GreenHouse
JF-Expert Member
- Oct 11, 2011
- 280
- 262
- Thread starter
- #221
Dawasco bili yake sio mchezo, na vile ulisema angalau kwa siku zisipungue lita 200 (Ndoo kubwa 10).
Labda option ya kuvuna maji ya mvua, ambayo sasa wasiwasi wangu hii sio ya mwaka mzima kutokana na majira ya mvua, hivyo hata return itakua ndogo kwa kutolima mwaka mzima!!
Tunajadili tu, but otherwise nikishasafisha shamba lazima nikuone!!
Ni kweli bili ya dawasco itakugharimu lakini maji ya aina yoyote ile hayapatikani bure. Kisima kinahitaji pump hivyo kuhitaji umeme either wa Tanesco, Solar au Generator, na zote hizo ni gharama japo si kubwa.
Unaweza kuvuna lita elf 50 za maji kwa mvua za wiki moja tu.
Mfano mzuri ni jana usiku. Mvua iliyonyesha jana dar kwa mtu ambaye tayari ana tank la kuhifadho maji ingetosha kabisa kujaza maji ya matumizi ya mwaka mzima au miezi kama 9. Hata kama mvua si za kila mwezi lakini sidhani kama inaweza kupita miezi 9 bila mvua kunyesha.
Karibu sana.