Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kweli kabisa balton wako juu mno kama kupunguza gharama
ni bora umtafute fundi muajiriwa pale balton umlipe yeye atoe utaalamu tu alafu wewe unamtafutia vijana wa kumsaidia kucompose system nzima.
Vifaa vinajulikana na vinapatikana hapa nchini tena kwa ruzuku ya serikali hata ukitaka kuimport bado bei ni cheap.
kama ni soil analysis na water test maafisa ugani wa serikali wanaifanya hiyo kazi bure labda uwalipe fadhila tu.
Lakini hiyo ni moja kati ya huduma za bure kwa mkulima
Ukifanya hivi unasave zaidi ya 50% ya price ya balton.
MamaNa, nitumie maelezo ya kina pamoja na picha hapa chipuainfo@gmail.com
Nimeshakutumia ndugu
Mkuu natia timu Jumapili kama tulivyoongea. Lakini naomba unitupie material hapa credentobi@gmail.com ili nijenge maswali muafaka nikitoka kukutembelea nikate shauri.
waoooh nice!
Nimeshakutumia, karibu sana.
Kwanini usimwage hapa mkuu kila mtu akafaidika kuliko kutuma kwa email kwa mmojammoja?
nauza materials na kusadia ujenzi wa greenhouse za ukubwa mbali mbali. Kwa sasa nina materials zinazoweza kucover greenhouse ya ukubwa wa mita nane kwa mita kumi na tano (8x15m), zina uwezo wa kuzuia jua, kuzuia wadudu na vihatarishi mbali mbali vya mazao.
Bei ni mil2.5 kwa materials pekeyake yaani 1/8 of an ancre drip lines, polythene cover (uv400 protected sheets), 70% micron insect netting...hizi zitakuwezesha kujenga greenhouse yako bila matatizo. Kitakachohitajika kutoka kwako ni wooden poles (nguzo kama zinazojengewa baa za makuti nk), tanki la lita 500 la maji na maji ya uhakika.
Ntakupatia mafundi na muongozo mzima wa kujenga greehouse yako ili kufanikiwa.
Faida za kulima katika greenhouse ni nyingi mno, ikiwemo matumizi mazuri na sahihi ya ardhi, kwani kiwanja cha ukubwa wa mita 8x15 kinaweza kukupa nyanya hadi tani 30 kwa mwaka, pilipili hoho tani 20 kwa mwaka na mazao mengine mengi yanayolimwa katika controlled environment.
Kuna wataalamu wa kutosha hivi sasa hapa dar es salaam wanaoweza kukupa muongozo, mbegu bora na fertilizers za uhakika.. Tuwasiliane kwa simu namba 0714881500 ili kupeana muongozo..
Karibuni sana.
Ili uweze kufanikiwa katika kilimo hiki, unahitaji maji ya uhakika minimum lita 200 kwa siku kwa ajili ya kumwagilia nyanya kwa matone, nitakupatia mabomba (driplines) zitakazokuwezesha kufanikisha hili.
Nb: Kumbuka greenhouse inajengwa kwenye eneo lililo wazi, lisilo na miti mirefu inayozuia jua...
Pia ni muhimu kufanya soil test na water test ili ujue ni kipi unahitaji kuongeza kwenye ardhi yako ili upate mazao ya uhakika... Naweza kukusaidia kufanya soil na water test kwa gharama nafuu kabisa kutoka nchi ya jirani (kenya). Gharama ni 250,000 kwa huduma hii pekeyake (complete soil analysis & water test).
nb::: Ujenzi wa greenhouse ya mfano umekamilika. Ipo mikwambe kigamboni::: Karibuni sana.
View attachment 140539 View attachment 140540 View attachment 140541 View attachment 140542 View attachment 140543 View attachment 140547
ebwana eb nambiye garama ya mita8 x 8
Hii kitu Green House ni muhimu sana katika mageuzi ya kilimo. Tafadhali usiachie uzi huu tunahitaji mwendelezo ili sote tupate faida.
Gharama 8*8m ni 2.7m all inclusive. Karibu sana
Nb: size inapopungua tegemea na mavuno kupungua pia.
]all inclusive unamanisha nini?
]
Namaanisha Tukiondoka site tunakuachia a fully functioanl greenhouse.
Hiyo Mil2.7 Itanunua material yote (insect netting, poly cover, poles, nails, films etc), Italipa Ufundi, Itanunua tank la maji la lita 500, itatandika drip lines kwenye greenhouse yako, italipa mbolea na matuta. Kitakachobaki ni wewe kuotesha miche ya zao unalotaka na kuhamishia kwenye ardhi na kuendelea kuihudumia mpaka ianze kukuzalia matunda.
Tunaotesha miche kwa gharama nafuu kabisa ya sh 500 kwa mche kwa Mbegu yoyote ya greenhouse. kwahiyo kama unahitaji kupanda nyanya au hoho au matango utatulipa 290,000 extra na baada ya mwezi mmoja tutakuja kukuhamishia miche yako shambani, wewe utakuwa na kazi ya kufungua bomba tu na kuitrain ifate njia yake sahihi.
Kama utaotesha mwenyewe, bei ya mbegu ni 175,000 kwa mbegu 1000, utahitaji trays 10 za kuoteshea zinazouzwa elf 7 kila moja na utahitaji Potting mix inayouzwa 4000 kwa kilo na utahitaji kilo 8. Karibu sana.