mamaNa,
Naweza kupata full package ya hii kitu ni Tshs ngapi? inclusive of everything. Vipi Mbegu, madawa na mbolea?
Pili nimeona umesema hizi zinatumia wooden poles, ndio mirunda?
Vipi kuliwa na wadudu?
Na kama eneo lina maji muda wote wa mwaka (mto mkubwa au kisima cha kudumu), naweza kulima kwa muda gani au mara ngapi kwa mwaka??
Full package ya greenhouse ni 3.5m kama uko Dar, Itaongezeka kidogo kama uko nje ya dar kwasababu ya kusafirisha materials na mafundi ila gharama haitozidi laki tano (hiyo nyongeza) hata kama utakuwa kigoma.
Yes zinatumia wooden poles Lakini sio za mirunda (life span yake ni ndogo mno), Tunatumia Mikaratusi yaani miti ambayo tanesco wanatumia kwenye kusimamisha nguzo zao za umeme... Tunakupa guarantee ya miaka 10, Structure yako haitokuja kuharibika kwani kuna preventive measures kubwa sana tunazichukua kuzuia kuoza na kuliwa na wadudu, special treatment na films maalumu...
Eneo lolote lile utalima mwaka mzima, hiki sio kilimo cha msimu.. Mvua inyeshe haitoingia kwenye kitalu shamba chako, jua liwake halitodhuru mazao yako kwani ndio mfumo mzima wa kilimo hiki (controlled environment)...Kama kuna maji ya mto au kisima au ya kuvuna mvua, yatafaa kabisa lakini ni muhimu tukayapima ili tujue ph level, sodium, manganese nk... hii itasaidia kukushauri aina ya mbolea na ratio. Kumbuka unatumia lita 250-300 tu kwa siku
Kuhusu mbegu zinazopandwa ni hybrid, zenye uwezo wa kutoa mmea unaoishi muda mrefu na zenye kuwa na mmea mrefu wenye futi zaidi ya Kumi...
Kuhusu mbolea - tunapokutengenezea greenhouse tunakuwa tumeshatengeneza matuta kwa mchanganyiko maalumu wa mbolea husika zitakazo kuza mimea na kuilisha mwaka mzima, kitakachobaki ni kufanya top dressing when needed, ntakufundisha jinsi ya kufanya hili...
Madawa - Tunajaribu kuwaelimisha watu kuacha kutumia madawa na viwandani kwani madhara yake ni makubwa sana kwa ardhi, mimea na binadamu kwa ujumla, hivyo tutakufundisha organic farming, fertilizing and fumigating.. hii ina gharama ndogo na mazao ni ya ubora wa hali ya juu na yenye ladha tamu...
Gharama ya mbegu ni 200,000 lakini kama utahitaji nikuoteshee kwenye greenhouse yangu ni 290,000 (kwa kutumia potting mix) yaani sh 500 kwa mche, na ntakuja kukupandia kabisa kwenye shamba lako baada ya mwezi mmoja....Angalizo: Kuna mbegu nyingi sana za bei rahisi, lakini haziwezi kuzalisha, hata kuthubutu kusogelea uzalishaji mazao wa mbegu hizi maalumu kwa greenhouse.