Jeneza lazikwa Tupu Mwili wasaulika ndani

Jeneza lazikwa Tupu Mwili wasaulika ndani

Swensa

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
2,880
Reaction score
4,295
JENEZA LAZIKWA TUPU MWILI WASAHAULIKA NDANI

Tukio la kushangaza limetokea katika kijiji cha Ikuti, kitongoji cha Kinyika, kata ya Ikuti wilayani Rungwe mkoani Mbeya baada ya wananchi waliokuwa wamemzika marehemu Maulid Bukuku kurejea nyumbani na kuukuta mwili wake ukiwa bado umelazwa kitandani.

Awali, wananchi pamoja na ndugu wa marehemu walikuwa wameelekea makaburini kwa ajili ya mazishi na kufanikisha shughuli hiyo wakiamini wamemlaza marehemu katika nyumba yake ya milele.

Hata hivyo, waliporudi nyumbani walipatwa na taharuki kubwa baada ya kuukuta mwili wa marehemu ukiwa bado ndani ya nyumba hali iliyozua sintofahamu kubwa.

Baadhi ya wananchi walidai huenda marehemu amefufuka huku wengine wakisema “amegoma kuzikwa,” jambo lililosababisha taharuki na watu kukimbia huku na kule wakishindwa kuelewa kilichotokea.

Baada ya hali kutulia na wafiwa kutafakari kwa kina, ndipo walipobaini kuwa katika pilikapilika za maandalizi ya mazishi walipeleka jeneza makaburini bila kuweka mwili wa marehemu ndani yake, na hivyo kuuzika mwili “kwa kusahau.”

Kutokana na tukio hilo, taarifa zilitolewa kwa uongozi wa kijiji kupitia mwenyekiti wa kijiji cha Ikuti, Hakimu Njela, ambaye aliwasiliana na Jeshi la Polisi pamoja na polisi kata kwa ajili ya hatua zaidi.

Baada ya kupata ruhusa rasmi, kaburi lilifukuliwa mbele ya wananchi na ndugu wa marehemu ambapo ilibainika kuwa jeneza lilikuwa tupu kabisa, hali iliyothibitisha kuwa mwili wa marehemu haukuwa umezikwa.

Hatimaye, mwili wa marehemu ulirejeshwa makaburini na mazishi kufanyika upya kwa kufuata taratibu zote zinazostahili.

NINI SABABU ZA MWILI KUACHWA

Kabla umauti marehemu alikuwa akiugulia kijiji jirani na alipofariki alikuwa amedhoofu.

Ndugu zake pamoja na wasamaria wema waliubeba mwili hadi nyumbani kwao kisha kuulaza kitandani chumbani ilhali jeneza likiendelea kuandaliwa,kama ilivyo mila na desturi za kinyakyusa ndugu jamaa na mara Fiji kununua blanket au shuka kuufunika mwili wa marehemu na ndivyo ilivyotokea.

Jeneza lilipoletwa ndugu wa karibu waliitana chumbani alikolazwa marehemu vikao vikiendelea na kila mmoja alitoka nje kwa wakati wake na waliporudi wakiamini mwili umewekwa sandukuni na ukatolewa nje kwa ibada fupi kisha jeneza kubebwa hadi makaburini na maziko kufanyika.

Ikumbukwe kuwa marehemu aliugua kwa muda hivyo alidhoofu na mashuka na blanketi alizofunikwa ilikuwa si rahisi kubaini kuwepo kwa mtu kitandani.

Sakata lilianza jioni watu waliokuwa hawana blanket za kujifunika ndipo walipoingia chumbani na kuchukua mashuka na ndipo walipobaini mwili wa marehemu kitandani.

Mkoani Mbeya matukio haya si mageni imewahi kutokea Ushirika Rungwe,Isanga Mbeya nk.

FUNZO
Unapotokea msiba ndugu wa karibu wanitahidi kuwa makini kuanzia hospitali hadi nyumbani ili kuepuka kuzika majeneza matupu au miili ya watu wengine.
1779535544060.jpg
 

Attachments

  • 1779535537954.jpg
    1779535537954.jpg
    353.9 KB · Views: 22
Maajabu!! Haya mambo yapo sio huko tu na hutokea kama ndugu wa marehem wasipokuwa makini au kuogopa kuangalia maiti au kumwongea mlinzi wa mortuary vibaya. Mimi nilishaona watu wamefata mwili ila wakaja na mwili tofauti. Yaani aliyefariki alikuwa mzee ila wakaja na mwili wa mmama. Mjukuu wa miaka kumi na mbili ndo alishtuka after mwili umewekwa hapo nje wanaangalia ndo wauingize ndani akasema kuwa huyo sio babu yake mda huo watu wameng'ang'ana kuwa mtu akifa mwili hubadilika ila yeye akakomalia kuwa yule sio babu yake kweli kuja kuchunguza wamepewa wa kike ikabidi warudishe upya. Hayo sio mageni bali ni maajabu.
 
Walaumiwe hai ndugu wazembe.walipanga nani nani nani wataueudisha mwili ndani ya jeneza ama Kila mtu akajiondokea Anamzengea mwenzie.

Hovyo kabisa😒
 
Back
Top Bottom