Jengo jipya la ubalozi DC - Dola milioni 10?


I couldn't agree with you more. Give credit where it's due. Your last sentence (in red) is full of wisdom. Feels relief to see other great thinkers taking a positive note on some issues.
 
 
 
Sasa tunalo hilo jengo la ghorofa 6, what's next? Au ndio tumempakaa nguruwe lipstick?

Watendaji ni walewale na performance yao ni hilehile.
 
 
10billion ? No wonder Obama anamvuta JK ubavuni kwake kila saa anajua analo lifanya .
 
Mnakumbuka scandal ya Dr Costa Mahalu na ofisi ya ubalozi Italy,waliponunua kwa bei ya juu na ufisadi?Hatujui sh ngapi zilitumika kuhamisha ubalozi wa Uingereza kutoka ofisi ya zammani kuja mpya!

Hizo billioni zingetumika kujenga shule hii:
Fidel80
Today, 03:37 PM


Ni kawaida kuona wanasiasa wakiwarubuni wananchi kwa kuwapa maneno matamu sana na yenye matumaini hapo mbeleni. Lakini cha kushangaza utekelezaji wake ni karibia na kipindi cha uchaguzi ndo utaona hao jamaa wapo busy sana kuboresha vitu napo kwa kulipua.
Sasa hili Taifa la kesho linaweza kujengwa kati hali hii?
JK tembeza bakuri basi angalau Taifa la kesho lisikalie vitofauri na kukaa kwenye madarasa ya vumbi kama hili. Elimu ni jambo la msingi kwa binadamu kuliko bakuri unalo tembeza la vyandarua ambavyo vinaishia wa wajanja wachache na wewe ukiwa kimya.
Ukiwa kama mkuu wa kaya kuna changamoto kubwa mbele yako inua Elimu.
__________________
Utamu wa pilipili ni muwasho wake :-D
 
Hata kama ni investment nzuri, utakuja kusikia hela zilikuwa zinaingia kwenye private accounts za waheshimiwa. Ndo hapo chacha
 

mheshimiwa unataka kugeuza ubalozi kuwa shule ya kujifunzia kiswahili,
du tafadhali..
 

Nakubaliana nawe mkuu, kama kuna ufisadi hapo sasa sijui lakini kama zilikuwa ni jitihada za dhati za kuwa na jengo lenye nafasi kwa ajili ya ubalozi nadhani ni uamuzi mzuri.
 
 
 
Mgonjwa Ukimwi,
Mkuu,
Fedha halali haikataliki hata siku moja. Hakuna nchi inayokataa fedha halali. Hakuna benki inayokataa fedha halali. Hakuna financial institution duniani inayokataa fedha halali. Hakuna muuzaji anayekataa fedha halali.

Mkuu nadhani tuachie hapo maanake imekuwa taabu...
Sikuandika sehemu yoyote ile kwamba Bank au financial institution zinaweza kataa fedha halali... sielewi hili umelitoa wapi? isipokuwa nazungumzia ununuzi wa Mjengo Marekani au nchi za Kibepari..Umeshindwa kuelewa kwamba hata hizo Bank na Financial Institution zinafanya biashara pia kwa hiyo hawakai fedha yako ila wanakataa biahsara isiyokuwa na faida kwao..Kila transaction wanayoifanya wanatafuta kuvuta chao na sii kazi ya kanisa...Mfumo mzima wa Kibepari ni mgumu kuliko unavyofikiria lakini rahisi sana kiutendaji kama utaelewa unavyofanya kazi.
Tanzania tuna cash kibao lakini hatuwezi kununua mitambo kama ya Barricks ya kuchimba dhahabu..Trust me, hatuwezi kuuziwa hata kama tunayo cash bank....tunataka sana tuyachimbe madini yetu sisi wenyewe lakini mfumo mzima unatuweka kati hatuwezi kufanya tunavyofikiria au kupanga.
Kwa hiyo sijasema sheria za US zinamkataza foreigner kununua nyumba au kukataa fedha yetu isipokuwa utaratibu wenyewe unakulazimisha kuingia mortgage hata iwe kwa miaka michache pamoja na kwamba unayo cash mkononi..
Imewatokea watu wangu wa karibu na sii kitu cha kusimuliwa..wewe umesimuliwa na rafiki yako, I was involved in the process.. maadam 99% ya mijengo unayoyaona city centre kwa maghorofa yapo ktk mikopo (mortgage) ni vigumu kuepuka hesabu za Bank ktk makadirio ya kile watakacho kivuta toka kila nyumba...Nina hakika kama kweli inawezekana hivyo ulivyosema, basi nyumba ya thamani ya Usd millioni 7 ndio utauziwa kwa Us millioni 10 kwani wenzako wameisha piga mahesabu ya miaka 20 ijayo watavuta ngapi toka jumba hilo la ghorofa 6..
 
 

....wewe Bob kama hujui kitu bora ukae kimya au uliza, maana haya mambo unayoongea yanasomwa na watu wengi sana,kukuita muongo nitakuwa rude lakini kitu ulichoandika hakina ukweli hata kidogo,FYI nina uzoefu na hizi financial institution zinavyofanya operate may be kuliko governor wako wa BOT!
 

Hakuna haja ya kurushiana madongo.. wewe nambie kile nisichokijua maanake nimetumia experience yangu mimi...nipo hapa kujifunza kama wengineo maanake somo moja lakini edition zinaweza kuwa nasoma ilopitwa na wakati..kisha sio tu maadam Mkandara kaandika basi ndivyo ilivyo...
Na sidhani ktk swala la madini nimezungumzia financial institution isipokuwa utaratibu wa kununua mitambo ya kuchimba madini kama ya Barricks..
Tunaihitaji sana mitambo hiyo, tunao vijana wamesomea madini na bila shaka asilimia 80 ya wafanyakazi pale Barricks ni Watanzania...Kwa nini tumeshindwa kununua mitambo yetu ssi wenyewe!
Unataka kunambia kweli ni Uongozi wetu ndio hawajui la kufanya?
 
Mgonjwa Ukimwi,
Umeshindwa kuelewa kwamba hata hizo Bank na Financial Institution zinafanya biashara pia kwa hiyo hawakai fedha yako ila wanakataa biahsara isiyokuwa na faida kwao.

Hapa mkuu naona tu unataka kuendeleza mjadala. Na mimi nitaufunga kwa kusema haya machache kuhusiana na nukuu yako hapo juu.

Mkandara unachanganya mambo hapa. Ununuzi wa nyumba unafanyika kati ya muuzaji na mnunuzi. Benki inahusika tu katika kufacilitate transcation kutoka katika account ya mnunuzi kwenda katika account ya muuzaji. Hapa benki kisheria HAINA BIASHARA.

Biashara ya benki inatokea tu pale mnunuzi anapoomba mkopo kwa kutokuwa na fedha za kutosha kumlipa muuzaji. Hapa ndipo benki inapofurahia kwani imepata biashara. Ukiwa na fedha tasilimu benki ambazo umezipata kwa uhalali, benki haina uwezo wa kukufanya usinunue nyumba.

Mkuu naona kwa makusudi mazima unataka kupotosha wasomaji kwamba ukiwa na fedha tasilimu halali kwenye account yako, benki watakataa kufanya biashara na wewe ati kwa sababu haina faida kwao kama ulivyodai kwenye nukuu hapo juu. Yani benki itakataa kumlipa muuzaji fedha ambazo wewe mwenyewe umeziweka? Benki inaingilia vipi matumizi ya fedha zako?

Anyways, kwangu hii topic na ununuzi wa nyumba kwa fedha tasilim naifunga na niliona vyema kurekebisha pale ulipokosea.

Mkuu wangu, tutakutana kwenye mjadala mwingine
 

Mkuu naona mgonjwa kakujibu kila kitu na sina cha kuongeza na pls usichanganye topic hapo na sisi kutoweza kununua mitambo kama ya Barrick....kuna kitu kinaitwa transfer of technology,ni kweli kuna vitu huwezi kununua hata kama una pesa,lakini sana sana hii ni kwenye mambo ya silaha,anyway hiyo ni topic nyingine lakini sina uhakika kama mitambo ya kuchimba madini ina fall humo
 
si rais alisema wezi wa epa walirudisha over $60 million, sasa si walitumia kidogo from that kununua jengo...the rest will go to pay the $30,000 a month maintenance cost for a couple of years 🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…