Bei iko juu ukilinganisha na ya nani? on each comparison there must be atleast two to compare. Unajua Mita moja ya mraba ya Poly cover inagharimu kiasi gani mpaka inaingia nchini?
Kama kuna cheaper option I suggest you go for it, every penny counts!!. Lakini kumbuka hii ni sayansi (inasomewa) na sio tu ushindani wa bei au kutaka kujilimbikizia faida.
Ikiwa umeshindwa kutofautisha no 2 na 3, sidhani kama utaweza kujenga mwenyewe kwa "Ku unga unga".[/QUOTE]
Hapo kwenye bluu, Bei yaweza kulinganishwa na ya Supplier mwingine!!!!, Lakini pia bei yaweza kulingwanishwa na Materials.
Kwenye Red nilifikiri ungefafanua zaidi kuliko kuanza kukatisha watu tamaa!!
Sasa Mkuu wangu hata material tunayotumia hujaja kuyaona, imekuwaje unajudge ni expensive au bei iko juu?? Supplier hata mmoja Tanzania Hakuna, utareason vipi kuwa kwa supplier mungine inaweza kuwa cheap?, Hivi unajua materials yanauzwaje na yanafikaje nchini kwa kodi ipi? Waliokuja wameona ubora wa materials na ujenzi, pamoja na elimu tosha ya kilimo hiki... Karibu na wewe unufaike.
Pole sana Ndugu Shark kama nimesomeka "Kukatisha Tamaa", maana yangu ilikuwa ni kwamba ujenzi wa Greenhouse unahitaji Elimu ya Kutosha kuhusu, Mazao Yanayopandwa, Elimu ua upepo, Chemistry ya Udongo na Maji, Kudhibiti vihatarishi mbali mbali vya mazao, nk. Hii ni Sayansi na sio tu ujenzi wa kawaida.
Kweli Supplier wanaweza kuwa na bei tofauti lakini kama nilivyosema hapo awali, Sijui Supplier yoyote anayeuza hizi materials Hapa Tanzania. Kwakuwa tunazotumia sisi ni imported kuna mambo mengi sana yanayosababisha bei kuwa kama ilivyo. Kifupi sio kubwa ukilinganisha na ubora wa mazao na wingi utakaokuja kuupata kwa muda lengwa.
Tofauti kati ya Poly cover na insect netting ni UV Polythene Sheets Ni Material maalumu yenye mtazamo wa nylon yanayotumika katika kilimo ili kuchuja jua kwa asilimia kadhaa na mmea utakaokuwa chini yake kupata mwanga wa jua unaostahili (bila kuungua wala kukaushwa au kusababisha high evaporation), Kila eneo lina Sheets zake za kutumia kutokana na kiwango cha jua (inabidi kisomwe), kasi ya upepo, matarajio ya mvua nk.
Na Insect Netting ni Neti Maalumu zinazotumiwa kwenye kilimo ili kuzuia wadudu wa aina fulani, mfano 17 mesh insect netting yenye 70% Micron ni maalumu kwa maeneo yenye white flies wengi na wadudu wanaoruka. Hizi ni neti kama neti za mbu tunazotumia vitandani lakini zenyewe zimetengenezwa kwa plastic na ni kumu sana hata ukipiga jiwe haijachiniki, Ina special treatment inayoua wadudu iwapo watatua juu yake kwa muda fulani.
Nadhani nimeeleweka sasa.
NB: Ili ujenge Greenhouse mwenyewe inabidi uwe umeshasoma vya kutosha haya mambo, sio tu kuweza kujenga kwa kupiga misumari na kufunika nylon, Kila sehemu na aina yake ya material, kila zao na aina yake ya ujenzi, Vitu kama upepo, ventilation, na sun rays ni muhimu sana kuvijua.
NB2: Ni wakati sasa watanzania tubadilike na kuangalia undani wa mambo kisomi zaidi na si tu kuangalia unafuu wa mambo.
Samahani kama majibu yangu yalikukwaza kwa namna moja au nyingine.
Karibu sana.