Ahsante sana...Gharama za materials ni none negotiable kwasababu sizitengenezi mimi, Lakini kwenye installation cost gharama inazungumzika kwasababu ni makubaliano kati yangu na mafundi. Pia Kama una mbolea yako au unaweza kupata lorry la mbolea sehemu, ni moja kati ya savings, au kama unaweza kuwa na tank la lita 200-500 ni vema zaidi... Lakini hiyo 2.5m ni ya kununua materials muhimu (polythene films, insect netting, drip lines na nursery set kwa ajili ya kukuzia miche ndani ya greenhouse)
Shukran na karibu sana tuijenge nchi yetu.vizuri sana, Hizi ndo habari tunazozitaka.
Kwa nyie mnaoishi Bongo water test anafanya Mama Kazinja (ni mhindi huyu), anafundisha Chuo cha Maji. Anatoa majibu baada ya siku 3 na gharama zake ni 150,000/=Mkuu soil analysis na water test wanafanya kupitia lab ya nani??? ......
Karibuni sana.
yaani kama umekuja muda muafaka, ila materials unatyoa kenya au hapa tz unaofisi yako? iko mtaa gani ofisi yako hapa tz, nataka kukutana na wewe unishauri mengi zaidi nimeangaika mpaka nikasema basi
Hii nimeipenda kuna wakati nilitaka kufanya huu umwagiliaji kwa njia ya drip lakini sikujua nianzie wapi,nikaenda hadi pale Mikocheni zamani pakiitwa Minazi pale ni kituo cha utafiti wa mbegu GMO na mambo ya green house,nikaambulia tu blah balh,panapo majaliwa mwakani nitamtafuta MamaNa ngoja nihifadhi namba zake za simu.Asante MamaNa kwa huu uzi muhimu,haya mambo ndio yanatakiwa na sio kila siku matangazo ya kuuza simu na magari
Vp kuhusu watu walioko mikoani mfano Arusha anaehitaji kufungiwa green house mnaweza fanya?
Inawezekana kabisa, hakuna shida yoyote. Karibu sana.
Kwa wale wanasafiri kwa njia ya Dar Mby, ipo moja imejengwa Rungemba kabla hujafika Mafinga mkono wa kushoto kama unakwenda Mby. Ukivuka kidaraja angalia kushoto kwako au kulia kwako kama unakuja Dar mara baada ya kupita Rungemba.
Hii tekinolojia italeta mapinduzi sana ktk kilimo, cha msindi tujiandae kusindika mazao yetu wenyewe.
Karibu sana, tuwasiliane kwa simu tuone ni jinsi gani tunaweza kufanya kazi pamoja.May God Bless you this is what I was looking for
Kiongozi hapo kwenye nyekundu umeongea jambo la msingi sana.
Karibu sana, tuwasiliane kwa simu tuone ni jinsi gani tunaweza kufanya kazi pamoja.