Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Nimefika Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora, kuna jambo limenisikitisha na baada ya kuwauliza Wenyeji, nguvu ndio zimeniisha kabisa.
Nimeambiwa huu sasa ni mwezi wa pili na nusu kuna jengo la Walimu katika Shule ya Msingi Nsololo halijarekebishwa baada ya paa lake kuezuliwa na mvua, hivyo Walimu kukosa sehemu ya kukaa.
Nilifika hapo kumtembelea ndugu yangu anayesoma katika shule hiyo na akanieleza kuwa Walimu wamekuwa wakikaa kwenye miti wakati wanaposubiri wenzao wamalize vipindi.
Nilipofuatilia zaidi nimebaini kuwa hakuna jitihada za msingi zilizofanywa licha ya kuwa Viongozi wa ngazi ya Wilaya wanajua kinachoendelea.
Hivi Ofisi ya Mkurugenzi wa Nachingwea haioni kinachoendelea? Vipi kuhusu kile kitengo cha maafa, nini kinaendelea? Hii sio sawa.