Jenga Greenhouse kwa gharama nafuu


Tafadhali msaada wako unahitajika. Nitavipata wapi kwa ruzuku hiyo ya serikali. Mimi nipo Dodoma, asante
 

ebwana eb nambiye garama ya mita8 x 8
 
Hii kitu Green House ni muhimu sana katika mageuzi ya kilimo. Tafadhali usiachie uzi huu tunahitaji mwendelezo ili sote tupate faida.
 
Hii kitu Green House ni muhimu sana katika mageuzi ya kilimo. Tafadhali usiachie uzi huu tunahitaji mwendelezo ili sote tupate faida.

Hakuna shaka ndugu, uzi utaendelezwa kila inapohitajika.
Karibu sana.
 
all inclusive unamanisha nini?
]

Namaanisha Tukiondoka site tunakuachia a fully functioanl greenhouse.
Hiyo Mil2.7 Itanunua material yote (insect netting, poly cover, poles, nails, films etc), Italipa Ufundi, Itanunua tank la maji la lita 500, itatandika drip lines kwenye greenhouse yako, italipa mbolea na matuta. Kitakachobaki ni wewe kuotesha miche ya zao unalotaka na kuhamishia kwenye ardhi na kuendelea kuihudumia mpaka ianze kukuzalia matunda.
Tunaotesha miche kwa gharama nafuu kabisa ya sh 500 kwa mche kwa Mbegu yoyote ya greenhouse. kwahiyo kama unahitaji kupanda nyanya au hoho au matango utatulipa 290,000 extra na baada ya mwezi mmoja tutakuja kukuhamishia miche yako shambani, wewe utakuwa na kazi ya kufungua bomba tu na kuitrain ifate njia yake sahihi.
Kama utaotesha mwenyewe, bei ya mbegu ni 175,000 kwa mbegu 1000, utahitaji trays 10 za kuoteshea zinazouzwa elf 7 kila moja na utahitaji Potting mix inayouzwa 4000 kwa kilo na utahitaji kilo 8. Karibu sana.
 

Mkuu asante kwa ukarimu wako, nilikuja, nimeona na nimejifunza.Naamini nimeanzisha safari ya kuuaga umaskini! Mzee uko njema kwa hiyo kitu, na kikubwa hasa ni uelewa wa kilimo na sayansi yake! Nilidhani ni kajamaa tu kamekutana na teknolojia hii na sasa kanataka tu kupata pesa. UMENIDHIHIRISHIA kuwa uko na kina kwenye kilimo pia!

Acha kwanza nisafishe shamba, maana sasa hivi mawazo yangu yote yako hapo kwenye habari ya greenhouse na possible faida zake.

Soon utapokea simu yangu, tayari kwa kazi.
 
Powa so mi nko Arusha, shamba liko na mazao sm by May tutafanya dil count me in
Ankojei
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…