Jenga Greenhouse kwa gharama nafuu

Hongera kwa fursa hii!

Binafsi nime review hii blog na pia information za kwenye website yako. Wenzetu wakenya wameanza zamani,problem yetu gharama zimewekwa juu kwa mtu wa wastani. Tumewasiliana pia kwa email though nimekupigia mara nyingi simu haipokelewi. Nimeona pia kipindi mnachoendesha TBC1.
Sababu nimekupigia ni
1.Kupata nafasi ya kuona actual greeenhouse huko uliko jenga. Seeing is believing!!
2. Tangu umeanza hii project,umeweza kujenga wapi dsm hii au jirani!?Utakubaliana nami kuwa tukipata nafasi ya kuonana na wateja wako na kupata positive testimonial itatupa imani kubwa zaidi na kukuza biashara yako. Nakubaliana na ww gharama zako ni reasonable compared na Balton lakini bado ni investment kubwa kwa mjasiriamali wa wastani;pesa na muda. Hivyo motivation ipo kwenye kutenda
 
Tafadhali tembelea MASKANI | Horti Organics kwa taarifa zaidi.

Kaka nimetishika kidogo,
Katika pitia pitia ya hii Website yako nimekutana kipengele kimoja cha bei nikashtuka sana.
[h=4]"Ujenzi wa Greenhouse unagharimu kiasi gani?[/h]Ujenzi wa Greenhouse unagharimu shilingi 35,000 kwa mita moja ya mraba kama itajengwa Dar Es Salaam, shilingi 37,500 kwa mita moja ya mraba kwa mikoa isiyo na baridi kali na 45,000 kwa mita moja ya mraba iwapo inajengwa katika mikoa yenye baridi kali kama Arusha, Mbeya, Iringa nk. Hivyo basi kama unajenga Greenhouse Dar Es Salaam na ina ukubwa wa mita za mraba 120 utakugharimu shilingi 4,200,000 Tu"
Hii naona inatofautiana na ile bei pale Juu ya 2.5Million, au kuna mahali sijaelewa?
 
Bei ya hapo ni ya material na bei ya kwenye website ni ya greenhouse nzima iliyokwisha jengwa na kupandwa miche. Hivyo ni vitu viwili tofauti
 

Samahani sana, napokea simu zaidi ya 500 kwa siku, ni ngumu sana kupokea zote zitakazoingia, ukiona simu haijapokelewa ujue naongea na mteja mungine hivyo suluhisho ni kutuma sms, Najibu msg zote kila siku na napokea sms zaidi ya 300 kwa siku
Ndio unaweza kuja kuona greenhouse yangu, ipo mikwambe kigamboni, Ukifika mikwambe uliza madereva wa boda boda wapi kuna nyumba ya manylon imepandwa nyanya utaonyeshwa tu, ni mita 100 kutoka barabara ya lami.
Najenga greenhouse mbili sasa hivi mbezi beach, nyingine mbezi kwa msumi, nyingine mkuranga, nyingine chanika, nyingine dodoma, mwanza, Arusha, Boko nk nk nk, Ukiongea na wateja sasa hv watakupa experiance yao nami lakini hawatokupa mafanikio waliyoyapata kwani ndio kwaanza mazao yao ni machanga mno.
 
Mkuu,

Hongera kwa kuleta hii mada naomba nitumie huo mchanganuo kwenye e-mail yangu LORDTICAL@GMAIL.COM

Mengine naona itakuwa rahisi nikifika Kigamboni kujifunza zaidi.

Natanguliza shukrani.
 
MamaNa naomba nitumie details zote kwenye email yangu jmakyao@gmail.com plx do that nataka kuanza june na nilishataka kuwapa balton hiyo kaz nipo arusha...
 
Asante sana mleta mada na wachangiaji wote, mie nina swali moja tu. Mazao yanayolimwa katika greenhouse kulingana na uzi huu ni strawberry, tomatoes, hoho, matango, pilipili. Kuna zao jingine tofauti na hayo? Lipi na lipi? Asanteni.
 

Mkuu me nipo Mwanza na nipo very very interested... hebu niunganishe na huyo mteja wako wa Mwanza nikaone afu nami nikuombe unitengenezee...seeing is believing!
 

Mkuu salute!

Nitafurahi kupata updates...!
 
Mkuu me nipo Mwanza na nipo very very interested... hebu niunganishe na huyo mteja wako wa Mwanza nikaone afu nami nikuombe unitengenezee...seeing is believing!
Nakuja mwanza Next week Mungu akipenda, tuwasiliane kwa simu.
 
GreenHouse
Je hizo green house za miti zinaweza kukaa muda gani?
Je ikitokea ikaharibika nini kama kampuni itafanya?
Nimetembelea blog yenu ila sijaona sehemu imeandikwa kuhusu mboga kama mchicha,sukuma wiki,
Je naweza lima mchicha, sukuma wiki na mboga nyingine kwenye green house?
 
Last edited by a moderator:

Greenhouse za miti zinakaa hadi miaka 10, lakini kila baada ya miaka mitano itabidi ubadili poly covers (hata kwenye chuma ni hivihivi)
Ikiharibika kwa sababu za kiufundi tutakurekebishia na kama ni uharibifu binafsi tutakucharge kurekebisha.. Kifupi kabla hatujakufungia greenhouse tutasign MOU na contract ya service delvery, haya mambo utayajua tukishaonana.
Napendelea zaidi kuongea na mteja kwenye simu au business email kwani inakuwa rahisi kukeep record ya nimeongea na nani nini. Hapa JF hata majina hatujuani.

NB: Kila aina ya mboga inaweza kulimwa ndani ya greenhouse.
Karibu sana.
 
GreenHouse,

Nikitaka kufunga huo Mtambo Bagamoyo Gharama zitakuwaje?
 
GreenHouse,

Nikitaka kufunga huo Mtambo Bagamoyo Gharama zitakuwaje?

Bagamoyo bei ni 37,500 kwa square meter moja, hivyo ukitaka kujenga ukubwa wowote zidisha urefu na upana kisha zidisha mara 37,500... Hii ni gharama ya kila kitu, kuanzia kupimiwa udongo na maji mpaka kupandiwa miche na kufundishwa kulima.
NB: Gharama ya usafiri wa Mafundi na Mimi ni nje ya gharama za ujenzi... Sisi tutagaramia usafiri wa material tu.
Mfano anayejenga greenhouse Singida atakuwa na tofauti na anayejenga katavi nk...The closer you are to the city the cheaper it is to build a greenhouse.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…