Jenerali Ulimwengu: Sioni ajabu mapinduzi ya kijeshi Guinea. Yatafika haraka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara

Jenerali Ulimwengu: Sioni ajabu mapinduzi ya kijeshi Guinea. Yatafika haraka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara

bne

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2016
Posts
1,679
Reaction score
2,016
Akihojiwa na kipindi cha BBC kinachorushwa na television ya star TV tarehe 7 mwezi huu kuhusu mapinduzi ya Guinea, Jenerali Ulimwengu amesema yeye haoni ajabu Kwa yale yaliyotokea Guinea.

Na akatabiri pia kuwa hali hiyo ya kimapinduzi ya kijeshi itafika Kwa Kwa haraka sana ktk nchi zote zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Alipoulizwa kwanini anawaza hivyo alisema kuwa kilichokuwa kinafanywa na Alpha Conde ya ukandamizaji, dhurumati, kutokujali demokrasia, na uvunjifu wa haki za binadamu ,vitendo hivyo viovu vinafanywa pia na baadhi ya Serikali zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara na nchi zetu za Afrika Mashariki.

Jenerali aliendelea kushangaa kuona AU na ECOWAS wakilaani mapinduzi hayo huku wakiwa walishindwa kukemea matendo mabaya ya Rais Conde.

Alisema hali hiyo ya kimapinduzi ya kijeshi hayana muda mrefu itafika ktk nchi zetu wakati wowote kuanzia sasa.

Jenerali Ulimwengu ambae kwasasa ni mtu mzima na mwenye busara ni mtu asiyependa unafiki na hupenda kusema ukweli na maneno yake mara nyingi hutimia kama anavyotabiri.
 
Anachoongea Jenerali ni sahihi kwa mujibu wa historical calculations wala sio utabiri.

Hauhitaji akili kubwa kuona yajayo East Africa ni km ya Guinea ndio maana Museveni alilaani sana hayo mapinduzi akijua yeye ni next.

A.U. nayo inatakiwa kuondolewa kimapinduzi tu haina maana tena,inalinda maslahi ya madikteta.
 
Mapinduzi ni mambo ya kizamani!
Siyo zamani hata hapa kwetu nikiwa primary miaka ile ya 90's nakumbuka Marandu alifanya mapinduzi pale NCCR hadi Mrema akajificha chini ya meza. Huku jasusi Maswi akijidai ni mfuasi mtiifu wa Mrema.

Umesahau haya mapinduzi Mwagito na yametokea kwenye kizazi hiki hiki cha kina Mbowe?
 
Natamani kuona hayo yakitokea na huku kwetu

Msukosuko wake hautakua mdogo, unaweza kuichafua nchi isitawalike tena na kuvuruga mipango yote. Kila mmoja wetu ataathirika kwa namna moja ama nyingine.

Ikitokea, ipangwe na kuratibiwa vizuri utekelezaji wake, vinginevyo ni shida tupu.
 
Mzee aache kututisha, wao wamekula maisha kukiwa hamna vita kipindi chao sasa iweje leo atutabirie dhiki?
 
Back
Top Bottom