Jengo jipya la ubalozi DC - Dola milioni 10?

si rais alisema wezi wa epa walirudisha over $60 million, sasa si walitumia kidogo from that kununua jengo...the rest will go to pay the $30,000 a month maintenance cost for a couple of years 🙂
.....sasa kuna hii issue ya BAE(rada)sijui atatwmbia nini tena maana kesi ishawiva huenda ikapelekwa mahakamani soon!!
 
Mkuu MgonjwaUkimwi kanijibu kitu gani?.. alivyosema kuuza nyumba ni kati ya mwenye nyumba na mnunuzi ati benk haina nafasi?..
Sii kweli kabisa kwa sababu majengo yote unayofikiria kununua hapo DC mjini yana mortgage, hakuna mtu anajenga au kununua nyumba kwa cash...na waliomaliza malipo utahesabu kama wapo.
Hii imemtokea mshikaji wangu mmoja alotoka huko bondeni kaingia na vijisenti vyake akauvaa mkenge kununua gari (Range sports) ambalo lipo bado ktk lease... Siku alipotaka kulisafirisha Bongo alipigwa chini kwa sababu Mnigeria aliingia mitini bila kulipa fedha za gari hilo kwa sababu kisheria halikuwa lake..
Hivyo, sikuwa na maana nasi tumefanya hivyo ktk kununua jengo hilo lakini ni ktk kukuonyesha kwamba mfumo wa huku bank na Financial institution zimeingia ktk kila biashara na zina control kwa kiasi kikubwa sana. Wewe unapokuwa na cash haina maana kwamba kila kitu kitakuwa rahisi kwako inatregemea pande zote mbili zimejengekja vipi na kuna utaratibu gani kisheria.
Somehow, hawa jamaa hutafuta njia za kuvuta service na interest zao, ndio maana ni vizuri sana kuwa na wakili wa Real estate na hata kama inawezekana tumenunua kwa cash basi nimesema its beneficial from a seller's point of view.

Kila jengo unaloliona limesimama mjini mkuu wangu kuna Financial Institution nyuma yake hivyo huyo mwenye nyumba ana mdhamini..Watu wanakufa hawajamaliza malipo hivyo ukinunua kwa cash bado Financial Institution itahusika kwani wao ndio wenye title deed..
 

Mkandara:

Unaweza kutumia cash. Lakini matumizi ya Cash yanapunguza mzunguko wa pesa katika real estate na uchumi wenyewe.

Kama ningekuwa mnunuzi wa nyumba hiyo. Ningelipa downpayment ya laki 5 na kuiwekea nyumba insurance ya nyumba na insurance ya mortgage yenyewe. Insurance ya nyumba ingesaidia pale maafa yanapotokea. Na insurance ya mortgage ingesaidia pale nitakaposhindwa kulipa.

Na pesa iliyobaki kama milioni 9.5 ningeifanyia mzunguko wa maana kwenye investments.
 
https://www.taxpayerservicecenter.com/RP_Detail.jsp?ssl=0050 0025

they got it for that price they said and here is the value of the building the link above have details on the sale and the value. so hakula mtu (unless labda zilitoka mil 11 hazina)
maybe the debate could be, was that particular building necessary, maybe that was the best suited for the needs, tourism is growing, maybe they are increasing staff at the embassy, who knows...




 
 
 
Tunaomba picha za hilo jengo kwa aliye huko
 
 
Hivi Bunge liliidhinisha hayo matumizi ya $10.5 million ili kununua jengo hilo? Au ni nani aliyeidhinisha matumizi hayo? Je, mbona habari hii ya kununua jengo hilo ilifanywa siri kali mpaka baada ya kununua jengo hilo ndiyo Watanzania tumefahamishwa? Hapa kuna harufu kali sana ya ufisadi.
 
MODS,

Nashangaa hiyo picha hapo inaonekana imewekwa nami wakati mimi sijaiweka picha hiyo. Mimi niliweka picha ya darasa toka gazeti la This day. Je, kulikoni na hiyo picha?


Babu something is not right, jana ilikuwa ukim-quote mtu, jina linatoka la mtu mwingine kabisa.

MJ
 
Jengo la ubalozi wa zambia lililoko sokoine drive dar es salaam lina wapangaji wa kawaida; hivyo si ajabu kwa ubalozi kupangisha kama mmoja wetu alivyohoji hapo nyuma
 
Jengo la ubalozi wa zambia lililoko sokoine drive dar es salaam lina wapangaji wa kawaida; hivyo si ajabu kwa ubalozi kupangisha kama mmoja wetu alivyohoji hapo nyuma

Kudos Edo

Achana na yule Mbwiga.
 
Babu something is not right, jana ilikuwa ukim-quote mtu, jina linatoka la mtu mwingine kabisa.

MJ

Inawezekana MJ, lakini kuhusu hiyo picha nimegundua kwamba niliweka link toka gazeti la This Day, leo ile picha ya darasa wameiondoa na kuweka picha nyingine kwa kutumia link ile ile ndiyo maana ile picha niliyoiweka ikapotea na kuwepo na picha ambayo mimi sikuikusudia kuiweka hapa. Nimeshaifuta ile picha na bandiko langu kwa MODS.
 


Poa mkuu.

Tuendelee kumkoma nyani usoni.

MJ
 
Kudos Edo

Achana na yule Mbwiga.

Kama yule ni Mbwiga basi wewe Simbwiga!! Sisi tunazungumzia balozi ambazo haziwezi kucompromise mambo yake ya usalama ndio maana ya reputable embassies; nadhani ile yetu ya Washington ina hadhi hiyo!! Sasa kama wazambia wanapangisha Clearing and forwarding agents basi hawamo katika kundi la balozi zenye hadhi tunazoelezea!!
 
Kudos Edo

Achana na yule Mbwiga.
Unajua Zambia walinunua hilo Jengo mwaka Gani? je Threat ya terrorism ilikuwaje wakati huo? Unajua hali ya Uchumi wao wakati huo ilikuwaje? na Sasa ikoje, mimi sitatumia maneno ya kijinga maana watu watashindwa kuelewa Mjinga ni Nani.
 
Unajua Zambia walinunua hilo Jengo mwaka Gani? je Threat ya terrorism ilikuwaje wakati huo? Unajua hali ya Uchumi wao wakati huo ilikuwaje? na Sasa ikoje, mimi sitatumia maneno ya kijinga maana watu watashindwa kuelewa Mjinga ni Nani.


August,

Yaani huyu anataka kuwafanya Wazambia kuwa ndio yardstick yetu kweli? Nikisema mediocrity inatawala hapa mtasema natukana?
 
Sina imani sana na mambo ya serikali kwani ufisadi haujashughulikiwa na hivyo basi ufisadi bado ni possible kuendelezwa na viongozi wetu...Kagoda fedha zilitolewa kwa madai ya investment kwenye kilimo,zikwapi? Hatujui kuwa fedha za ununuzi wa jengo hilo zimetoka wapi,wengine wanasema ni za ubalozi. Tunapochemsha sisi ni kwamba hatuulizi,wenzetu hata pesa za vita huwa wanaulizwa viongozi kwamba watazitoa wapi,transparency ni muhimu hapa,serikali imetoa wapi hizo fedha?

Pili je dhumuni lilikuwa ni uwekezaji ama kupata jengo la ubalozi? Hapo ndipo mjadala uanzie,tusichanganye issue ya kupata mahali pa kufanyia kazi za ubalozi na issue ya investment,hizo ni two separate issue kwasababu sidhani kama walihama hapo walipokuwepo kwasababu labda ni jengo baya ama halikidhi mahitaji ya matumizi....Nadhani uamuzi huo wa kununa jengo ulilenga zaidi kwenye kuinvest zaidi ya simply kupata jengo la matumizi,madai yakiwa kwamba ni bora kuinvest kwani still wanalipa kodi,ninavyoona inawezekna ni watu binafsi tu wamewekeza kwa kutumia mwavuli wa serikali kwani bado sioni kama investment hiyo itamnufaisha vipi mtanzania given the fact kuwa bilioni 10 ni ndogo kwa wengine,ila bado kwa wenye pesa hizo(watanzania)ni nyingi sana na zingeweza kutumika kwa priorities za tofauti,unless tuambiwe kuwa mapato ya ubalozi yanatumika kwa shughuli za ubalozi pekee na si vinginevyo...Tuelewe kwanza mfumo wa usimamizi wa fedha wa balozi zetu na kama balozi zetu zinatumia fedha za kodi ama zinajiendesha zenyewe,kama zinatumia pesa za kodi then ni kivipi mwananchi atanufaika?na kama hawatumii fedha za kodi then hiyo si investment ya serikali ni ya watu binafsi ama ya taasisi inayoitwa "Ubalozi"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…