siku hutumia maneno yale yale.
Watanzania tubadilike, tuwaze namna ya kuendeleza nchi yetu. uangalie ni maeneo yapi tunahitaji kuyapa nguvu na kukuza uchumi. Tuwekeze kwenye elimu ya kisasa.
Mzee Ulimwengu amekuwa ktk siasa muda mwingi huko nyuma. Allizunguka ulimwengu. Uwa nikiangalia Tanzania hatuna scholarship maalum kwa nchi za nje. Ukiachana na zile zinazojumuisha nchi zinazoendelea, au Jumuia ya Madola.
Zaidi tulionayo pekee inayopokea watanzania wasiozidi wawili ni ya Mwl Nyerere Scholarship ktk chuo alichosoma huko Uingereza. Ukilinganisha na mataia kama Nigeria, Uganda, Ethiopia, Rwanda na hata Burundi ambazo zinakuwa na scholarship huko nje kwa wingi.
Hivi balozi zetu wanaanya nini? Wanashindwa kushawishi vyuo vya nje au serikali za huko kuwa na scholarship maalum kwa ajili ya watanzania? Tunahitaji watanzania wengi waende nje wasome na kuwa na teknolojia, warudi kuitumikia nchi. Rwanda wameanya hivyo. Ethiopia, Nigeria na hata Ghana.
Nilikuwa chuo huko nje, viongozi kutoka Ethiopia wamekuwa na ziara kadhaa ktk hicho chuo kujenga mahusiano, na kinapokea waethiopia wengi wakipata scholarship. Niliwahi kuona baadhi ya viongozi wa kitanzania ktk dini wakitembelea lakini sikuwasikia wakiongea chochote kile zaidi ya kuonesha ukubwa wao na kusemana. Kuna kiongozi mmoja ilibidi tuwe na mabishano ya muda kisa anamsema kiongozi mwenzie ili wazungu wamuone mbaya. Na alikuwa wanapanga kumwondoa. Hii ndo akili zetu watanzania hata tunapozuru nje hatuachi asili ya kusemana.
China ni tajiri na wanatechnolojia kubwa lkn bado wanapeleka vijana wao wengi nje kwenda kusoma, Korea kusini, India na nyinginezo. Tanzania tunahitaji mabadiliko. Nakumbuka nilipoingia kuanza kazi za serikali huko nyuma, wapambe walianza kunieleza mabaya ya yule alopita ktk hiyo ngazi niliokuwepo. Nilichoona ni vema iwe msimamo wangu sikunyanyua mdomo kumsema au kuuliza juu ya mtangulizi wangu. Nililenga nini kinatakiwa kutekelezwa katika majukumu yangu na si kumuongelea mtu. Hii iliondoa tabia zao za umbea, na hawakuendelea kumsema huyo mtangulizi. Nilibaki kumheshimu na hata kuna muda tuliongea kwa uzuri tu kwenye simu.
Watanzania tuache majungu tujikite ktk kuleta mabadiliko ya kimaendeleo. tuache kujipendekeza, wakati mwingine tunatumia hela nyingi kusherehesha mambo yasiyo na maana badala ya kujikita kuleta maendeleo kwa wananchi. Serikali ipo kuwatumikia wananchi na si wananchi kuitumikia serikali. Serikali ipo kutatua kero za wananchi na si viongozi kujiona wao ni wamaana sana kuliko wananchi.
Wananchi leo akili zetu zimeishia katika katiba, hivi kuna nchi ngapi duniani zingine hazina katiba lakini wanamaendeleo makubwa. Tazama nchi za Umoja wa nchi za Kiarabu. Uingereza isiyo na katiba ya kuandikwa. unahitaji viongozi wanao iwazia Tanzania mioyoni mwao. Viongozi ambao wapo kuhakikisha Tanzania inapiga hatua ya kimaendeleo kuliko tubaki kama tulivyo kila iitwapo leo.
Kuna research nyingi huko vyuoni, lkn zinaachwa tu kuchakaa na baadae kuchomwa moto huko vyuoni. Wasomi wamegeuka machawa wa wanasiasa.
Kwa nini nchi yetu tusiwe na chombo ambacho kinachunguza hizi research na zile bora wahusika watambulike na research zao zitumike kuleta mabadiliko ktk nyanja mbalimbali. Nchi moja nayoijua huko Ulaya utumia vigezo hivi na wanapopata research muhimu hata sheria ubadilishwa ili kukidhi haja. Hii inatia moyo vijana wetu, na pia kuendesha nchi kisayansi na si kichawa.
Namalizia hata tukimsema JPM mara mia, haitotusaidia kitu. Na tunapoteza muda wetu bure wakati yeye kapumzika, na uenda anatuangalia na kusikitika na hasa kucheka kama alivyozoea. Chuki uwa haina lolote la maana juu ya mwanadamu. Bali upendo hata kwa wale wanaokuchukia. Hii uleta kuishi maisha ya amani zaidi.