Jenerali Ulimwengu: Sioni ajabu mapinduzi ya kijeshi Guinea. Yatafika haraka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara

Jeshi lafaa likatae zuluma na sio kuvizia teuzi,jeshi la teuzi linachoweza labda kupindua meza na sio kupindua dhuluma.
Jeshi linapokuwa sehemu ya dhuluma hilo sio jeshi la wananchi
 
Hongera Generali Ulimwengu. Kwa uzoefu wake wa Siasa za nchi hizo, na ukizingania amekuwa ndani ya siasa hizo kwa miongo takribani 4 hivi, anajua kabisa nini kinaenda kutokea soon.

Watu wanasahau kuwa hao wanaofanya mapinduzi si ndugu wala wajomba au mashangazi wa watawala.

Ndugu zao ni hao wanaodhurumiwa haki zao, wanateswa na kufungwa kwa sababu za uongo, ni hao wanaobebeshwa mizigo ya Kodi na matozo ya kila aina...hao ndio ndugu zao, wajomba, shangazi, Baba wakubwa na wadogo, Mama wakubwa na wadogo nk.

Ukiona mwanasiasa kuntu kama Ulimwengu anasema hayo, ujue hata huko ndani ya wanaofanya mapinduzi kuna yanayoendelea yenye mlengo huo.

Siku atatokea shujaa mmoja na wenzake, watahakikisha hawafanyi makosa km yalebya miaka ya 80...

Ahsante Kaka Ulimwengu, kuwaeleza ukweli na kupeleka ujumbe kwa wahusika kuwa wanaweza kufanya kwasababu sababu zipo, nia ipo na uwezo wanao.
 
Akihojiwa na kipindi cha BBC kinachorushwa na television ya star TV tarehe 7 mwezi huu kuhusu mapinduzi ya Guinea, Jenerali Ulimwengu amesema yeye haoni ajabu Kwa yale yaliyotokea Guinea...
Kuna mambo mawili Jumuia iliyostaarabika haiwezi kuvumilia, inatakiwa kuwa na ZERO TOLERANCE: ugaidi na mapinduzi ya kijeshi. Ukiona mtu anatoa lisingizio, chochote kile, ukimchimba utakuta ana lake jambo ukilitafuta utalipata tu. It is conclusive evidence we have lost this person.
 
Mzee aache kututisha, wao wamekula maisha kukiwa hamna vita kipindi chao sasa iweje leo atutabirie dhiki?
Tusiogope kivuli cha ukweli....ndio calc za siasa zilivyo....utabiti ni sawa
 
AU ni club ya viongozi wa nchi za kiafrika kukutana kupongezana jinsi wanavyo watesa wananchi wao. Mmoja wao akipinduliwa hukauka makookwa kupiga kelele aachiwe.
 
Akihojiwa na kipindi cha BBC kinachorushwa na television ya star TV tarehe 7 mwezi huu kuhusu mapinduzi ya Guinea, Jenerali Ulimwengu amesema yeye haoni ajabu Kwa yale yaliyotokea Guinea...
Baada ya mapinduzi,maisha ya wa Guinea yameshakuwa bora au wanashangilia upepo huku akina Bounay ndio wakibadili kula jikoni? πŸ˜‚πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Mapinduzi bado sio njia salama
Nchi nyingi Sana zimepindua lakini hakuna cha maana kimefangika ni kubadili walaji jikoni.

Mapinduzi yenye tija labda yaongozwe na wananchi tuu sio wanajeshi kuanzia mali,Mauritania,Egypt na nchi nyingi za Western Afrika lakini hakuna kipya
 
Akihojiwa na kipindi cha BBC kinachorushwa na television ya star TV tarehe 7 mwezi huu kuhusu mapinduzi ya Guinea, Jenerali Ulimwengu amesema yeye haoni ajabu Kwa yale yaliyotokea Guinea...
Itakuwa vzr,tuyatoe haya majitu serikalini,tuweke damu mpya,

Nikisikia haya majina,Ndugai,Samia,Maghufuri, Kikwete, Mkapa, Mwigulu, Jafo, Majaliwa nahisi kichefu chefu,
 
Hiyo para grafu ya chini kabisa umeongeza wewe lakini tukubaliane hilo
 
Reactions: bne
Akihojiwa na kipindi cha BBC kinachorushwa na television ya star TV tarehe 7 mwezi huu kuhusu mapinduzi ya Guinea, Jenerali Ulimwengu amesema yeye haoni ajabu Kwa yale yaliyotokea Guinea...
China na Russia hakuna mapinduzi kwani haki za binadamu ni kwenye karatasi tu.
 
Hongera Generali Ulimwengu. Kwa uzoefu wake wa Siasa za nchi hizo, na ukizingania amekuwa ndani ya siasa hizo kwa miongo takribani 4 hivi, anajua kabisa nini kinaenda kutokea soon...
Mm bwana Niko pamoja Na wewe kwakweli kwanguvu zetu tumeshindwa kuondoa udharimu, lbs wao wanaweza saidia.

Unajua hats Guinea wananchi walishindwa kabisa kumuondoa konde HADI jeshi lilipoingilia kati
 
Lkn kama serikali iliyopo madarakani inatumia wanajeshi kutesa watu, kupiga watu Na kuumiza watu, ajabu inakua wapi jeshi hilo hilo likiwageuka wao?
 
Mwisho wa kunukuu.
 
Lkn kama serikali iliyopo madarakani inatumia wanajeshi kutesa watu, kupiga watu Na kuumiza watu, ajabu inakua wapi jeshi hilo hilo likiwageuka wao?
Kama wanapewa mgao hutokaa usikie hadi Yesu anarudi.
Ukiona Dikteta ana savaivu ujue anaelewa kula vizuri na hawa watu
 
A.U ni uchuro tu hapa Africa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…