Jenerali Ulimwengu: Sioni ajabu mapinduzi ya kijeshi Guinea. Yatafika haraka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara

Jenerali Ulimwengu: Sioni ajabu mapinduzi ya kijeshi Guinea. Yatafika haraka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara

Kama ni utabiri wa kweli basi Waafrika tumeshindwa kujitawala. Tulipiga kelele wakoloni watuache tujitawale wenyewe lakini baada ya miaka zaidi ya 60 tunawaza mambo ya mapinduzi ya kijeshi. Junta au utawala wa kijeshi siyo jibu la matatizo yetu. Ni dalili ya kuwa demokrasia imetushinda na tumeshindwa kujitawala. Tungewaacha tuu wakoloni watawale mpaka tujifunze kwao jinsi ya kujitawala. Nchi kama South Africa ilichelewa kupata uhuru lakini iliwasaidia watu wake wajifunze jinsi ya kujitawala na kuendesha nchi. Sisi wengine tulikuwa na kiherere tukawafukuza mapema.

#FailedStates
 
Yahya Jammeh hakupinduliwa alipoteza uchaguzi kwa Adams Barrow akakatalia madarakani Ecowas wakatishia kumtoa akakimbia mwenyewe.
Hana tofauti na waliong'angania madarakani wakatolewa kwa mkuku
 
Kosa alilofanya Alpha Conde ni kugusa maslahi ya wanajeshi hapo ndio shida ilipoanzia...

Alpha Conde na wenzie ujinga hawakuanza leo wala jana, ni miaka mingi sana wanafanya ukandamizaji huu... lakini hao wajeda tunaowasifia walikuwepo na walimlinda kwa nguvu zote..

Utaona hapo shida ni ile ile tu, ubinafsi na unafiki wa WaAfrica kujali matumbo..

Pale Cameroon kuna lijamaa linafanya ufala na wajeda wapo tu wanaliangalia...ila siku yakiguswa maslahi yao nao tutawaita mashujaa.
Upo sahihi Mkuu.
 
Kwa mzee wa miaka 83+ kung'ang'ania madaraka na kutaka atawale mpaka afe si mambo ya kizamani tu, bali ni ya kishamba na kishenzi sana.

Mapinduzi ya kijeshi ndio njia pekee iliyobaki maana sanduku la kura halishemiwi hata kidogo na wananchi ni mbumbumbu/cowards wasioweza kujitokeza na kushinikiza ving'ang'anizi kuachia madaraka kwa mujibu wa Katiba.

AU ni akina nani? 95% ni wazee 78+ ambao wapo madarakani kwa wizi, unyang'anyi na udanganyifu. Dictator Konte ni mwenzao na lazima wamtetee.

View attachment 1933057
Sanduku la wananchi halina maana tena. Akina Hamza tu
 
Msukosuko wake hautakua mdogo, unaweza kuichafua nchi isitawalike tena na kuvuruga mipango yote. Kila mmoja wetu ataathirika kwa namna moja ama nyingine.

Ikitokea, ipangwe na kuratibiwa vizuri utekelezaji wake, vinginevyo ni shida tupu.
Mapinduzi siyo kitu kizuri cha kutamani na mara nyingi yanaharibu nchi husika. Mungu atuepushe na mijitu kama Alpha Conde (ambaye sasa hivi yuko ndani ya gereza alilokuwa anawaweka wapinzani wake) ili wasituharibie bara letu la Africa na atuongezee akina Hichilema.
 
Unadhani mapinduzi yakitokea tutabaki kama hivi unachat tu kwa uhuru. Mapinduzi yanaleta dhiki soma historia nchi zilizofanya mapinduzi kama waliishi kwa raha tena.
Mapinduzi ni laana
No vizuri ukawashauri hao viongozi wa Afrika kusimi mwa jangwa la Sahara ili waache kujimilikisha nchi, watu na raslimali zote na badala yake wawe na uongozi jumuishi na shirikishi vinginevyo wanatengeneza mazingira rafiki ya mapinduzi ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya.
 
Kama ni utabiri wa kweli basi Waafrika tumeshindwa kujitawala. Tulipiga kelele wakoloni watuache tujitawale wenyewe lakini baada ya miaka zaidi ya 60 tunawaza mambo ya mapinduzi ya kijeshi. Junta au utawala wa kijeshi siyo jibu la matatizo yetu. Ni dalili ya kuwa demokrasia imetushinda na tumeshindwa kujitawala. Tungewaacha tuu wakoloni watawale mpaka tujifunze kwao jinsi ya kujitawala. Nchi kama South Africa ilichelewa kupata uhuru lakini iliwasaidia watu wake wajifunze jinsi ya kujitawala na kuendesha nchi. Sisi wengine tulikuwa na kiherere tukawafukuza mapema.

#FailedStates
Sure! Yote yanayotokea Africa kwa kushindwa kujitawala yalitabiriwa katika kitabu cha Animal Farm kilichoandikwa mwaka 1944. In fact kama siyo wakoloni kuja kuktutawala kimabavu na kuvuruga mifumo yetu ya kijadi ya machifu nk, tusingekuwa na hii mifumo ya hovyo ya kuibiana kura kwenye masanduku.
 
Akihojiwa na kipindi cha BBC kinachorushwa na television ya star TV tarehe 7 mwezi huu kuhusu mapinduzi ya Guinea, Jenerali Ulimwengu amesema yeye haoni ajabu Kwa yale yaliyotokea Guinea.

Na akatabiri pia kuwa hali hiyo ya kimapinduzi ya kijeshi itafika Kwa Kwa haraka sana ktk nchi zote zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Alipoulizwa kwanini anawaza hivyo alisema kuwa kilichokuwa kinafanywa na Alpha Conde ya ukandamizaji, dhurumati, kutokujali demokrasia, na uvunjifu wa haki za binadamu ,vitendo hivyo viovu vinafanywa pia na baadhi ya Serikali zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara na nchi zetu za Afrika Mashariki.

Jenerali aliendelea kushangaa kuona AU na ECOWAS wakilaani mapinduzi hayo huku wakiwa walishindwa kukemea matendo mabaya ya Rais Conde.

Alisema hali hiyo ya kimapinduzi ya kijeshi hayana muda mrefu itafika ktk nchi zetu wakati wowote kuanzia sasa.

Jenerali Ulimwengu ambae kwasasa ni mtu mzima na mwenye busara ni mtu asiyependa unafiki na hupenda kusema ukweli na maneno yake mara nyingi hutimia kama anavyotabiri.
Ni kweli kabisa. Tz ni nchi moja wapo ambayo haina chaguzi huru na haki.
 
Siku hizi amechukua nafasi ya shehe yahaya?
Anazeeka vibaya...Nahisi ni mtu mwenye uchungu mwingi baada ya ku realise positions kubwa alizotamani kuwa nazo na huku muda ukiwa umemtupa mkono...
 
Unadhani mapinduzi yakitokea tutabaki kama hivi unachat tu kwa uhuru. Mapinduzi yanaleta dhiki soma historia nchi zilizofanya mapinduzi kama waliishi kwa raha tena.
Mapinduzi ni laana
Ndio maana tunaishi kwa dhiki sababu ya mapinduzi ya ccm Zanzibar
 
Mapinduzi ni mambo ya kizamani!
Na kuvunja katiba na kutokuheshimu demokrasia ni mambo yaliyopitwa na waksyi kabisa katika ulimwengu huu uliostarabika. Ulimwengu yuko sahihi, next time tusishangae ni ........a
 
Hivi mapinduzi yanapotokea uchumi nao unakua?,hahahahahahaha,msiwaze mapinduzi nyie nchi huwa kama imekumbwa na msiba wa kitaifa
 
Back
Top Bottom