Jenga Greenhouse kwa gharama nafuu

Jenga Greenhouse kwa gharama nafuu

Hongera kwa fursa hii!

Binafsi nime review hii blog na pia information za kwenye website yako. Wenzetu wakenya wameanza zamani,problem yetu gharama zimewekwa juu kwa mtu wa wastani. Tumewasiliana pia kwa email though nimekupigia mara nyingi simu haipokelewi. Nimeona pia kipindi mnachoendesha TBC1.
Sababu nimekupigia ni
1.Kupata nafasi ya kuona actual greeenhouse huko uliko jenga. Seeing is believing!!
2. Tangu umeanza hii project,umeweza kujenga wapi dsm hii au jirani!?Utakubaliana nami kuwa tukipata nafasi ya kuonana na wateja wako na kupata positive testimonial itatupa imani kubwa zaidi na kukuza biashara yako. Nakubaliana na ww gharama zako ni reasonable compared na Balton lakini bado ni investment kubwa kwa mjasiriamali wa wastani;pesa na muda. Hivyo motivation ipo kwenye kutenda
Nauza Materials na kusadia ujenzi wa Greenhouse za ukubwa mbali mbali.

Kwa sasa Nina materials zinazoweza kucover greenhouse ya ukubwa wa mita nane kwa mita kumi na tano (8x15m), Zina uwezo wa kuzuia jua, kuzuia wadudu na vihatarishi mbali mbali vya mazao.

Bei ni Mil2.5 kwa materials pekeyake yaani 1/8 of an ancre drip lines, Polythene Cover (UV400 Protected sheets), 70% Micron insect Netting...Hizi zitakuwezesha kujenga Greenhouse yako bila matatizo. Kitakachohitajika kutoka kwako ni Wooden Poles (nguzo kama zinazojengewa baa za makuti nk), tanki la lita 500 la maji na maji ya uhakika.

Ntakupatia mafundi na muongozo mzima wa kujenga greehouse yako ili kufanikiwa.

Faida za kulima katika greenhouse ni nyingi mno, ikiwemo matumizi mazuri na sahihi ya ardhi, kwani kiwanja cha ukubwa wa mita 8x15 kinaweza kukupa Nyanya hadi Tani 30 kwa mwaka, Pilipili hoho tani 20 kwa mwaka na mazao mengine mengi yanayolimwa katika controlled environment.

Kuna wataalamu wa kutosha hivi sasa hapa Dar Es Salaam wanaoweza kukupa muongozo, mbegu bora na fertilizers za uhakika.. Tuwasiliane kwa simu namba 0714881500 ili kupeana muongozo.

Karibuni sana.
Ili uweze kufanikiwa katika kilimo hiki, unahitaji maji ya uhakika minimum lita 200 kwa siku kwa ajili ya kumwagilia nyanya kwa matone, Nitakupatia mabomba (driplines) zitakazokuwezesha kufanikisha hili.

NB: Kumbuka Greenhouse inajengwa kwenye eneo lililo wazi, lisilo na miti mirefu inayozuia jua...

Pia ni Muhimu kufanya Soil Test na Water Test ili ujue ni kipi unahitaji kuongeza kwenye ardhi yako ili upate mazao ya uhakika... Naweza kukusaidia kufanya soil na water test kwa gharama nafuu kabisa kutoka nchi ya Jirani (kenya). Gharama ni 250,000 kwa huduma hii pekeyake (Complete Soil analysis & Water Test).

NB::: UJENZI WA GREENHOUSE YA MFANO UMEKAMILIKA. IPO MIKWAMBE KIGAMBONI::: KARIBUNI SANA.

View attachment 140539 View attachment 140540 View attachment 140541 View attachment 140542 View attachment 140543 View attachment 140547

Kuna watu wengi sana wamenipigia na kuomba niwasaidie kufanya mchakato wa kuandika mchanganuo wa kuomba mkopo bank (bankable business plans and proposals) au taasisi za fedha ili wafanikishe mradi huu.

Habari njema ni kwamba, tumeingia makubaliano maalumu na kampuni moja hapa nchini (Biznocrats consulting enterprise) inayojihusisha na kuandika michanganuo ya kibiashara, ushauri wa kifedha, accounts nk na wamekubali kuwaandikia wateja wetu wote michanganuo hiyo kwa gharama ya asilimia moja tu (1%) ya mkopo Minimum 500,000 na wanakuhakikishia hautokosa mkopo wa aina yoyote.

Kama unahitaji huduma hii, tuwasiliane ili tuweze kufanikisha hili pamoja.

Karibuni sana.
 
Tafadhali tembelea MASKANI | Horti Organics kwa taarifa zaidi.

Kaka nimetishika kidogo,
Katika pitia pitia ya hii Website yako nimekutana kipengele kimoja cha bei nikashtuka sana.
[h=4]"Ujenzi wa Greenhouse unagharimu kiasi gani?[/h]Ujenzi wa Greenhouse unagharimu shilingi 35,000 kwa mita moja ya mraba kama itajengwa Dar Es Salaam, shilingi 37,500 kwa mita moja ya mraba kwa mikoa isiyo na baridi kali na 45,000 kwa mita moja ya mraba iwapo inajengwa katika mikoa yenye baridi kali kama Arusha, Mbeya, Iringa nk. Hivyo basi kama unajenga Greenhouse Dar Es Salaam na ina ukubwa wa mita za mraba 120 utakugharimu shilingi 4,200,000 Tu"
Hii naona inatofautiana na ile bei pale Juu ya 2.5Million, au kuna mahali sijaelewa?
 
Kaka nimetishika kidogo,
Katika pitia pitia ya hii Website yako nimekutana kipengele kimoja cha bei nikashtuka sana.
"Ujenzi wa Greenhouse unagharimu kiasi gani?

Ujenzi wa Greenhouse unagharimu shilingi 35,000 kwa mita moja ya mraba kama itajengwa Dar Es Salaam, shilingi 37,500 kwa mita moja ya mraba kwa mikoa isiyo na baridi kali na 45,000 kwa mita moja ya mraba iwapo inajengwa katika mikoa yenye baridi kali kama Arusha, Mbeya, Iringa nk. Hivyo basi kama unajenga Greenhouse Dar Es Salaam na ina ukubwa wa mita za mraba 120 utakugharimu shilingi 4,200,000 Tu"
Hii naona inatofautiana na ile bei pale Juu ya 2.5Million, au kuna mahali sijaelewa?
Bei ya hapo ni ya material na bei ya kwenye website ni ya greenhouse nzima iliyokwisha jengwa na kupandwa miche. Hivyo ni vitu viwili tofauti
 
Hongera kwa fursa hii!

Binafsi nime review hii blog na pia information za kwenye website yako. Wenzetu wakenya wameanza zamani,problem yetu gharama zimewekwa juu kwa mtu wa wastani. Tumewasiliana pia kwa email though nimekupigia mara nyingi simu haipokelewi. Nimeona pia kipindi mnachoendesha TBC1.
Sababu nimekupigia ni
1.Kupata nafasi ya kuona actual greeenhouse huko uliko jenga. Seeing is believing!!
2. Tangu umeanza hii project,umeweza kujenga wapi dsm hii au jirani!?Utakubaliana nami kuwa tukipata nafasi ya kuonana na wateja wako na kupata positive testimonial itatupa imani kubwa zaidi na kukuza biashara yako. Nakubaliana na ww gharama zako ni reasonable compared na Balton lakini bado ni investment kubwa kwa mjasiriamali wa wastani;pesa na muda. Hivyo motivation ipo kwenye kutenda

Samahani sana, napokea simu zaidi ya 500 kwa siku, ni ngumu sana kupokea zote zitakazoingia, ukiona simu haijapokelewa ujue naongea na mteja mungine hivyo suluhisho ni kutuma sms, Najibu msg zote kila siku na napokea sms zaidi ya 300 kwa siku
Ndio unaweza kuja kuona greenhouse yangu, ipo mikwambe kigamboni, Ukifika mikwambe uliza madereva wa boda boda wapi kuna nyumba ya manylon imepandwa nyanya utaonyeshwa tu, ni mita 100 kutoka barabara ya lami.
Najenga greenhouse mbili sasa hivi mbezi beach, nyingine mbezi kwa msumi, nyingine mkuranga, nyingine chanika, nyingine dodoma, mwanza, Arusha, Boko nk nk nk, Ukiongea na wateja sasa hv watakupa experiance yao nami lakini hawatokupa mafanikio waliyoyapata kwani ndio kwaanza mazao yao ni machanga mno.
 
Mkuu,

Hongera kwa kuleta hii mada naomba nitumie huo mchanganuo kwenye e-mail yangu LORDTICAL@GMAIL.COM

Mengine naona itakuwa rahisi nikifika Kigamboni kujifunza zaidi.

Natanguliza shukrani.
 
MamaNa naomba nitumie details zote kwenye email yangu jmakyao@gmail.com plx do that nataka kuanza june na nilishataka kuwapa balton hiyo kaz nipo arusha...
 
Asante sana mleta mada na wachangiaji wote, mie nina swali moja tu. Mazao yanayolimwa katika greenhouse kulingana na uzi huu ni strawberry, tomatoes, hoho, matango, pilipili. Kuna zao jingine tofauti na hayo? Lipi na lipi? Asanteni.
 
Samahani sana, napokea simu zaidi ya 500 kwa siku, ni ngumu sana kupokea zote zitakazoingia, ukiona simu haijapokelewa ujue naongea na mteja mungine hivyo suluhisho ni kutuma sms, Najibu msg zote kila siku na napokea sms zaidi ya 300 kwa siku
Ndio unaweza kuja kuona greenhouse yangu, ipo mikwambe kigamboni, Ukifika mikwambe uliza madereva wa boda boda wapi kuna nyumba ya manylon imepandwa nyanya utaonyeshwa tu, ni mita 100 kutoka barabara ya lami.
Najenga greenhouse mbili sasa hivi mbezi beach, nyingine mbezi kwa msumi, nyingine mkuranga, nyingine chanika, nyingine dodoma, mwanza, Arusha, Boko nk nk nk, Ukiongea na wateja sasa hv watakupa experiance yao nami lakini hawatokupa mafanikio waliyoyapata kwani ndio kwaanza mazao yao ni machanga mno.

Mkuu me nipo Mwanza na nipo very very interested... hebu niunganishe na huyo mteja wako wa Mwanza nikaone afu nami nikuombe unitengenezee...seeing is believing!
 
Naomba nitoe mrejesho wa maendeleo wa Greenhouse yetu ya mfano iliyopo Mikwambe kigamboni.
Tumepanda nyanya greenhouse nzima, tuliotesha miche kwenye nursery trays tar 3 march na tar 24 march nusu ya miche ikahamia ardhini na tar 2 April Nusu nyingine ikahamia ardhini. Tumefanya hivi ili kuongeza production cycle kwa wiki moja na kama process ya kutest bugs kwenye udongo, kwani kama kungekuwa na vihatarishi mimea ingeharibika nusu tu na si kitalu kizima...
Sasa hivi Miche yenye wiki mbili ardhini imeshafikia urefu wa futi moja na nusu na unene wa 16mm. Na ile yenye siku 4 imeshafika cm25 na unene wa mm6. Haya ni maendeleo mazuri sana na Mungu akijaalia ntazidi kuleta mrejesho hapa mwenzi kwa mwezi au kila baada ya wiki mbili... Naambatanisha picha kwa kumbukumbu zenu.

View attachment 149561 View attachment 149563 View attachment 149646
View attachment 149649 View attachment 149647 View attachment 149648

Mkuu salute!

Nitafurahi kupata updates...!
 
Mkuu me nipo Mwanza na nipo very very interested... hebu niunganishe na huyo mteja wako wa Mwanza nikaone afu nami nikuombe unitengenezee...seeing is believing!
Nakuja mwanza Next week Mungu akipenda, tuwasiliane kwa simu.
 
GreenHouse
Je hizo green house za miti zinaweza kukaa muda gani?
Je ikitokea ikaharibika nini kama kampuni itafanya?
Nimetembelea blog yenu ila sijaona sehemu imeandikwa kuhusu mboga kama mchicha,sukuma wiki,
Je naweza lima mchicha, sukuma wiki na mboga nyingine kwenye green house?
 
Last edited by a moderator:

Greenhouse za miti zinakaa hadi miaka 10, lakini kila baada ya miaka mitano itabidi ubadili poly covers (hata kwenye chuma ni hivihivi)
Ikiharibika kwa sababu za kiufundi tutakurekebishia na kama ni uharibifu binafsi tutakucharge kurekebisha.. Kifupi kabla hatujakufungia greenhouse tutasign MOU na contract ya service delvery, haya mambo utayajua tukishaonana.
Napendelea zaidi kuongea na mteja kwenye simu au business email kwani inakuwa rahisi kukeep record ya nimeongea na nani nini. Hapa JF hata majina hatujuani.

NB: Kila aina ya mboga inaweza kulimwa ndani ya greenhouse.
Karibu sana.
 
GreenHouse,

Nikitaka kufunga huo Mtambo Bagamoyo Gharama zitakuwaje?
 
GreenHouse,

Nikitaka kufunga huo Mtambo Bagamoyo Gharama zitakuwaje?

Bagamoyo bei ni 37,500 kwa square meter moja, hivyo ukitaka kujenga ukubwa wowote zidisha urefu na upana kisha zidisha mara 37,500... Hii ni gharama ya kila kitu, kuanzia kupimiwa udongo na maji mpaka kupandiwa miche na kufundishwa kulima.
NB: Gharama ya usafiri wa Mafundi na Mimi ni nje ya gharama za ujenzi... Sisi tutagaramia usafiri wa material tu.
Mfano anayejenga greenhouse Singida atakuwa na tofauti na anayejenga katavi nk...The closer you are to the city the cheaper it is to build a greenhouse.
 
Back
Top Bottom