Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya Tandahimba linaungua moto!

Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya Tandahimba linaungua moto!

gambachovu

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2011
Posts
1,854
Reaction score
292
Chanzo cha moto kitajulikana hapo kesho..
(shoti ya umeme huenda)

Ila,baada ya jengo hilo kuungua kwa muda,umeme ukakatika..

Askari wanapatrol mitaani na kupiga mabomu kutuliza ghasia..

Jirani na ofisi hiyo pana maduka ya wafanyabiashara,ambao huenda maduka yao yakaathirika kwa moto huo,maana huduma za kuzima mioto mawilayani,ndiyo hivyo tena..

2230.....
Hakuna taarifa juu ya kudhibitiwa ama kutodhibitiwa kwa moto huo hadi sasa,wala hasara iliyopatikana..

Updates zaidi kesho..
0605hrs:

Inasemekana maduka yote yameteketea kwa moto ulioanzia kwenye ofisi ya OCD.. Maeneo hayo ni jirani na soko,hivyo mabanda mengi ya biashara yameathirika!

-Watu wameanza safari kwenda vijijini na sehemu nyingine za jirani

- Kwa wenye ndugu,wasio na ndugu wamepanda basi la Dar..

0700hrs
- Yasemekana chanzo cha moto ni hujuma!
-Baadhi ya familia zaomba hifadhi kituo cha Polisi(kwa OCS) ambako kuna ukumbi mkubwa wa canteen unaotumika kwa sherehe na vinywaji baridi na vikali...

1320hrs:
- Helikopta ya Polisi inarandaranda juu..

1800hrs:
-Afande Paul Chagonja amefika,amekagua madhara ya moto kwenye ofisi ya OCD na maduka ya wafanyabiashara. Hii ni ikiwemo gari aina ya Suzuki Escudo ya mfanyabiashara aliyekuwa kaipaki barabarani akijaribu kuokoa mali zake,na kuja kuikuta inateketea.

-Amesikiliza kilio cha baadhi ya wafanyabiashara juu ya hasara waliyoipata,na vipigo vilivyoambatana nayo..

-Baadhi ya raia waliokuwa wamekimbilia vijiji jirani wamerudi kuangalia maafa,na hivi giza linapozama,nao wanarudi vijijini kwani hawajajihakikishia usalama wao bado!
Wengine ambao leo hawakupata usafiri,wanatarajia kuondoka kesho...

0615hrs:
-Kamishna wa Polisi Paul Chagoja,jana aliitamka namba yake ya simu ya kiganjani kwa yeyote mwenye taarifa kuhusu vipigo na mioto. Akaomba mtu awe huru kubeep,kutuma ujumbe,kumpigia,na kama hatakuwa na woga,basi leo(Alhamisi) aongee naye ana kwa ana madhila waliyopata raia,naye atazipokea na kutafuata namna ya kuzifanyia kazi.

1950hrs
-Jopo lililokuja na kamanda Chagonja limeshinda likihoji wafanyabiashara waathirika mmoja mmoja..
-Siku ya Ijumaa saa 4 asubuhi,kikao kimeandaliwa na Diwani wa kata,akishirikiana na uongozi wa chama tawala na serikali wameandaa mkutano wa wananchi wote ili kuwekana sawa juu ya amani ya mji wa Tandahimba,na vitongoji vyake.....
Gee Cee
 
Pole kwa askari wetu na tafadhali tunaomba mliopo karibu mshiriki kuokoa maisha watu waliopo kwenye jengo hilo mfano mahabusu na mali ya serikali hasa bunduki
 
mkuu tupe stori nzuri kuhusu hizo ghasia

Ghasia ilikuwa ni kwa watu kujaa eneo la tukio kitu ambacho kinahatarisha hata usalama wa vifaa,samani,nyaraka,n.k.

Ila tunadhani ni ajali ya shoti ya umeme.. Kesho tutakuwa na habari zaidi za uhakika..

By Gee Cee
 
Samahani bana; hilo jengo ni la ofisi yake binafsi au ofisi ya serikali(Kituo cha Polisi)?
 
Pole kwa askari wetu na tafadhali tunaomba mliopo karibu mshiriki kuokoa maisha watu waliopo kwenye jengo hilo mfano mahabusu na mali ya serikali hasa bunduki

Hiyo kazi itafanywa na askari wenyewe mkuu..

Halafu,jengo la OCD liko mbali kama Km 1 hivi kulifikia la OCS ambalo ndilo hutunza ammunition na mahabusu..

Kwa sasa raia wamejifungia ndani,kwa maana askari hawataki vikundi mitaani(labda kwa sababu za kiintelijensia)na kuna kamvua kananyesha muda huu..

Ila amri ya mabomu naona imekwishasitishwa..
 
hiyo kazi itafanywa na askari wenyewe mkuu..

Halafu,jengo la ocd liko mbali kama km 1 hivi kulifikia la ocs ambalo ndilo hutunza ammunition na mahabusu..

Kwa sasa raia wamejifungia ndani,kwa maana askari hawataki vikundi mitaani(labda kwa sababu za kiintelijensia)na kuna kamvua kananyesha muda huu..

Ila amri ya mabomu naona imekwishasitishwa..

afadhali kama mabomu yamesitishwa!
 
Kinachoshangaza askari wanapiga mabomu! kulikoni hapa jamani? MOTO halafu MABOMU!?

In Tanzania if you are not confused, then your head is not working properly.

Moto, hakuna zimamoto, wananchi wanakuja kusaidia, polisi wanawatanya wananchi na mabomu!!!!!!!!!!!!!!!

God have mercy on this country, what have we done to you to deserve this!!!!!!!!!
 
Huenda yalikuja na FFU wiki iliyopita walipokuja kutuliza ghasia..(hata hivyo hawajaondoka bado)
 
Sasa yaweza kuhisiwa na kuhusishwa na yaleyale madai ya wananchi ya korosho..
 
Bora angeungua tu na huyo OCD kwani amekuwa kikwazo kikubwa kwa wananchi pindi wanapodai haki zao.
 
Habari toka TBC1 (Jambo Tz) zinasema kuwa wananchi wenye hasira kali wamechoma Kituo cha Polisi moto! Habari zaidi Marin Hassan amedai zitafuata!
 
Polisi wakishindwa kufanya kazi, wananchi wanachukua jukumu. Hii ni hatari sana kwa nchi yetu.
 
Back
Top Bottom