Wakuu zangu,
naona bado mnajadili swalai la ununuzi wa jumba hilo la Ubalozi..
Kwanza kabisa navyofahamu mimi Marekani na nchi zote zilizobobea Uibepari, huwezi kununua nyumba kwa cash money yaani ulipe zote billioni 10 kwa sababu uuzaji wa nyumba hutegema interest inayokusanywa kwa kila mwezi na mara zote transaction ni lazima zipitie financial institution kisheria kutokana na michezo ya money laundry, hakuna exceptional wala untouchables ktk sheria za wenzetu..kumbukeni tu wenzetu wana system nzima inayo monitor mabadilishano ya fedha kati ya muuzaji na mnunuzi. Unaweza kulipa sehemu kubwa kama down payment ili kupunguza urefu wa miaka ya mkopo lakini mara zote inerest zao hubakia pale pale ktk hesabu zao kinachobadilika sana ni miaka ya ulipaji...
Kwa hiyo hata kama utakuwa na cash Us millioni 10 ni vigumu na pengine haiwezekani ukanunua nyumba kwa cash money kama tunavyofanya Bongo chini ya mpango wa Mkapa anayesifiwa kwa kuweka misingi bora (my a...) ya ukusanyaji fedha wakati nchi nzima vitu vinauzwa kwa Dollar na unaweza kwenda ka kapu la fedha benki usiulizwe umezipata wapi, zimelipiwa kodi au maswali mengine. Ndio maana watu wengi hushangaa kuona celebrity wa Marekani wakifilisiwa nyumba na magario ya kuchukuliwa..Ni sheria za mortigage na leasing zinazowabana kutonunua cash kwa sababu benki zinavuta interest na serikali inavuta kodi zake toka pande zote kwa transaction zote za kupokezana fedha kila mwezi.
Pili, inaonyesha watu wana wasiwasi na gharama za Ukarabati, hii sii kitu kwa nchi za Kibepari, mara zote Mpangaji hubeba mzigo wote yaani unapopanga nyumba mara nyingi unalipia gharama za ukabrabati, maji, umeme na ghasia zote ikiongezewa ka asilimia 10 hadi ishirini juu yake. Kwa hiyo malipo ya mwezi kwa hizo ghorofa tatu nyingine inaweza kabisa kukabiri matumizi na kodi zote kisha tukabakia na kitu kidogo pamoja na thamani ya mjengo kuongezeka kila mwaka..
Labda tatizo ambalo naliona mimi ni moja tu.. tanzania ni nchi huru ambayo kulingana na sheria za UN, jengo hilo litawakilisha nchi yetu yaani Tanzania..Sasa sielewi ikiwa kuna mtu mpangaji akifanya fujo, wizi au lolote lile itakuwa ndani ya serikali yetu au ya Marekani? Na Je, mtu akitaka kujisalimisha ktk Ubalozi wetu ni eneo gani linahesabika kuwa milki ya Ubalozi wetu ikiwa jengo hilo hilo lina wapangaji...nimesikia swala hili limewahi kutokea ktk ubalozi wa Uganda ingawa sifahamu kisa haswa kilichotokea..
Nje ya hapo, wakuu zangu hakuna investment yenye uhakika kushinda nyumba na msije changanya nyumba za kuishi na haya majengo ya highrise mijini kwani ktk mtikisiko huu wa uchumi nyumba nyingi za makazi (watu binafsi) zimeshuka thamani lakini sii nyumba za upangishaji wala highrise office buildings katikati ya mji...sidhani kama mmeona jengo kubwa likiwekwa mnadani - for closure.