Bw Magezi kwanza naomba usichukulie kwamba anacho fanya kikwete ndicho kinachopingwa, kwani hata cha nkapa kuuza nyumba za serikali kinapingwa kununua ubalozi italy kwa kuongeza cha juu kinapingwa na hata ofisi ya ubalozi uingereza kunaweza kuwa na madudu ingwa hayajaibuka nk nk.
Sasa tukirudi kwenye hili jambo, wewe ukiwa ni mtu mwenye akili ni lazima una mahitaji ya nyumba, sasa suala linakuja unataka nyumba ya choo kila chumba au yenye ya kawaida yenye choo kimoja, au ya kati yenye choo extra kwa master bedroom tu. Sasa uamuzi wako wa busara utatokana na uwezo wako wa kifedha na mambo mengine ya kimsingi kama eneo, usalama na shughuli unazotaka kufanya.
Sasa baada ya utangulizi huo tuje kwenye hili jambo, kwanza tunasikia tulikuwa na jengo la zamani, sasa sijui kwanini waliliuza na kununua hilo, aidha lilikuwa halitoshi , na pili jee tulio liuza tulipata fair price au huku tunaliwa na kule tunaliwa.
halafu linakuja hiyo busara ya kulinunua hili la sasa je ni wa busara, na je bei ni halali , na hiyo paper iliyo kwenda kwa waziri mpaka baraza la mawaziri mpaka kwenye budget inasemaje? maana najua utayarishaji wa budget mpaka inapopita na mpaka utekelezaji muda utakuwa umepita, sasa na hii economic recession bei kweli haijapungua, je mahitaji yetu ni ya hilo ghorofa nk nk.