Asante sana kwa kutuletea hii kitu kwa bei nafuu. Nami pia naomba unitumie huo mchanganuo kwenye email yangu ( fmlyimo@yahoo.com ). Pia naomba unielekeze lilipo shamba la demo nije nikutembelee nijionee hayo mambo mazuri.
Hiyo dili imekaa poa sana hiyo, israel ni jangwa lakini wana export vegetable kuliko kawaida, siku nyingi nimekuwa na mipango ya kuwa na Greenhouse, tutatafutana. Ifike wakati vijana wa kitanzania tutumie elimu yetu kuzalisha na siyo kutembea na vibahasha kuomba kazi
Kweli kabisa, Hii technology na material ninayotumia yametoka Israel na Marekani. Kifupi Greenhouse imevumbuliwa miaka ya 1800 Huko Italia lakini waisrael wakaivalia njuga na hivi sasa wao ndio biggest exporters wa fruits and vegetables, kwa mfano wao ndio waliogundua kilimo cha Maembe cha high density yaani wanapanda miembe 900 katika heka moja na inakuja kuvuna maembe 600 kwa kila muembe, bila kutumia madawa.
Karibuni sana tulime kisasa, Tutaikomboa hii nchi.
Kilimo ndio kitu pekee hautaulizwa na TRA kwani kina msamaha wa kodi. Ni ushuru na malipo madogo madogo sana.
Ardhi tunayo, Nguvu tunazo, na Uwezo Tunao... Kwanini Hatuendelei!!!
Hapo kwenye maembe naomba nikupm ili tusiharibu hii mada.
NCH hii kutofanikiwa ni Utayari wako manake kila kitu kipo kwenye Elimu za Ujasiliamali ndo kabisaa,,,! mamaNA nimechukua Nmba J3 ya tar 3 Nitakuja kigamboni,,!
mamaNa nashukuru sana kwa maelezo yako, naomba kitu kimoja, uwezo wangu kipesa siyo mkubwa, hitaji langu ni kuanza kufanya manunuzi ya vifaa kidogo kidogo hasa hayo makaratasi ya kuezekea, je nitayapata wapi hapa jijini Dar es Salaam?
Nimeshakutumia ndugu.Mama Na......Nashukuru Sana Kwa Elimu Na Mwanga Ulioutoa Kuhusiana Na Green House Technology Katika Kilimo Chenye Manufaa Na Tija, Natumai Kupitia Thread Hii Watanzania Wengi Wataelimika Na Kupata Hamasa Zaidi Ya Kufanya Kilimo Chenye Tija Hata Maeneo Ya Mijini Kwani Kwa Kutumia Teknolojia Hii Hauhitaj Kuwa Na Eneo Kubwa Hvyo Unaweza Hata Kuifanya Back Yard Nyumbani Kwako.
Nami Pia Ninaomba Unitumie Mchanganuo Mzima Wa Kutengeneza System Hii Kuanzia Materials Na Bei Zake Ukijumlisha Pia Hizo Drip Line Za Umwagiliaji Kwa Matone. Kwa Muda Mrefu Nimekuwa Nikihtaji Hii Technology Kwa Bei Nafuu Katika Kufanya Integration Vizuri Ya Ufugaji Wa Samaki Na Kilimo Cha Mboga Mboga Na Matunda, Pia Katika Designing And Establishment Ya Aquaponics System.
Nitumie Kupitia Email Hii: Daveaquatz@gmail.Com.
Nashukuru.
Karibu sana, tuombe uzima.
Ujenzi wa greenhouse ya mfano umekamilika. Ipo mikwambe kigamboni,
Karibuni sana.
View attachment 141656 View attachment 141657 View attachment 141658 View attachment 141661 View attachment 141662
Mkuuu Kigamboni kuna sehemu ina udongo mwekundu? Nilifikiri ni Kichanga tu au umetoa sehemu nyingine huo udongo?
kaka hii ishu ni fantastic..najipanga mkuu..
Udongo wangu sio mwekundu na sijautoa kokote, ni mweusi wa kichanga flani ila nadhani hiyo reflection ya films za juu na camera vimechangia kuonekana mwekundu. Au unarefer baadhi ya picha hapo, yes kuna nyingine hazijapigwa kigamboni... udongo mwekundu upo sehemu nyingi tu kigamboni...
Nilikua najaribu kufanya comparison na udongo wangu wa kichanga Mkuranga kama utafaa kwa nyanya na Hoho shamba langu ni pure kichanga itabidi kufanya soil analysis kwanza kabla ya kufanya chochote