Kama una mazuri yake umekatazwa kuyasema? Anzisha uzi wa mazuri ya mungu-mtu wako. Usifunge watu midomo waliopitia mabaya ya yule dikteta kuyasema. Hili ni jukwaa huru. Wee ni nani mpaka ufunge watu midomo? Hata Muumbaji wetu ametupa uhuru wa kuchagua kati yake na shetani.
Mzee Mwinyi alisema maisha ni hadithi. Jiandikie hadithi yako nzuri wakati ukiwa hai. Kama ulikuwa mtu wa kutukana, kuua, mwenye hasira, mwonevu, mvunja katiba, mwongo... km huyo kipenzi chako ndio hadithi yako hiyo uliyojiandikia. Haiwezi kubadilika baada ya kuzikwa.
Unataka umlazimishe Lissu aliyepigwa risasi kwa amri ya yule jambazi amsifu? Hautafanikiwa. Kama una sifa zake nzuri, anzisha uzi. Watu tuliathirika na udikteta wake hatutaacha kusema. Kama kujinyonga, jinyonge.
Eti sina exposure! Jifariji tu. Ujerumani nimesoma (MSc Heidelberg) na Kijerumani naongea, angalau cha kuombea maji. Hakuna watu wanamsifia Hitler Ujerumani ya leo. Kuna kundi dogo sana la watu wanaitwa neo-nazis ndio wanakubali sera zake. Ni dogo kama mlivyo Sukuma gang kwa sasa hapa Tanzania.
Yaani unataka nimsome kwenye kitabu dikteta ambaye nimeishi maisha yake nikiwa mtu mzima? Sihitaji kusoma vifo vya akina Mawazo, Azory na wengineo kwenye vitabu. Sihitaji kusoma kuenguliwa kwa wagombea kwenye chaguzi eti kwenye vitabu ama kura za kwenye mabegi za 2020 kwenye vitabu. Ni mambo niliyoshuhudia.
Nadhani umepata elimu ya kutosha bure.
Akili zisizo angalia kwa mapana. Umesoma vitabu, ulishawahi kwenda Ujerumani ukakuta majungu ya Hitler kama hapa? JPM hajaandikiwa kitabu. Andikeni kitabu ijulikane wazi. Na inaonesha huna exposure, kwa taaria yako Hitler na watu wanatukuza itikadi yake hadi leo, nenda Ulaya hata Marekani.
Usioanishe historia za Carl Peters na majungu. Nadhani huna uelewa mzuri kujua nini nimeongelea. Na katika waandishi wazuri wanapoandika kitabu uangalia pande mbili. Za mazuri aloanya mtu na mabaya. Si kumtangaza mtu kwa mabaya tu!
Hilo neno sukuma gang kwangu naona kawaida hata ukiita mara kumi sibabaiki, kwa sababu akili upi uwaza mashambulizi na si uchambuzi wa kina.
Na inaonesha ujaelewa kabisa nilichokiongelea unarukia rukia tu. Sikulaumu ila uelewa wako ndo ulipoishia.