Mkuu MgonjwaUkimwi kanijibu kitu gani?.. alivyosema kuuza nyumba ni kati ya mwenye nyumba na mnunuzi ati benk haina nafasi?..
Sii kweli kabisa kwa sababu majengo yote unayofikiria kununua hapo DC mjini yana mortgage, hakuna mtu anajenga au kununua nyumba kwa cash...na waliomaliza malipo utahesabu kama wapo.
Hii imemtokea mshikaji wangu mmoja alotoka huko bondeni kaingia na vijisenti vyake akauvaa mkenge kununua gari (Range sports) ambalo lipo bado ktk lease... Siku alipotaka kulisafirisha Bongo alipigwa chini kwa sababu Mnigeria aliingia mitini bila kulipa fedha za gari hilo kwa sababu kisheria halikuwa lake..
Hivyo, sikuwa na maana nasi tumefanya hivyo ktk kununua jengo hilo lakini ni ktk kukuonyesha kwamba mfumo wa huku bank na Financial institution zimeingia ktk kila biashara na zina control kwa kiasi kikubwa sana. Wewe unapokuwa na cash haina maana kwamba kila kitu kitakuwa rahisi kwako inatregemea pande zote mbili zimejengekja vipi na kuna utaratibu gani kisheria.
Somehow, hawa jamaa hutafuta njia za kuvuta service na interest zao, ndio maana ni vizuri sana kuwa na wakili wa Real estate na hata kama inawezekana tumenunua kwa cash basi nimesema its beneficial from a seller's point of view.
Kila jengo unaloliona limesimama mjini mkuu wangu kuna Financial Institution nyuma yake hivyo huyo mwenye nyumba ana mdhamini..Watu wanakufa hawajamaliza malipo hivyo ukinunua kwa cash bado Financial Institution itahusika kwani wao ndio wenye title deed..