Jenga Greenhouse kwa gharama nafuu

Jenga Greenhouse kwa gharama nafuu

Namaanisha mbegu, pamoja na dawa za organic zisizo za greenhouse. =mamaNa;8954928]Karibu sana,
Unamaanisha nini sina za outdoor?
Nafanya Drip irrigation installation kwa ukubwa wowote wa shamba, na kukuandalia matuta organically.
Pia natoa ushauri wa kitaalamu na kufanya mpango mkakati wa shamba (farm planning), mfano una shamba lako la heka kadhaa na unapenda kufanyiwa analysis ya nini ulime kwa wakati upi na kwa soko lipi...
Muda si mrefu ntaweka tovuti yetu hewani ili mjionee ni jinsi gani tunaweza kupambana na changamoto za kilimo kwa kutumia teknolojia rahisi kabisa na za bei nafuu.

Karibu sana.
[/QUOTE]

Kila mbegu ya kulimwa nje ina bei yake, Je ungependa kujua bei ya mbegu gani? au unataka miche?
Dawa za organic zisizo za greenhouse za ugonjwa gani? kila zao lina jinsi yake ya kulitibu magonjwa yake.
NB: Kwa maswali nje ya greenhouse, naomba unipigie simu au PM ili tusiharibu uzi huu.

Karibu sana.
 
Namba yangu ni 0714881500,
Karibu sana.

NAI SAVE NAMBA YAKO NA NTAKUPIGIA MWEZI WA NNE,kenya naona hata ufugaji wa samaki wanafanya kwenye greenhouses,samaki wanakuwa under controlled environment,ningependa nijue kama una access na watu wanaouza pond liners,nina bwawa la samaki la mita 20/30 nisingependa kulijengea,
 
Ninayo ndugu, nipigie au pm mahitaji yako.
 
Karibu sana,
Unamaanisha nini sina za outdoor?
Nafanya Drip irrigation installation kwa ukubwa wowote wa shamba, na kukuandalia matuta organically.
Pia natoa ushauri wa kitaalamu na kufanya mpango mkakati wa shamba (farm planning), mfano una shamba lako la heka kadhaa na unapenda kufanyiwa analysis ya nini ulime kwa wakati upi na kwa soko lipi...
Muda si mrefu ntaweka tovuti yetu hewani ili mjionee ni jinsi gani tunaweza kupambana na changamoto za kilimo kwa kutumia teknolojia rahisi kabisa na za bei nafuu.

Karibu sana.

Where the hell were you all these days? Thanks God you are here now watu kama nyie ni adimu sana nchini ntakuwa mteja wako muhimu sana very soon
 
Ukipanda pilipili hoho kwenye green house unaweza kuzivuna kwa muda gani kabla hazijafa na kuhitajika kuzing'oa kupanda zingine au zao jingine? zinachukua muda gani tangu kupandwa hadi kuvuna? Vp soko la Matango kwa Dar liko vp? Je Matango yanachukua muda gani hadi kuvunwa? Ni siku 45 au ?
 
Where the hell were you all these days? Thanks God you are here now watu kama nyie ni adimu sana nchini ntakuwa mteja wako muhimu sana very soon
Karibu sana Ndugu.
Umenivunja mbavu hapa.... Eti where the hell were you!! LoL
 
Ukipanda pilipili hoho kwenye green house unaweza kuzivuna kwa muda gani kabla hazijafa na kuhitajika kuzing'oa kupanda zingine au zao jingine? zinachukua muda gani tangu kupandwa hadi kuvuna? Vp soko la Matango kwa Dar liko vp? Je Matango yanachukua muda gani hadi kuvunwa? Ni siku 45 au ?

Hoho kwenye greehnhouse unaweza kuvuna nyingi kwa mkupuo mara 5 au 6 (approx tani2-3 at once), then utakuwa unavuna kilo 30-50 per week depending on matunzo... Kisha mti ukifikia miezi 9 utaanza kupunguza production. Hoho tunaotesha pembeni kwanza kwa siku 35 na kuhamishia miche kwenye ardhi na zikishatimiza umri siku 90 ndio unaanza kuvuna, utavuna weee mpaka miezi 9 hv kwa kasi kubwa na zitaanza kushuka uzalishaji, zikifikisha mwaka unang'oa na kupanda nyingine.

Matango yanachukua siku 7-10 kugerminate (baada ya kuoteshwa pembeni), kisha unahamishia chini na baada ya wiki 12 utaanza kuvuna. Mwezi uliopita kuna kujana amelima open field na ameuza kiroba kimoja 120,000 kwa bei ya jumla. Soko lipo ni utafiti tu nani wa kumuuzia mengi kwa mkupuo.
NB: Matango huanza kuvunwa yakishatimiza wiki 12 na sio siku 45. Unapolima kwenye Greenhouse tegemea mazao kama hayo chini....
 
Thanks kwa maelezo mkuu inatia moyo sana.
 
mamaNa,

Kuna suala la uchavushaji wa maua (pollination), kwa wengi wetu tumeshazoea uchavushaji unafanywa na wadudu (insects kama nyuki, vipepeo, nk.). Je kwenye greenhouse suala la uchavushaji linakuwaje, maana wadudu hao hawaingii.
 
Kama greenhouse ni kubwa kuanzia robo heka, nyuki (bumble bees) tunawaingiza na kuwafanya waishi humo na watafanya pollination bila matatizo. na kama ni kwa ukubwa huu wa 8*15 basi tutakufundisha jinsi ya kufanya pollination mwenyewe kwa kutingisha maua ya minyanya kwa namna ya kuichavusha, na kama budget inaruhusu kuna vibrator unaweza kutumia kukidhi hitaji hilo. Au electric toothbrush itafaa pia.
 
mamaNa,

Kuna suala la uchavushaji wa maua (pollination), kwa wengi wetu tumeshazoea uchavushaji unafanywa na wadudu (insects kama nyuki, vipepeo, nk.). Je kwenye greenhouse suala la uchavushaji linakuwaje, maana wadudu hao hawaingii.
Point ya msingi sana mkuu
 
mamaNa,

Just in summary!

2.5mil inakusanya nini?

Na nini kiko nje ya hii package ambacho nitatakiwa kuwa nacho? Mi nina shamba tu!!
 
Last edited by a moderator:
Ntakupatia mafundi na muongozo mzima wa kujenga greehouse yako ili kufanikiwa.
Nimekuwa nikitafuta sana habari kuhusu hii kitu. Nashukuru sana kwa kuileta hapa. Naamini umasikini utapigwa teke.

Naomba nikuulize swali la uelewa kidogo mamaNa. Niko sehemu inaitwa Ipinda, Kyela Mbeya. Je, unaweza nipatia mafundi? Kingine ni aina ya miti mnayotumia kujengea, natoa hela halafu wewe unaniletea ama inakuwaje?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu soil analysis na water test wanafanya kupitia lab ya nani??? Mamlaka ya maji pale ubungo wanafanya water test kwa 150,000 na majibu ni baada ya wiki sita. Kenya bei hiyo hiyo majibu wiki moja. Soil analysis nilishaenda mpaka sua, majibu hakuna. ni longo longo kwenda mbele... utakaa hata miezi nitatu usipewe jibu la uhakika... katika suala hili ni bora uingie gharama kwani ndio msingi mzima wa greenhouse unapolala... compitition ya vyakula kwa mimea ni kubwa sana kwenye condensed enviroment... Hivyo ni lazima ujue udongo una mapungufu gani ili uweze kuulisha chakula (fertilizers) zinazostahili... maji pia kama ph level imekosewa unaweza kujikuta unaunguza nyanya zako zote kwa acid na mbolea... kuna mzee hakusikiliza huu ushauri akanunua ya balton, sasa hv kageuza greenhouse yake stoo...
Nb: mafundi wa balton wana install steel tunnels, hawajui wooden ones...
Nimeshapita kote huko na mwisho nimeamua kushirikiana na wakenya....
Kuhusu gharama za films, kuwa makini sana na mchujo wa uv rays, usijekuuziwa nylon...
Otherwise, ni kweli kabisa ukijenga mwenyewe unasave 50%.

Karibuni sana.

Mkuu nimeipanda sana hii technologia yako ya kutumia poles kwani za Balton ni gali sana.
  • Umesema kuna garantee ya kudumu kwa miaka kumi ila hapo nina wasisi kwani hizo nguzo za miti zinaathiriwa na mambo mengi kama mchwa na kadhalika.
  • Je nahitaji niwe na jumla ya shilingi ngapi ili uweze kunipa green house iliyokamilika tayari kwa kuanza kazi maana niliwapigia balton siku za nyuma bei ikanikimbiza.
  • Nimechukua namba yako nitakutafuta; kwa sasa nalima matikiti pale kwala ila ni maono yangu kulima nyanya,matango na hohoo kwani vinalipa sana
 
Back
Top Bottom