Jengo la ghorofa lililokuwa likijengwa limeanguka katika Barabara ya 9, eneo la Eastleigh, Nairobi, Ijumaa, Oktoba 23, 2026, huku hofu ikitanda kuwa baadhi ya watu huenda wamenasa kwenye kifusi. Idadi ya watu walioathirika bado haijathibitishwa.
Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo lilisababisha vurugu eneo la tukio, huku baadhi ya watu wakiripotiwa kuanza kupora mali. Ambulensi pia ziliripotiwa kushambuliwa kwa mawe, hali iliyochelewesha kwa muda juhudi za waokoaji kufika eneo hilo.
Polisi waliofika eneo hilo walitumia vitoa machozi kutawanya umati uliokuwa umekusanyika.
Taarifa zaidi kuhusu walioathirika na juhudi za uokoaji zinatarajiwa kutolewa kadri tukio hili linavyoendelea kufuatiliwa.
Source : Citizen digital